Ederra
Member
- Mar 2, 2022
- 92
- 533
SEHEMU YA 01
Nilikuwa kwenye usingizi mzito mno ambapo nikaamshwa na sauti ya mwanaume aliyekuwa anagonga dirisha langu na kuniita.
"Ederra! Ederra!"
Bado sikujua alikuwa nani. Alijaribu kuita kwa sauti ya chini mno kuashiria kuwa hakutaka mtu mwingine yeyote amsikie.
Nikashika simu yangu na kuangalia saa. Ilikuwa saa kumi na dakika chache ya usiku.
"Wewe ni nani?" Niliuliza.
"Mimi ni Brian. Naomba nifungulie Ederra tuongelee huko ndani." Alisema kwa sauti ya chini zaidi iliyojawa na wasiwasi mkubwa.
"Brian yupi? Brian wa humo ndani kwa Brenda?"
Nikauliza tena.
"Ndio ni mimi Ederra. Ni Brian wa humu ndani. Naomba nifungulie. Nipo hatarini. Nifungulie tuongelee huko ndani."
"Brian kwani kuna tatizo gani? Nakufunguliaje uingie chumbani kwangu na wewe ni mume wa mtu? Tena ni mume wa mwenye nyumba wangu?"
"Naomba nifungulie Ederra. Nina shida kubwa. Nifungulie nakupa milioni moja cash nikiingia tu humo ndani."
Nilikuwa kwenye mshangao mkubwa. Nilishindwa kuelewa kwanini Brian alitaka kuingia chumbani kwangu usiku ule. Chumba changu kilikuwa chumba cha nje kwenye nyumba nzuri kubwa. Nilikuwa mpangaji pekee kwenye nyumba ile. Mwenye nyumba alikuwa dada mmoja wa miaka 40 hivi ambaye nilizoea kumwita "Da Brenda".
Niliogopa sana kumuingiza chumbani kwangu. Kwanza nilihofia usalama wangu kwa kuwa sikujua nia yake. Na pia niliogopa ingekuwaje Brenda angegundua kuwa nilimuingiza mume wake chumbani kwangu. Walikuwa na miezi miwili tu tangu walipofunga ndoa na mvulana yule mrefu kiasi, mwembamba, mweusi mwenye sura ya kuvutia.
Brian alikuwa na umri wa miaka 32 hivi nadhani. Alikuwa akilelewa na Brenda, mwanamke mwenye uwezo wa kifedha, biashara mbalimbali na jumba la kifahari. Kiufupi Brian alikuwa Marioo.
Licha ya uoga niliokuwa nao nilijikuta namfungulia Brian mlango. Ahadi ya milioni moja ndiyo iliyonishawishi.
"Asante sana Ederra kwa kunipa hifadhi."
Brian alinishukuru mara baada ya kuingia na kukaa kwenye sofa. Alikuwa amevaa T-shirt nyeusi na pensi fupi ya kadeti na mgongoni alikuwa na begi. Akatoa begi lake mgongoni na kufungua zipu. Akatoa kibunda cha hela na kunipatia.
"Chukua hii Ederra. Ni zawadi yako kwa kuniruhusu kuingia chumbani kwako."
"Brian umetoa wapi hizi pesa?"
Niliuliza kwa woga huku nikisita kuzipokea.
"Ni pesa za Brenda. Nikwambie tu ukweli. Nimemuibia Brenda pesa. Nataka nitoke hapo getini. Nimeshindwa kutoka kwa kuwa funguo sijaiona pale inapokaa. Nadhani geti alifunga Brenda. Itakuwa ameiweka sehemu tofauti. Naomba nipatie funguo yako ya geti nitoke hapo getini niondoke."
Brian aliongea huku akiniangalia kwa jicho la huruma.
"Hee Brian mimi sina funguo ya geti. Yangu ilipotea tangu wiki iliyopita. Brenda aliniambia angenipatia nyingine lakini bado hajanipa."
Maneno yangu hayo yalionesha kumnyong'onyesha sana Brian. Aliegemea sofa na kushusha pumzi ndefu.
"Basi sikia Ederra. Naomba nihifadhi humu kwako mpaka asubuhi. Geti likishafunguliwa nitatafuta nafasi ya kutoka bila kuonekana na mtu yeyote."
"Brian hapana. Naomba utoke muda huu. Utanisababishia matatizo. Naomba utoke Brian."
Niliongea kwa hofu na hasira.
"No Ederra usifanye hivyo. Naomba nihifadhi mpaka asubuhi tu. Chukua hiyo milioni moja. Asubuhi nitakuongeza mbili nyingine kabla sijatoka."
Kabla sijajibu chochote ghafla sauti ya vishindo vya miguu ikasikika ikielekea getini. Nikasogea dirishani taratibu na kuchungulia. Alikuwa Brenda. Nikamuona akisogea kwenye geti. Nadhani alikuwa anajaribu kujiridhisha iwapo geti likuwa wazi au lilifungwa. Alijaribu kufungua. Halikufunguka. Alionesha kuwa alikuwa mtu mwenye wasiwasi na haraka.
Akatoka pale getini na kwenda kwenye choo cha nje kilichokuwa upande mwingine wa fensi ya nyumba. Akafungua mlango na kuchungulia. Kisha akaufunga na kuingia tena kwenye nyumba kubwa. Hapo nikagundua kuwa alikuwa anajaribu kumtafuta Brian.
"Brian umeshanitia kwenye matatizo! Brenda anakutafuta kama kichaa. Naomba utoke kabla sijapiga kelele. Naomba utoke sasa hivi."
Niliongea huku mapigo ya moyo yakienda mbio. Niliogopa sana.
"Ederra usifanye hivyo. Naomba nisaidie. Nitakupa pesa niliyoahidi. Nisaidie nakuomba."
Punde Brenda akawa ametoka tena nje ya nyumba yake. Safari hii hakuwa peke yake. Alikuwa na mdogo wake wa kiume aliyeitwa Jose pamoja na dada wa kazi aliyeitwa Zena.
"Lakini ameondokaje nje ya geti wakati geti limefungwa na funguo ninayo mimi?" Na sidhani kama ameruka ukuta kwa sababu fensi ina umeme huko juu. Swichi ya umeme wa fensi ipo ndani ya stoo. Nimeangalia, haikuzimwa."
Brenda alikuwa akiongea.
"Au kuna sehemu amekata nyaya za umeme za fensi? Inawezekana alikuwa amejiandaa kufanya hili tukio"
Jose aliuliza.
"Dah hata sijui. Na pesa alizochukua ni nyingi. Ni milioni 25. Nimepiga simu yake zaidi ya mara 20 haipatikani. Ameshaizima."
"Dada ngoja kukuche kidogo tukatoe taarifa Polisi watusaidie."
Jose alishauri.
Watu wale waliendelea kuongea na kushauriana pale nje kwa zaidi ya saa nzima. Tayari kukawa kumekucha. Zena akaanza shuguli zake za usafi wa nyumba. Brenda na mdogo wake wakaingia ndani ya gari na kuelekea Polisi.
Kwa kweli tamaa ya pesa iliniingia. Lakini hofu ilinitawala zaidi. Nikawaza ingekuwaje wangerudi na Polisi na kisha Polisi wakaamua kukagua chumbani kwangu. Nilikuwa kwenye hatari kubwa. Punde Zena akaja kugonga mlangoni kwangu.
"Ederra, Ederra!"
Nikanyamaza kimya nikijifanya nimelala. Lakini aliendelea kugonga. Nikaona bora nilimsikilize.
"Abee"
Nikaitikia.
"Nifungulie nije nikupe ubuyu shoga yangu."
"Ubuyu gani na wewe Zena? Me nimelala saa hizi."
"Kumekucha bwana. Amka nikupe ubuyu. Brian amemuibia Brenda usiku na ametoroka."
"Hee kweli?"
Nikajifanya kujitia mshangao wa uongo.
"Kweli. Brenda amechanganyikiwa. Wameenda Polisi huko. Sijui kama watampata."
Zena aliendelea kujiongelesha umbea wake na kisha akatoka pale mlangoni kwangu akaendelea na shuguli zake.
"Brian umeshanitia kwenye matatizo. Mpaka sasa huu msala ni wetu wote. Nimesikia pesa ulizochukua ni milioni 25. Sasa baki na 15 nipe 10 nifanye mpango wa kumzuga Zena aingie nyumba kubwa utoke haraka uondoke. Vinginevyo tutakamatwa."
"Poa"
Brian alijibu kishingo upande na kutoa vibunda vingine vya pesa. Jumla akawa amenikabidhi milioni 10. Nikazifunika na shuka pale juu ya kitanda.
Punde nikatoka nje.
"Zena naomba niazime chaja yako. Chaja yangu inasumbua."
"Chaja gani jamani. Wewe si unatumia I-phone?. Mimi sina chaja ya I-phone."
Kwa kweli hapo Zena alikuwa ameniweza. Ni kweli nilikuwa na I-phone.
"No nataka ya chaja ya Android. Nina simu nyingine nataka niichaji."
Niliamua kumdanganya. Sikuwa na simu nyingine yoyote zaidi ya I-phone yangu.
"Haya subiri nimalize usafi nitaenda kukupatia."
"Hapana Zena. Naomba kanichukulie sasa hivi. Nataka nimpigie mtu. Simu yangu imezima".
Zena akakubali na kuingia ndani. Nikarudi chumbani haraka na kumuashiria Brian atoke. Brian akasimama na kuanza kuelekea mlangoni. Kabla hajatoka nje tukasikia sauti ya geti likifunguliwa. Tulistuka sana. Nilipochugulia dirishani nikamuona Baraka akiingia ndani ya geti. Baraka alikuwa mpenzi wangu. Ndiye aliyekuwa amenipangia chumba na kunilipia kodi. Ilikuwa ni kawaida yake kuja bila taarifa.
"Brian ingia chooni ujifiche. Huyo aliyeingia ni Baraka. Ni mchumba wangu. Anakuja humu ndani."
Brian bila kuuliza wala kuongea chochote alikimbia haraka na kuingia chooni. Chumba changu kilikuwa na choo cha ndani.
Punde Baraka akagonga mlango. Nikamfungulia.
"Ederra wangu jamani! Nilikumiss sana."
Baraka aliongea huku akinikumbatia.
"Asante baby. Nilikumiss pia."
Nilijaribu kujifaanya mwenye mahaba lakini akili yangu haikuwa sawa hata kidogo. Baraka aliniongezea tatizo juu ya tatizo. Punde Zena akaita.
"Ederra. Chaja hii hapa."
Nikasogea mpaka mlangoni na kupokea chaja. Kisha nikarudi na kukaa kitandani pembeni ya Baraka. Nilikuwa na wasiwasi mkubwa.
"Nambie baby. Nimeona nikufanyie surprise leo. Nina hamu sana na wewe."
Baraka aliongea huku akinifunua kitenge nilichovaa na kuanza kunipapasa mapajani. Nilinyamaza kimya na kutulia nikijaribu kufikiria cha kufanya wakati Baraka akiendelea kufanya utundu wake.
ITAENDELEA