Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Hilo Raia Mwema la leo tarehe 9 Oktoba 2019 TOLEO MAALUM LA MWALIMU NYERERE Balozi Abbas Sykes anaeleza toka siku ya kwanza 1952 Nyerere kenda nyumbani kwao Mtaa wa Stanley na Sikukuu kaongozana na Joseph Kasella Bantu kuja kumuona kaka yake Abdulwahid Sykes aliyekuwa Acting President wa TAA na Secretary hadi siku amekwenda kuchukua maiti ya Mwalimu London na kujanayo Dar es Salaam kwa mazishi.
Hii ni historia yao ya miaka 40 wakiwa pamoja wakijuana vizuri sana Abbas akiwa kijana mdogo wa miaka 23.
Wakati naangalia TV usiku mmoja wakionyesha ndege ya Air Tanzania Corporation (ATC) iliyokwenda kuchukua mwili wa Mwalimu Nyerere London camera ikapita kwa Abbas Sykes kwa haraka lakini nilimtambua bila wasiwasi wowote kuwa ndiye yeye.
Wakati ule yeye alikuwa ndiye Mwenyekiti wa ATC nafasi aliyoteuliwa na Rais Benjamin Mkapa.
Nilikuwa na kawaida kila nikija Dar es Salaam kutoka Tanga lazima nipite ofisini kwa Bwana Ally Sykes kumjulia hali kisha niende nyumbani kwa Balozi Abbas Sykes.
Safari hii nilikwenda kwa Balozi Sykes kwa nia khasa ya kutaka kujua safari yake ya London kwenda kuchukua mwili wa Mwalimu Nyerere.
Bwana Abbas tukiwa mimi nimekaa kwenye kiti changu ninachokipenda ndani ya ukumbi wake, kiti ambacho kinanipa mandhari ya mchanga mweupe wa bahari na bahari yenyewe na yeye kama kawaida amekaa kwenye kiti cha baba mwenye nyumba kwani huwa siku zote ndicho kiti chake nilianza mazungumzo kwa kumpa pole kwa msiba wa Mwalimu Nyerere.
Balozi Sykes akaitikia ile pole yangu kisha akasema, ‘’Unajua mimi kama Mwenyekiti wa ATC nilitiwa katika msafara wa kwenda kuuchukua mwili wa Nyerere.
Ingekuwa si hii nafasi yangu ya uenyekiti nisingepata fursa na heshima ile kwani hawa viongozi walioko madarakani hawajui kuwa Nyerere sisi ni ndugu yetu.’’
Nilijua bila ya kuuliza kuwa ile, ‘’sisi,’’ Balozi alikusudia wao Sykes Brothers. Nilikuwa sijapatapo kumsikia Bwana Abbas akijinasibisha udugu na Nyerere.
Mara zote alipokuwa akieleza harakati za kudai uhuru alikuwa akimweleza Nyerere katika nafasi ya urafiki wake na kaka yake Abdul na kama kiongozi wa TANU, hili la udugu ndiyo siku ile nalisikia kwa mara ya kwanza.