Sina heading ya kuipa hii ishu...

Easymutant

R I P
Joined
Jun 3, 2010
Posts
2,564
Reaction score
1,133
Mke wa Frank anajivunia mume mtulivu, hashindi baa na hatongozi videmu.

Akitoka kazini huenda kucheza basketball na hurudi nyakati za dinner.
Siku moja mkewe akamhurumia. Anachoka na kazi. Mtu gani asiyependa
starehe japo kidogo?

Mke akamlazimisha outing, Frank akabisha lakini taxi ikafika.
Gonga Club & Lodge.

Walipofika mlangoni tu, mlinzi akaita, "Mambo Frank!" "Poa"

"Nilidhani huwa huji club, inakuwaje mlinzi anakufahamu?"
Mke akauliza
Yule mgambo, mchana analinda ofisini kwetu, usiku anapiga part time
hapa" akajibu Frank

Wakachagua meza. Kukaa tu tayari mhudumu ameshaleta castle lager.

Akamuuliza mama anakunywa nini. Mhudumu alipoondoka mama akauliza,
"amejuaje unakunywa castle kama hakufahamu?"

Wakati Frank anajikanyaga aanze vipi kujitetea, mhudumu wa vyumba akawa
amefika na kuuliza.

"Mkuu kama kawaida nimekuandalia namba tano, nendeni tu vinywaji
Nitawaletea huko huko"

Kufikia hapo mama akawa hana simile tena, akanyanyuka akitukana kama
chizi. Akatoka nje mbio na kuingia katika taxi iliyokuwepo pale.

Wakati anapatana bei na dereva, Frank naye akaingia. Mama
yakamporomoka matusi kibao na kilio juu. Alipovuta kamasi na kupiga
kwikwi akamsikia dereva anasema.

"Duh, eee Mzee Frank huyu Malaya uliyeokota leo balaaaaaaaaaaaaaaa
Kuliko wa jana!!!!!!"
 
Asante lakini nilishairusha wiki mbili tatu zilizopita imetulia sana
 
maisha jamani....Heaven forbid!!!:A S 13::A S 13:
 
Kazi kweli kweli.... kwahiyo hiyo mazoezi ya basketball huwa ni balaa..................
 
Asante lakini nilishairusha wiki mbili tatu zilizopita imetulia sana

Na wewe uliitoa wapi DA, ila imetulia.... kumbe mazoezi ya basketball ni mazoezi ya kuchukua mademu duu!!!
 
na huyo mama nini kutafuta vitu vya kumuua akiviona
 
ha haaaaaaaaaaaa, usimsemee mtu ambaye huwi naye 24/7.
 
Frank nae, mazoezi ya Basket no Rum na 5.... duh!!!
 
kazi ipo sijui nisiolewe maishani manake nahisi ntamchinja mtu nikimfuma
 
Its a good joke na umeiweka kwa kiswahili kumatch mazingira tunayoelewa.

Imetulia
 
kama ingekuwa kweli nahisi huyo mama angezimia kwa shock!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…