kibangubangu
JF-Expert Member
- Dec 10, 2018
- 272
- 353
SEHEMU YA 1
Danieli aliingia bila hodi,nyumbani kwa mpenzi wake alichokiona mbele ya macho yake aliamua kuyafumba, huku mwanaume aliyembele yake akiokota nguo zake kwa haraka zilizotapakaa sakafuni ili kujifunika.
Kabla hajafumbua macho,alisikia sauti ya mwanaume huyo aliyeonekana kumfahamu ikimwambia “Nisamehe kaka pole sana jamani” alisema mwanaume huyo huku akitoka nje ya chumba hicho kwa kasi ya ajabu.
Kitandani alikua amebakia msichana mrembo,akiusitili mwili wake kwa shuka lililolowa jasho la purukushani za tendo la uzinifu.
Hakuweza kukutana na macho ya mpenzi wake ambaye alikua mbele yake...Daniel kifua chake kilikuwa kinawaka moto na koo lake lilikuwa likiganda kwa maumivu ya mwanaume harisi yenye hasira zisizo elezeka...
Alikuwa amefadhaika kihisia,hata hivyo, alivuta pumzi ndefu na kuishusha taratibu,akamwita
Graceeeeeeeeee.........!!!!!!!!!????
Grace hakujibu kitu huku akijikunja pale kitandani kama,chatu aliyekamata windo au kamba ifungayo mzigo,akifunika uso wake ulio jaa woga na aiibu kwa mikono yake inayo tetemeka ila yenye kucha ndefu za urembo.
"Grace"......... aliita tena ulinifanyia nini nikakusamehe? Unawezaje kunifanyia tena? Je, hii ni laana au kitu gani? Je, Musa si X wako,imekuaje unaruhusu tena anakuchezea heshima yako na yangu?!,na kudharirisha kimapenzi?”
"EEEEEhhhh Mungu nisaidie nisichanganyikiwe"
Daniel alisali asipoteze akili.
Grace akafungua kinywa chake kwa sauti ya chini na woga akasema "Sama.....Samahani mpenzi wangu"
Midomo ya Daniel ilitetemeka na kilio kilimtoka huku akimtizama mpenzi wake kwa uchungu,"Unasema samahani???!", alifoka
kwasira kali na chuki zilianza kumwagika kwenye mishipa yake,kama sumu ya nyoka koboko ingiapo katika mishipa ya kiumbe hai..
Daniel akashika kiti cha plastiki kilichokuwa karibu na T.V na kukibamiza ukutani. Kiti kilivunjika vipande vipande na kikitoa sauti za midondoko ya vipande vyake katika sakafu.
Samahani Daniel tafadhali…..” Grace alilia huku akimsogelea Daniel lakini jinsi Daniel alivyokuwa akimtazama Grace kama chui akaamua kurudi nyuma.
Uliomba msamaha mara ya kwanza,na ya pilli na sasa unataka msamaha tena...?!"
Grace akanyamaza na kukaa mwisho wa pembe ya kitanda huku macho yake yakiwa yamemtoka kwa kuchanganyikiwa.
"Pole sana Danie tafadhali..." Alilia kwa kwikwi.
“Tatizo lako ni nini hasa Grace”? Kwa nini unapenda kuniumiza sana? Hivi mimi kukupenda ni hatia!???Huu ni mwaka wa tatu wa uhusiano wetu!
Na umeamua leo unisaliti siku ya kumbukumbu ya uchumba wetu unajua leo nilikuja kwa kustukiza,unajua nilikua nakuja kukufanyia kitu gani msaliti wewe? ”
Dani aliingiza mkono mfukoni mwake na kutoa kisanduku…. Tazama… nimesema tazama juu!” Akamwita Grace!
Grace Alishtuka alipoona kisanduku cha pete… midomo yake ilitetemeka…..
Akasema “Daniel….. Tafadhali nisamehe mara hii ya mwisho, ninaahidi haitatokea tena” aliomba msamaha huku akitokwa na machozi.Daniel alicheka kwa uchungu na kusema "kwani mimi ni mjinga, siyo?"
Grace alisimama kwa woga, shuka likidondoka na kudhihirisha mwili wake kuwa ulikua upo uchi huku akimkimbilia na kumrukia Daniel na kumng'ang'ania kama gundi.
Grace alipomkumbatia akasema "Daniel...Si unanipenda...au... hunipendi akimtizama machoni....
Daniel huku akitabasamu kwa hasira, aliinamisha kichwa chake upande wa kushoto na kurudisha macho yake kulia kuelekea kwake.Akamwambia kwa kumnong'oneza Grace sikioni na kusisitizia kila neno alilosema.......
“Usiponiondolea mwili wako huu wa uasherati katika mwili wangu ulioukumbatia sasa hivi Grace, haki ya Mungu naapa.......ninamalizana na wewe nitakacho kufanya,hakuna mbwa yoyote duniani hapa atakayeweza kukutizama hata mara moja,hata hao wajinga unaolala nao hawatataka kuwa na chochote kuhusu wewe".
Alitishwa na maneno ya Daniel yaliyomtoka huku akijaa sura ya kutisha aliyomwonesha Grace.
Grace kwa haraka alijitenga naye mara moja bila kujaribu kuufunika mwili wake;
Akajificha kwenye kona ya chumba, akilia huku uso wake akiuziba kwa viganja vyake vilivyo bakiza jasho na manukato ya mwanaume aliiyefumaniwa naye.
Daniel akalirudisha kisanduku kile cha pete mfukoni na kupiga hatua chache kuelekea alipokuwa amejikunyata Grace.
Mwangalie wewe mwanamke...Nakuchukia Grace...unaniadhibu kwa mapenzi yangu kwako.
Daniel Alifungua mlango na kuondoka huku akiubamiza mlango kwa nguvu nyuma yake.
Grace alitoka alijikongoja na kuinuka akajifuta uso kwa mikono yake; alitembea polepole kwenye chumba, akasimama kwenye sanduku la mbao lililokuwa likining'inia ukutani.
Sanduku liliandikwa “First Aid” ilikuwa imeandikwa kwa ufasaha.Akaifungua na kutumbukiza mkono wake wa kulia.Akachukua kikopo kidogo cha dawa.
Haraka akakifungua na kukipeleka mdomoni. Alinyanyua kidevu chake huku vilivyomo ndani ya kikopo vikiingia mdomoni.
Harufu ya kidonge ilimkera, akafumba macho; akameza mate....
ITAENDELEA.......
*Script writing
*Story writing