SIMULIZI: Vijana waongo

N'yadikwa

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2014
Posts
7,427
Reaction score
10,905
Vijana watatu wasomi wa Chuo Kikuu kimoja walitoroka mtihani kwa sababu hawakujiandaa.

Wakaja na mkakati wa namna ya kumdanganya Mhadhiri; hivyo wakakubaliana wajichafue kwa kujipaka Oili chafu na grisi kisha wakaenda kuonana na Mhadhiri.

“Mkuu tunaomba radhi hatukuweza kufanya mtihani. Kwa sababu tulihudhuria sherehe za Harusi na wakati tukirejea gari likaharibika hivyo wakati tukitengeneza tukachafuka na tukashindwa kufika chumba cha Mtihani”

Mhadhiri akaelewa na kuwapa siku Tatu wajiandae kwa ajili ya mtihani maalum wa peke yao yaani Special exam...(kumbe jamaa anawapanga!!)

Baada ya siku tatu kuwadia,vijana wakasoma hasa na kujiandaa kuukabili mtihani huo maalum kila mmoja akiwa na matarajio ya kufanya vizuri.
Mhadhiri akawaweka kwenye vyumba vitatu tofauti kila mmoja kwenye chumba chake japo maswali ni yale yale;
Maswali yenyewe yakawa ni haya hapa;

MTIHANI WENYEWE
1. Ni nani aliekuwa akioa na kuolewa?(25mks)
2. Harusi ilifanyikia wapi? (25mks)
3. Ni wapi hasa eneo mahali gari lilipoharibikia?
(25mks)
4. Ni aina gani ya gari lililoharibika? (25mks)

Marking scheme: majibu yenu sharti yafanane!!!
Bado vijana hao wapo ndani ya chumba cha mtihani wakati huu tunaojadili hili!! [emoji23]
SOMO : Ukweli utakuweka huru.
 
pia ufundi wa magari wameanza lini
(1 marks)
 
Hapo kwenye majibu mfanano ss ndo patam
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…