Simulizi yangu ya kwenda kwa waganga wa kienyeji sehemu mbalimbali nchini na nje ya nchi

Inaendelea

Nilifika Songea na kuanza kufanya biashara ya kununua na kuuza mahindi nilijichanganya na wazoefu biashara ikawa inaenda poa, pale nilipokuwa nimepanga kulikuwa na nyumba kama nne kwenye eneo moja kulikuwa kama kota,walipanga wafanyakazi na kuna jamaa wengine nao wafanyabishara wa mahindi na dili nyingine nyingi nyingi,dili chafu na safi walikuwa wamepanga pale pale.Nikaibiwa walivunja chumba changu na kikasafishwa kila kitu tene waliiba mchana,kuna vijana wawili walikuwa wamepigwa marufuku kuingia maeneo yale nilivyowaambia jamaa zangu wakawahisi wale vijana,wakaniambia nenda kwa Binti Ndembo ukawakomeshe,kipindi hiko Ruvuma kulikuwa na mganga anaitwa binti Ndembo alikuwa mashuhuri sana alikuwa anapatikana wilaya ya Namtumbo.

Sikwenda kwa binti Ndembo nilienda kwa mganga mmoja alikuwa anaishi karibu na msikiti wa mkoa nilifika kwake muda wa saa moja giza likiwa limeanza kuingia,nikaingia kwenye chumba cha uganga na kumuona mganga nikamueleza shida yangu akanisikiliza na kunitajia kiasi kidogo cha fedha ambacho aliniambia nitampa mara tu nitakavyopata vitu vyangu nikamuambia sawa,mganga akafanya uganga wake na alivyomaliza alianza kujaza upepo kwenye tyubu ya baiskeli aliniambia kadri anavyojaza na matumbo ya wale wezi nayo yatakuwa yanajaa
 
ndo imeisha
 
kutamka tu yanga umetukwaza wengine, inaonekana hii story Ni ya Simba tu, hivyo kwaheri ndugu yangu, machungu ninmengi Sina mda wa kuhangaika nawe
 
ila mi Ni Simba dam dam, sijapenda tu ulivyohusisha ushabiki na story yako, hkukuwa na sababu Wala maana
 
[emoji23][emoji23][emoji23]akiishusha yote naomba nishtue maana huyu mapicha picha kaanza mapema sana
kweli jamani, Mimi pia mnitag, Mana uyu fala anajiona tuna shida Sana na story yake, Yani imekua trend Sasa jf, kwamba itaendeleaaa, naomba muwaambie mods kwamba hi Ni trend inatusumbua Sana wateja wao waipige ban, yaani unasema tu itaendeleaaa inakuwa ban ya miezi sita, Kuna wale wanaweka mwendelezo kwa link kwenye post yao ya Kwanza, wapewe heshima na ulinzi wa jkt
 
Nikamwambia sawa endelea akaanza kujaza tyubu ikawa inajaa mwishowe mpira ukapasuka mganga akaniambia tushaua,nilistuka nikamuuliza unasemaje akarudia tushaua kwa sababu Mpira ulivyopasuka na matumbo ya wezi nayo yatakuwa yamepasuka,nikamuuliza sasa tunafanyaje akaniambia ondoka urudi kesho nikamwambia sawa,nikarudi getoni huku nawaza naanza tena kununua vitu.

Nikafika geto nikawasimulia jamaa zangu kilichotokea,walichukia sana nilipowaeleza sikwenda kwa binti Ndembo lengo lao lilikuwa kusikilizia kama binti Ndembo ni mganga kweli au la.
Wale vijana sikuwahi kuwaona tens.

Jamaa walikuwa magijwi wa kuzunguka kwa waganga, walikuwa wanaenda Msumbiji, Congo kufuata waganga.

Niliendelea kufanya biashara yangu ya mahindi wakati huo Mdigo alikuwa kaenda Msumbiji kununua magari mabovu na kuyaleta Tanzania na kutatengeneza kisha kuyauza,huyu Mdigo walikuwa na uwezo mkubwa wa kutambua fursa mapema ingawa naye alikuwa bingwa kwenye mambo ya ushirikina.

Baada ya Mdigo kuondoka na Mimi nilihama kwenye zile nyumba nikaenda kupanga kwenye nyumba moja ipo mtaa wa Mahenge,nilihama kwa sababu jamaa nilikuwa siendani nao pia biashara yao chafu ingeweza kusababisha tusombwe nyumba nzima.

Sababu nyingine ya kuhama nilikuwa nimepata demu mmoja anaitwa Y myao kutoka Tunduru alikuwa anakatika kuliko panga boi,alikuwa fundi kweli kweli,ningempeleka pale kwa jamaa zangu wangembeba tu,maana wao kuchangia demu kwao ilikuwa kitu cha kawaida.Pamoja na ufundi wake Y alikuwa mkorofi sana Mara kwa Mara tulikuwa tunagombana kwa sababu za kipuuzi na Mimi nilikuwa siyo mnyonge akizingua nilikuwa namzingua Mara mbili yake,Y akapata mimba,usiku wa SAA 4 anaweza akakuagiza ukamnunulie Coca cola,nilikuwa kijana Mdogo sijui lolote akiagiza hivyo lazima nimwambie maneno ya kijeuri ambayo alikuwa anachukia sana.

Ugomvi ukawa unaendelea mwishowe akaniambia naenda kutoa mimba yako nikamwambia nenda,nikampa elfu 30 akaenda kutoa,usiku akaja geto kulala lakini Siku hiyo hatukulala tumbo lilikuwa linamuuma akawa anajinyonga nyonga usiku kucha,sababu ya kuumwa ni kuna vitu walivisahau kuvitoa,Siku ile nilijua atakufa,SAA Tisa usiku nikazima taa zote za nje na ndani nikatoka nje ,pale nyumbani kwa nyuma kulikuwa na korongo kubwa nikawa naenda kuangalia njia nitakayoitumia kwenda kutupa maiti ya Y ikitokea amekufa.

Y hakufa lakini kama ningefanya vile ungekuwa uamuzi wa kipumbavu sana maana MTU wa kwanza kukamatwa ingekuwa mimi,watu wengi waliujua uhusiano wetu.
Nikarudi ndani Y alikuwa anaendelea kuugulia maumivu makali sana huku anajinyonga nyonga nilimuonea huruma sana.Nilikuwa sijaenda kanisani miaka mingi lakini Siku ile nilijikuta nasali sala zote,nilipiga magoti ,nilinyanyuka nikawa natembea huku naomba kama Walokole.

SAA 11 asubuhi Y bado alikuwa anaugulia maumivu makali nikapiga simu kuita boda boda ikaja ikampeleka kwa Daktari aliyemtoa mimba.
Mchana akawa amepona baada ya kwenda kutolewa vitu vilivyosahaulika.
Ukorofi uliendelea tukaachana.

Siku moja nilikuwa geto nikapigiwa simu kuna tajiri anataka mzigo nikaenda kumuona alikuwa kijana mmoja kutoka Njombe jamaa zangu waliniunganishia nikaenda nikamkuta kijana Mdogo mwenye mwili mdogo,walikuwa wanakunywa na kufanya maongezi na Mimi nikajiunga nao.
Nikafanya maongezi na tajiri tukakubaliana kesho yake atapakia mzigo na kulipa fedha zote,tajiri alikuwa anawanunulia pombe jamaa zangu lakini hela alikuwa anazitoa kwenye diary, nilijiuliza maswali mengi sana,alikuwa anafunua diary na kutoa fedha,hela zilikuwa haziishi wala diary haionekani kutuna.

Kesho yake muda wa SAA mbili usiku tajiri akalipa fedha milioni nane nikazichukua nikaenda nazo geto nikafunga mlango nikaziweka kwenye begi wala sikutoka Siku ile.
Asubuhi hakukuwa hata na buku,begi halijafunguliwa mlango umefungwa lakini fedha hazipo.Nilichanganyikiwa.
Nikaenda kijiweni kwa jamaa zangu nikawaeleza majanga ya
liyonikuta walisikitika sana wakasema itakuwa tajiri kazivuta.
Nikarudi geto huku nimechanganyikiwa nilijiuliza maswali mengi sana nakumbuka machozi yalinitoka.
Jioni nikaona namba ngeni inaingia kwenye simu yangu mtandao wa MCEL wa Msumbiji alikuwa Mdigo akaniambia Msomi nasikia wamekupiga,aliendelea kusema na ukiendelea na usomi wako watakupiga sana.Ingawa nilikuwa naenda kwa waganga lakini sikuwa nakubali
sana mambo hayo mazingira tu yalinilazimisha.
Siku ile niligundua naishi kwenye Dunia ya ushirikina ,nikatamani niajiriwe yaani nianze kuhangaika kutafuta ajira, nikakumbuka ajira walizokuwa wanafanya niliomaliza nao chuo, lakini nikikumbuka mishahara yao ya laki sita nikasema wacha niendelee kuishi kama wanavyotaka, yaani niendeleze ushirikina.

Kule machimboni Chunya kuna dogo mmoja nilipomaliza shule ya msingi nilimuacha madarasa manne,yeye alianza kuchimba zamani kwahiyo alibahatika kupata hela. Siku moja tuligombana aliniambia braza wewe umenizidi elimu na umri tu...Yalikuwa maneno ya ukweli ila yaliniuma.Kila nikiyakumbuka Yale maneno huwa nazidi kupata hasira niliapa ipo Siku nitamzidi elimu,umri na fedha.

Nikapanda pikipiki nikaelekea kwa mganga alikuwa anaishi kijiji kimoja kabla hujafika Namatuhi barabara ya kwenda Msumbiji.
Nilishaanza kuwa gwiji kwenye mambo hayo.Nilifika kwa mganga asubuhi sana nilienda kwa masuala mawili tu nizipate fedha zangu na nisiibiwe tena kizembe.

Itaendelea.
 
Apig
Mkuu unamlipa nn? Ana kazi zake yaani kuna watu hamjielewagi eti na komandi juu kwani unalipa?
 
Thanks,nilichelewa kuiona,hata hivyo nilitoka mapema goli la pili la wagosi sikuliona.
 
Inaendelea

Baadhi ya watu hasa washika dini najua nawakera lakini simulizi kama hizi mnaweza kuziepuka kwa kutokuzisoma.
Ila msibague dhambi hata zingine msiwe mnazifanya maana kuna kiongozi mmoja mkubwa sana wa dini hapa Tanzania anatembea na mke wa mtu

Nilionana na mganga nikamueleza shida yangu akaniambia nenda kalete nyoya kubwa la mkiani LA jogoo linaloangalia juu,Siku ile ndipo nilipogundua kuwa kwenye Yale manyoya ya jogoo ya mkiani makubwa jogoo wengine yao yanayoangalia juu na wengine chini.

Ikabidi niende sokoni kununua jogoo kwa ajili ya kupata nyoya tu,lakini nilikuwa na mawenge nikanunua mwenye nyoya linaloangalia chini,nikalipeleka kwa mganga akalikataa akaniambia kalete linaloangalia juu,nikaenda tena kununua LA jogoo linaloangalia juu.
Nikampelekea mganga akafanya uganga wake akachanganya na dawa nyingine akanipa karatasi akaniambia niandike ninayoyataka nikaandika akachukua ile karatasi akachanganya na lile nyoya na madawa yake akaniambia niongozane na msaidizi wake tupande mlima tukachome dawa mlimani,ila tukianza tu kupanda hakuna kuongea,huo mlima alikuwa anautumia kwa shughuli zake za uganga na matambiko tukapanda mlimani na kiberiti ,mlimani kulikuwa na upepo mkali sana,kila tukiwasha njiti inazima kwa sababu ya upepo ikabidi tushuke chini.
 
Moja ya kitu ulichoshindwa kukifuata katika simulizi yako ni utaratibu, yaani umechemsha kwelikweli Daraja la miti yaani umeanza vizuri, baadaye umechanganya soda, energy drink na gambe humo humo nadhani maji yatakuwa chini 😷!.
 
Semina za kipuuzi kma hizi mi sinaga time nazo kabisaπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…