wana blog wote,
wasalaam!,sita kukupotezea muda mwingi naomba sana munisaidie shida yangu
hii kwani nahisi dunia yote nimebaki peke yangu!!.kifupi mimi ni kijana
wa miaka 29 na nimesoma mpaka chuo kikuu,japo bado sijabahatika kupata
kazi.nilisoma shule ya bweni ya wavulana tupu,tangu kidato cha kwanza
mpaka cha sita.
Nilipokua shule tangu kidato cha kwanza nilifundishwa au kuiga tabia ya
kupiga punyeto (Masterburation).na ilikua ni tabia ya kawaida kabisa
hapa shule na kutokana na hilo hakika sikujua kama ina madhara yoyote.Niliendelea kupiga punyeto kuanzia kidato cha mpaka kitado cha sita mfululizo na nikawa adicted kabisa.Baada ya kujua madhara yake niliamua kuacha kabisa tabia hii na hili nimeliweza.Nilipofika chuoni niliingia kwenye uhusiano na msicha ambae nilmpenda sana na tulipendana sana.Nilipojaribu kushiri nae tendo,nilishindwa kabisa na sichukui muda hata wa dakika 1 nimeshamwaga!Hili tatizo liliendelea kujirudia mara nyingi sana katika uhusiano wetu na mpenzi wangu alikosa raha sana na kulalamika simlizishi katika mapenzi,na baada ya mudaakanichukia,mapenzi yakapungua na mwiso akaomba tuachane naakaniaacha!!. Nimekaa mwenyewe muda mrefu sana na najihisi mpweke sana,na sina raha.Je naweza kupata mtu wa kunipenda katika hali hii na kuyaelewa matatizo yangu na kuangalia jinsi ya kunisaidia?Je naweza kupata tiba ya tatizo hili?kwani hata sehemu zangu za siri zimesinyaa na imekua laini,na ukiamuka asubuhi inakua imelala tu!!.
naomba msaada wako,na kama kuna msicha yoyote yuko tayari kunipenda kwenye hali hii aniandikie kwenye e-mail yangu kulwa12@fastmail.fm
NAOMBA MSAADA WENU WADAU.
Kulwa 12, pole sana! Nianze kwa kusema hivi:
1. Rafiki yangu mmoja alikuwa akimwuguza kaka yake, ambaye ilitokea akawa kama kichaa. Baadaye huyu mdogo mtu naye akadhani ni kichaa (nadhani alianza kufanya mambo ya ajabu na watu wakaanza kumshtukia). Ilitokea kwamba nilipata nafasi ya kwenda likizo na nikaenda kumtembela. Akanisimulia yalimpata kaka yake na hali iliyokuwa imeanza kujitokeza kwake. Akavua shati na kunionesha mwili wake na jinsi ambavyo alishakwenda kwa waganga wa kila aina na kuchanjwa mwili mzima lakini haikusaidia kitu. Niliongea naye kwa muda wa saa 6 (six hrs) hivi na kumwambia kama angekuwa kichaa asingejitambua na kwa vile alikuwa anajihisi ni kichaa, niliamini siyo kichaa. Niliamini kuwa kichaa hawezi kujua kuwa ni kichaa! Hivyo, nilimshauri tukutane tena kwa mazungumzo zaidi. Nia ilikuwa kumwaminisha ili aamini kuwa siyo kichaa. Kitu kingine alichonieleza ni kwamba hakuwa anaweza kunusa kitu chochote kiwe cha manukato au kinachonuka vibaya kama choo kilichojaa! Basi ilibidi tuwe tunakutana mara kwa mara na hatimaye alianza kunusa vitu tena na akaamua kutoamini waganga waliokwishamlia hela zake nyingi na hadi leo jamaa ni mzima wa afya na kila nikimkumbusha hali yake tunacheka sana na tunaweza kuongea kwa simu hata kwa saa hivi.
2. Kulikuwa na jamaa mwingine pia alikuwa anatoka kwenye familia isiyo na uwezo sana na hivyo hali ya nyumbani kwao haikuwa ya neema sana. Huyu bwana kila nikikutana naye alikuwa anaonesha uso wa huzuni sana. Siku moja nikaenda nyumbani kwake ili nijue kitu gani kinaendelea kichwani mwake. Akanisimulia jinsi wachawi wanavyomtafuta wamwue. Nilimwonea huruma sana. Nikamwuliza anajuaje kwamba wachawi wanamtafuta. Akajibu pale nyumbani hafugi paka lakini kila mara anona paka wakikimbia na kupotea. Nyumba yake ilikuwa karibu na kichaka na ninavyojua kwa nyumba za vijijini lazima panya wawe wengi. Na hivyo niliamini paka walifika pale mara kwa mara siyo kwa kutumwa na wachawi bali kuwinda panya. Hata huyu bwana nilimwaminisha kuwa haumwi na wala hakuna mchawi anayemwinda isipokuwa amehusisha kuwepo kwa paka mara kwa mara pale nyumbani na wachawi. Naye ilibidi nimpe ushauri wa muda mrefu na hatimaye naye akapona tatizo lake na akaamini nilichokuwa namweleza ni kweli. Leo hii anaishi kwa amani na ana afya nzuri.
3. Rafiki mwingine naye alikuwa na shida kama yako. Naye alijizoesha kupiga punyeto muda mrefu tu tangu shule ya msingi hadi chuo kikuu. Hatimaye akapata tatizo kama lako na alikuwa anaona aibu kuwambia watu. Aliona ajaribu kuwa na mchumba lakini alikuwa anaepuka kufanya naye mapenzi. Siku moja alisema aliamua ajikakamue na alipofanya, siku hiyo mzee hakuamka. Yule rafiki yake wa kike akachukia sana na kumwambia kumbe alikuwa akimpotezea muda wake bure: "Unaonekana mwanaume kumbe ni mwenzangu? Niache na usinishike tena," alisema. Huyu rafiki yangu alijisikia vibaya sana. Basi ilibidi anyenyekee na kusema alipata mfadhaiko wa akili lakini kabla ya hapo alikuwa mzima tu. Alisema kila anapokuwa peke yake ajiona yuko sawa lakini akiamua kufanya mapenzi mapigo ya moyo yanaongezeka na hatimaye hali kama hiyo ikatokea. Baadaye aliamua kuoa kwani alikuwa anajiona ni mzima kabisa. Akapata mchumba, wakapanga harusi na hatimaye ikawa ndoa. Ila siku ya kulala na mke wake hali kama ile ya mwanzoni ikajirudia. Mkewe akamwambia: "Yaani uko hivi? Ina maana muda wote tutakuwa hivi?" Huyo bwana alisema hakujua cha kufanya. Kuanzia siku hiyo mke wake alikataa kulala naye tena - ikapita kama miezi 9 hivi bila kushiriki tendo la ndoa. Huyo bwana alisema kwa hali hiyo alianza kufikiri ni lini itawezekana tena. Alijaribu mitishamba ya kuongeza mbegu za kiume lakini haikusaidia. Kila akitaka kufanya ana'ejaculate' hata kabla ya dakika hivi. Baadaye alisema alifikiri sana na kusema: "Mungu wangu, kwa nini umeruhusu hali hii itokee kwangu?" Siku moja. alisema, akafikiri kuwa siyo mgonjwa ila tatizo lake limetokana na kuwa na mazoea ya punyeto. Aliamua kuacha kutumia dawa, ambazo aliona hazikumsaidia kitu. Akajiaminisha kuwa haumwi. Ilitokea siku moja alimwambia mke wake wafanye na walipofanya akaweza na hata baada ya kumaliza mzee alibaki amesimama na hata mke wake akamwambia kuwa amechoka wapumzike hadi kesho yake au siku nyingine. Huyo bwana aliniambia kuwa kuanzia siku hiyo hadi leo tatizo lake lilisha bila dawa ispokuwa kujenga imani kuwa yeye siyo mgonjwa, ni mzima!
Kwa mifano hii nataka nawe ukisoma ushauri huu uufanyie kazi. Usijali hata kama itachukua muda - ila amini kuwa uko sawa! Tatizo lako ni kwamba ubongo umesharekodi kupiga punyeto na ili urudie hali ya kawaida inabidi ufanye mazoezi: 1. Kila siku lala chali na weka mikono yako sambamba na miguu yako - ipe nafasi isigusane. 2. Funga macho na taratibu vuta hewa ndani (inhale kwa kutumia pua) na ikijaa sana iachie (exhale) taratibu kwa kutumia mdomo. Fanya hivi ukihesabu hata mara 50 hivi (kama una muda). Hili zoezi linakufanya uwe 'relaxed'. 3. Kama unasali, mwombe Mungu "akuponye" (akuondolee tatizo lako), ukisema Mungu amekuumba na kukubariki ili uishi kwenye familia na upate mwenza na unataka umpate huyo mwenza na ushi naye kama mume na mke na wakati kwa hali uliyo nayo sasa haiwezekani. 4. Fanya hivyo kila siku na usiwe na kikomo (fanya iwe sehemu ya ratiba ya maisha yako). 5. Tumia asali ya nyuki wadogo - vijiko 2 (table spoons) kila siku kila unapoenda kulala. Fanya hii iwe pia sehemu ya mlo au ratiba ya maisha yako. Nina hakika Mungu, atakusaidia! Ubarikiwe sana!