Simulizi za Mlosi Mtulutumbi: Misingi ya Mafanikio

Simulizi za Mlosi Mtulutumbi: Misingi ya Mafanikio

IsangulaKG

JF-Expert Member
Joined
Oct 14, 2010
Posts
706
Reaction score
386
MISINGI YA MAFANIKIO

Sehemu ya Kwanza

Na Mlosi Mtulutumbi


Neno mafanikio lina tafsiri tofauti kwa kila mtu , na mimi pia nakubalia na hali hii kwani kubadili maisha yako toka kiwango Fulani kwenda kiwango kingine ni mafanikio pia. Tofauti na wengi wanavyodhani, kuwa tajiri si kipimo pekee cha kufanikiwa bali kwa kuwa watu wengi wamepitia machungu mengi katika kutafuta mali basi mali au utajiri inatafsiriwa wengi kama mafanikio. Wakati kwa wengine kununua kupata kazi nzuri, kuoa au kupata watoto ni mafanikio, wengine kununua gari au kujenga nyumba ni mafanikio pia.
Mwanasaikolojia, Abraham Maslow katika nadharia yake ya ngazi za mahitaji ya binadamu hasa katika mambo ya motisha ili pawe na ufanisi wa jambo, aliamini kwamba kila mtu ana motisha ya kufanya kazi au jambo lolote ili kutimiza mahitaji yake fulani. Kadri mwanadamu anavyotimiza mahitaji yake ya ngazi ya chini ndipo hujibidiisha kufanikisha mahitaji yake ya ngazi inayofuatia. Kuna ngazi kadhaa za mahitaji ya kibinadamu kuanzia na mahitaji ya msingi kama vile mahitaji ya kimwili, usalama, mapenzi na heshima na mahitaji ya ukuaji binafsi. Ili mtu aseme amefanikiwa katika mahitaji ya juu yaani ukuaji binafsi ni lazima apate mafanikio katika mahitaji ya msingi kwanza. Mahitaji ya awali yakikamilishwa ndipo sasa mtu anafikia kiwango cha juu sana cha mafanikio ambacho ni ukuaji binafsi. Mahitaji ya kimwili ambayo ndiyo ngazi ya nchini kabisa ya mahitaji ya kijamii ni kama vile chakula na maji. Kadri ambavyo mahitaji haya ya ngazi ya chini hayajatoshelezwa, ni motisha tosha kwa mwanadamu kuendelea kuhangaika kila siku kupata vitu hivi. Mtu mwenye njaa anahitaji chakula, hitaji hili la chakula huamsha msukumo wa kifisiolojia, hisia na fikra ambazo hujidhihirisha katika tabia ambazo zinaelekezwa kupunguza hitaji la chakula kwa kupata kitu chochote cha kula nah ii yaweza kuhusisha hata fikra za kuiba. Pale mtu anapokula, msukumo huo hupungua na hitaji la chakula husimama na hata tabia ambazo zilijielekeza katika kutimiza hitaji la chakula hukoma pia. Baada ya ‘kufanikiwa’ kuwa na uhakika wa chakula, chakula hakiwezi kuwa kichocheo cha kufanikisha mahitaji mengine. Kwa mfano, iwapo utatengeza mradi wa kuwavuta akina mama wajawazito kujifungulia kliniki kwa kutoa chakula cha bure hospitalini sehemu ambayo mahitaji ya chakula yamekwisha toshelezwa ni vigumu kufanikiwa. Lakini sehemu ambayo mahitaji ya chakula hayajatoshelezwa, iwapo utagawa chakula kwa wananchi ili wakupigie kura wakati wa uchaguzi ni rahisi kufanikiwa kwa sababu hitaji la chakula husukuma tabia zao (pengine na maamuzi) ili mradi tu watimilize hitaji lao la chakula kwa wakati huo.
Hata hivyo, mahitaji haya si lazima yajitosheleze kwa asilimia mia moja ili mwadanamu ahitaji mahitaji ya ngazi ya juu. Mfano, mtu akipata mlo mmoja wa jioni, usiku ukikaribia lazima atahitaji mahali salama pa kulala (ambalo ni hitaji la ngazi ya juu zaidi) lakini kama ana njaa hata akipata mahali pa kulala bado tabia zake zitajielekeza katika kutimiza hitaji la msingi yaani chakula!

Baada ya kufanikisha mahitaji ya ngazi ya chini mfano chakula , mwanadamu sasa hujibidiisha kufanikisha mahitaji ya kiusalama, hapa namaanisha nyumba na usalama. Mahitaji haya huwa kichocheo cha mafanikio kwa mtu ambaye tayari amefanikisha mahitaji ya awali kama nilivyosema hapo juu. Mahitaji ya usalama hujumuisha hamu ya kuwa salama, hali ya utulivu, ushirikiano, ulinzi, kutokua na hofuna uhitaji wa mifumo ya sharia na kanuni. Baada ya kutosheleza mahitaji haya ndipo mwanadamu huwa na mahitaji ya kijamii kama vile upendo na hitaji la ushirikiano na wanajamii wengine na kujisikia kama sehemu ya jamii.
Baada ya mahitaji haya ndipo mahitaji ya kuheshimika katika jamii yanapochochea tabia za binadamu. Mahitaji ya kuheshimika ni pamoja na hamu ya kujiheshimu na kuhesimiwa, hamu ya kupata sifa katika jamii (reputation), ufahari (prestige) , utukufu (glory) kuhodhi mamlaka au mali (dominance), kutambuliwa, kuonwa mtu muhimu, na kukubaliwa kijamii

Kila mwanadamu anahangaika sana kufanikisha mahitaji ya ngazi ya chini kama njia ya kufanikisha yake ya juu, kwa bahati mbaya matukio kadhaa katika maisha ya mwanadamu humfanya ashindwe kufanikisha mahitaji yake ya juu. Kwa mfano ufukara, kushindwa kufaulu mitihani baada ya kusoma kwa miaka kadhaa, kukosa au kupoteza kazi, kutopata mavuno ya kuridhisha baada ya rabsha za kilimo na kadhalika, mambo haya hufanya mtu aliyekuwa anakaribia kufanikisha mahitaji ya ngazi moja kushindwa kuyafikia na kurudi katika ngazi ya awali. Maslow aliona kwamba kati ya watu mia moja, ni mmoje pekee anayeweza kufanikisha mahitaji yake ya ngazi ya juu yaani kuheshimika kwa sababu mifumo ya kijamii inawezesha mtu kumtambua mtu mwenye mafanikio (ukuaji binafsi) kwa kuangalia heshima, upendo alio nao na uwezo wake wa kutimiza mahitaji mengine ya kijamii.
Hata hivyo, kutokana na nadharia hii ya Abraham Maslow ambayo inakubalika sana na wanataaluma wengi ingawa ilipata upinzani wa wanasaikolojia wachache bado inatuonyesha kuwa mwanadamu ana mahitaji ya hali ya chini na ya juu na kwamba mwanadamu kwanza anahangaika kutimiliza mahitaji ya chini kabla ya kufikiria mahitaji ya ngazi ya juu. Mtu mwenye njaa kwa mfano hawezi kufikiria kuwa na ufahari katika jamii na ni lazima tabia zake zitaelekezwa kutimiza mahitaji yake ya chakula. Mtu mwenye chakula cha kutosha, makazi bora na usalama anahangaika kutimiza mahitaji ya kuheshimika kwa jamii. Tabia zake zitaelekezwa katika kuhakikisha kuwa anatambuliwa na kuheshimika katika jamii. Siku zote watu hawa hawawezi kuwa na tabia au fikra zinazofanana. Mtu mwenye hitaji la chini yaani chakula anawaza chakula na mtu mwenye mahitaji ya ngazi ya juu ya kuheshimiwa anawaza na kufanya matendo yatakayotimiliza hitaji lake la kuheshimiwa. Kwa kuwa mtu mwenye mahitaji ya juu anawahitaji hawa wenye mahitaji ya chini ili kutimiliza mahitaji yake ya kuheshimika kwani wao (wenye mahitaji ya chini) ni sehemu kubwa sana ya jamii, ni rahisi kufanya mambo yatakayotimiliza mahitaji ya watu wa chini japo kwa muda mfupi ili waweze kumkubali kama vile kugawa chakula n.k. Tena , watu wenye mahitaji ya sifa na heshima kwa jamii wanazo tabia za wazi zinazodhihirisha uhitaji wa sifa na heshima kutumia vyombo vya habari wakati nwa kutoa ‘msaada’ ili jamii anayohitaji imheshimu itambue kile alichokifanya.
Hebu fikikiria mtu mwenye njaa kali ambaye alikuwa anawaza hadi kuiba chakula shambani mwa jirani na ghafla akapewa kilo mbili za mchele ambazo hakutarajia kupata, ni lazima atamheshimu huyo aliyemtimilizia mahitaji yake pasipo kujali kuwa anatumika kutimiliza hitaji la mtu mwingine ‘kuheshimika katika jamii’

Hata hivyo ukweli ni kuwa kila mwanadamu anavyotatua hitaji lake la ngazi ya chini na kupata uhakika wa hitaji lake wenye mlengwa wa kudumu, tunasema amepata mafananikio. Baada ya kufanikiwa katika ngazi hiyo, huanza sasa kujibidiisha kutimiliza hitaji la ngazi nyingine ya juu.
Kwa ujumla, Kinyume cha mafanikio ni vile tusivyotaka maisha yetu kuwa. Kila mtu anahitaji uhakika wa mahitaji yake kila afikiapo ngazi fulani lakini utapata matokeo yale yale iwapo utaendelea kufanya mambo yale yale yanayokuweka hapo ulipo. Mabadiliko ni lazima ikiwa unataka kutimiza mahitaji ya ngazi ya juu kuliko hayo ya sasa. Changamoto haziepukiki na lazima kuzikabili. Katika kitabu chake cha ‘within you is power’, Henry Hamblin anasema ‘changamoto katika maisha ni kama mawimbi ya bahari, tunatofautiana jinsi tunavyozikabili, wakati wengine wakirdhika na kuacha kukabili changamoto kama vile mawimbi yanavyomzamisha mtu asiyeogelea, wengine hujibidiisha kuzikabili changamoto kama vile muogeleaji anayojibidiisha kuelea juu ya wimbi il asizame’

Mwili wa binadamu ni ushahidi tosha wa kukabiliana na changamoto. Kinga ya mwili hupigana na maambukizi au vijidudu vya maradhi vya aina nyingi kila siku lakini bado unaendelea kuishi. Kama kinga ikisimama kufanya kazi basi hutaishi muda mrefu, suala ni kwamba kama kinga yako ya mwili haichoki kukabiliana na wadudu unaowaingiza mwilini kupitia kinywani, sikioni, machoni, kwenye ngozi, sehemu za siri nk , kwa nini wewe uchoke kujibidiisha ili utimilize mahitaji yako?
Watu hulaumu mabadiliko, mabadiliko ya kiuchumi, mabadiliko ya hali ya hewa, mabadiliko ya mila na desturi n.k. pasipo kujua kuwa hata wao hubadilika pia. Binadamu hubalika kila siku mfano nywele hukua kwa wastani wa sentimente moja na milimeta ishirini na tano au tuseme nusu nchi kila mwezi na Idadi ya watu huongezeka kwa zaidi ya 228,000 kila baada ya masaa ishinini na nne. Mabadiliko hayaepukiki, yapo na kila siku yanatokea. Kazi kubwa tuliyonayo ni kuyafanya mabadiliko yaendane na mabadiliko katika utimizaji wa mahitaji yetu ya kibinadamu vinginevyo mabadiliko yatakuacha nyuma.

Tofauti kubwa kati ya mwanadamu na mnyama ni kuwa mwanadamu ana uwezo wa kuchagua kile anachotaka. Punda hawezi kuchagua kiwango cha mzigo wa kubeba ila mwanadamu humchagulia. Kuku hachagua mgeni wa kumla ni mwanadamu ndiye huchagua. Kwa sababu tuna uwezo wa kufanya uchaguzi wa maisha, hii ina maanoa sisi ni viongozi wa maisha yetu. Ukiamua kuishi kifukara unakuwa kiongozi wa maisha yako ya ufukara na vivyo hivyo familia yako unayoingoza ina uwezekano mkubwa wa kuwa fukara hata vizazi vijavyo. Wewe kama mzazi, ukichagua kuishi kifukara leo na wanao wakazaliwa katika ufukara hata wakijibidiisha kujiondoa kwenye ufukara bado utaendelea kuwavuta kuwarudisha katika ufukara.

Vijana wengi wanaotoka katika ufukura, huchukua muda mrefu sana kujiondoa huko iwapo watatumia njia halali kwani bado ndugu na jamaa ambao ni mafukara watamvuta kurudi ufukarani kadri anavyojitahidi kujiondoa huko. Mara utaambiwa bibi anaumwa kisukali mara yabidi umjengee mzee nyumba na kadhalika na kwa kuwa hakuna mifumo ya kiserikali inayotoa ulinzi wa jamii fukara basi yule anayejibidiisha kujitoa katika ufukara huwa ndilo tegemeo la mafukara wote katika eneo alilotoka.

Lakini hii si sababu ya kutosha kutojibidiisha kujiondoa katika ufukara na ni lazima tusiwe mateka wa misukumo inayoshawishi ufukara. Ni lazima tufanye mabadiliko na si kuacha mabadiliko yatokee yenyewe. Pasipo kujali vikwazo vyetu au vikwazoi ambavyo watu wengi wamekabiliana navyo, wale waliovishinda ndiyo waliofanikiwa kimaisha. Jambo la msingi ni kuwa iwapo utaendelea kufanya mambo yale yale ambayo unayafanya kila siku ni lazima utapata matokeo yako ya kila siku. Mfano mkulima akiendelea kutumia jembe la mkono wakati mahitaji ya chakula ya familia yameongezeka hataweza kupata chakula ncha kutosha kutosheleza mahitaji ya familia.

Kama vile ambavyo nyumba imara hutegemea msingi imara, Wataalamu wa masuala ya kijamii wamependekeza missing mikuu mitano ya mafanikio. Haya ni mambo ambayo LAZIMA yawepo ili mtu afanikiwe.


Sehemu ya Pili itahusu: Msingi wa Kwanza wa mafanikio
 
Mkuu mbona unatuchanganya kidogo, maana unatuambia Maslow katika mahitaji ya kwanza muhimu anasema tunahitaji chakula cha uhakika. Sasa mwanasiasa akikupa kilo mbili ya mchele hapo kweli atakuwa amempa mtu uhakika wa chakula. Maana arudi tena mpaka miaka mitano ijayo, napata tabu kama chakula kwa maelezo yako ndio sababu hapa in Maslow's perpective ya kutoa kura.

Kingine ni tofauti ya binadamu na mnyama aipo kwenye kuchagua, tofauti yetu hipo kwenye reason ability or intelligence. Binadamu anaweza ku-reason wanyama wengi awawezi au wapo very poor. Hatahao binadamu vilevile wanatofautiana na uwezo wa ku-reason sababu ni upeo ambapo chanzo chake ni experience tofauti za mazingira binadamu aliyopitia, elimu, upatikanaji wa habari or being informed etc. Na ili ndio linaweza mfanya binadamu ajue au afahamu fursa tofauti zinafananje.

That is where the poverty debates begin maana tatizo si binadamu tu pekee mazingira yake pia yanachangia kumfanya mtu awe maskini au tajiri kurudia tena vitu muhimu exposure, knowledge and environment. Mfano naweza kufahamu ya kuwa miwa yangu inaenda tengenezewa sukari ambayo inaenda kuuzwa bei ya juu, je ninao uwezo wa kutengeneza sukari mi mwenyewe ili nifaidike au hata najua jembe la mkono alifiki mbali je ninao uwezo wa kununua trekta au hata n'gombe na kumpachika jembe? kama sina huo uwezo then politics will determine my fate, again kama sijui wajibu wa serikari (tunarudi palepale kwenye elimu/ignorance) ina maana siwezi kupiga kura kimaslahi, kwa sababu sielewi hata sera zenyewe za vyama zinasimamia nini au hata watatekeleza vipi, to change that power matrix yaani vyama vya siasa viwaogope wapiga kura, inataka wapiga kura wajue wanataka wapewe nini in the first place na chama gani kinaweza hivyo, hapo ndio tulipo; upeo wa jamii bado mdogo. Lakini habari za ufisadi is not convincing to me kwamba mwakani machungwa ya shambani kwangu yote nitauza. Habari hizo peleka mahakamani.

Na kama mzazi bado ajafahamu umuhimu wa kura ya maslahi anaweza asione umuhimu wa elimu ya mwanae pia, na hapo ni kumnyima akili ya kuweza kupima maamuzi yake ya baadae. Kwa mnajili huo poverty then turns into culture kama serikari aitaingilia kati, you know what ndio maana siasa safi kumbe ndio kila kutu ili society iendelee. Nyerere alishalisema hilo long time ago, but then he was educated and exposed si ni kwa sababu hizo ndio akapigani uhuru wa taifa pia, sasa unategemea maskini atajikwamua vipi bila ya kujengewa mazingira ya kukuza huwezo wake wa kureason, kuwekewa mazingira ya kukopesheka ili alime kisasa, kuwekewa soko la uhakika na mengineo yenye kuboresha maisha yake, embu tuache kuzani maskini kule vijijini wanajitakia wenyewe as if those people lie in beds all day and are happy to live with restricted choices.
 
Chakula cha uhakika si sawa na mlo wa siku moja, bali uwepo wa uhakika wa chakula kwa siku zote!
 
Back
Top Bottom