waungwanaTz
Member
- Aug 6, 2024
- 11
- 9
YAI
Kwa kuwa alikwa mwanae,Chuwa hakumwita mwizi bali,alimwita mdokozi.
Chuwa akasahau ya kuwa, kile kinachofanywa na mwanae hakina tofauti na kilichofanywa na kina fulani ila kwa kuwa mwanae ameiba mboga madhara ya wizi wake yanaiathiri familia tu na kwa kuwa kina fulani wameliibia taifa,madhara ya wizi wao yanaliathiri taifa zima.
" Umleavyo,ndivyo akuavyo"
Chuwa akamlea hivyo hivyo.
Alipomaliza vya nyumbani,akaanza vya jirani.
Siku moja.....
lengo la simulizi hili ni kumtaka kila muungwana kufanya yafuatayo:
1.Kutujuza mayai mazuri na mabaya aliyowahi kuatamia.
2.Kufafanua misemo iliyotumika kwenye simulizi hii.
3.Kuvaa viatu vya mzee Haji na kumpatia ushauri Chuwa.