jamani wadogo zangu poleni na hata wewe
smile nakuandikia hii comment hebu ukisha isoma ifanyie kaz, sipend jins ambavyo mnateswa na nafsi zenu wenyewe wapenzi wangu.
Kwanza suala la kujiamini katika mapenz linasababishwa na nini? Ukisha pata jibu hapa basi mengine yote yatakuwa rahisi.
Jibu ni kwamba kujiamini kunatokana na kuwa na mpenz ambaye ana kidhi au niseme ana meet vigezo unavyovitaka kwa kiasi kikubwa. Kumbuka vipo vigezo ambavyo mume wa aina yeyote mtarajiwa anatakiwa awe navyo kama vile kujiamini, awe na nidhamu, awe muwajibikaji, awe na upendo, awe anajali, asiwe mtu asiyejua wajibu wake hasa katika mahusiano, awe mwenye kupenda familia. Pia awe mtu mwenye msimamo na anaye mpenda au mcha mungu. Hivi kwangu mimi ni vigezo vya lazima sana kwa mume mtarajiwa. Sasa kama ukimpata mtu anaye meet haya kwa kiwango kikubwa definately utakuwa na confidence naye.
Ishu ya kwamba ataniacha na kuoa mtu mwingine inakuja kama miongoni mwa hivi vigezo vikubwa hutaviconsoder. Mathalani mtu mwenye upendo, anayejali, muwajibikaji, anayependa familia, mwenye msimamo na mcha mungu, basi atakuwa ni mtu ambaye anataka mke na mwenzi wa maisha na wala siyo wa kubip tu. Inatakiwa sasa hivi mfike mahali ma boyfriend muachane nao na mtamani kuwa wenzi wa maisha. Unajua ni kweli kuwa boyfriend wako anaweza kuishia kuwa mumeo na pia kuna wakati hili huwa halitimii na ii husababishwa na ma bf wengi kuchaguliwa kwa kigezo cha uhandsome na u much know kuliko vitu muhim nilivyovitaja hapo juu.
Pia ifike mahali ninyi wadada muwe outstanding in such a way mtu akitoka na wewe aone kabisa you can make a good wife na siyo a good cinema or outing partiner. Wadada mnajisahau sana kwenye hili try to be real msiwe ni watu kwa muonekano wa kwanza mnapendeza kwenda out, cinema na beach lakini muonekano wa ndani wa kuwa mama utakayelea familia yenye ndugu toka pande mbili na watoto mnaonekana hamtaweza. Na hili linaonekanaga bila hata kuish na mtu. So take care sana na aina ya muonekano mlionao.
Mwisho kabisa nasisitiza kusali na kumwachia mungu afanye, wewe timiza ya kwako na mengine yaliyo ya mungu mwachie. Siwanyimi kutooka bali nawaambia ukweli manake ninawaskia sana hawa ambao huwa wanataka kuoa na wanakuja na hoja kuwa bint fulan simui kwasababu yule ni wa cinema tu au ni wa kula raha tu bufuture hana.
Mwisho mod naomba ukurasa na mimi niwe nawafunda hawa wadada wa jf manake naumia sana kwa ajili yao.
Nawasilisha