Simulizi za waungwana: Nzi hasiyefuata ushauri, huifuata maiti mpaka kaburini

Simulizi za waungwana: Nzi hasiyefuata ushauri, huifuata maiti mpaka kaburini

waungwanaTz

Member
Joined
Aug 6, 2024
Posts
11
Reaction score
9
NZI

Licha ya kuonywa na wazee,Chuwa aliziba masikio.
Akaendelea kutumia fedha za mabeberu ili kuendesha kampeni zake.
Baada ya kushinda uchaguzi na kuingia madarakani,mabeberu wakataka rejesho,
rejesho hilo lilikuwa ni kumsainisha Chuwa mikataba mibovu ili wabebe mali za kijiji.
Kadri mali za kijiji zilivyozidi kusombwa,
ndivyo wanakijiji walizidi kuishi maisha magumu, mwisho wa siku wakakosa uvumilivu na kutaka kuingia njiani.
Chuwa alipoiyona hasira ya wanakijiji,akaanza kuwaza awadhibiti vipi.
Wakati anatafakari zaidi,maneno aliyoambiwa na wazee wale yakamjia kichwani.
Mwanetu!
“Kheri ya mzalendo aliyeshika panga mkononi kuliko beberu aliyeshika peni mkononi”
Maneno yale yalimpa Chuwa ukakasi,
akawaza tena afanye nini lakini hakupata jibu,
alipohisi anazidi kuchanganyikiwa akaona.......

 
Back
Top Bottom