Simulizi tamu ya aliyewekeza kwenye taaluma

Askarimaji

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2016
Posts
269
Reaction score
651

Injini ya meli kubwa iliharibika, na hakuna alieweza kuitengeneza, wakaamua wamtafute fundi mwenye uzoefu wa miaka 30, alipofika akaiangalia injini yote kwanzia juu hadi chini, baada ya kukagua kila kitu akatoa nyundo ndogo iliyokua kwenye begi lake akagonga sehemu flani ya injin kidogo sana one tap tu. Just like that

Injini ikawaka na kuwa nzima, baada ya wiki moja ya majaribio haikua na tatizo tena fundi akamwambia mmiliki wa ile meli kuwa gharama za jumla za kurekebisha ile injini ni dollar $ 20,000/= sawa na Tsh 48,568,209/= milion arobaini na nane laki tano, elf sitini na nane miambili na tisa

Mmiliki akashtuka kwa mshangao sana akamuuliza yule fundi "Niniii! Kitu gani kikubwa ulichofanya? Katafute karatasi uandike kwa maandishi nini kikubwa ulichofanya hadi nikulipe hiyo pesa"

Fundi kwa upole tu akamjibu tajiri kwa kumwambia "sawa", akachukua karatasi na akaandika vitu viwili tu pamoja na gharama zake, akaandika

1. Kugonga kidogo nyundo moja : $ 2 sawa na Tsh elfu nne tu ya Tz

2. Kujua sehemu gani na wapi nipige hiyo nyundo : $19,998/= sawa na Tsh million arobaini na nane laki tano na kama elfu sitini na sita.

Tajiri aliposoma invoice akakosa cha kusema na akalipa pesa ya watu.
Duniani watu hawajali wewe ni nani wanajali unajua nini tuwekeze kwenye kuongeza ujuzi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…