Sina raha

Maisha mafupi dada yangu. Kukosa raha sbbu ya mtoto wa mwenzio, haifai.
Na ili uwe na amani lazima hilo likutoke moyoni, na njia pekee ni kutell the truth.
HOW?
Kaa na mumeo and tell him the truth about all the incident ya siku uliotumia simu ya shoga yako. And tell him it was you and not her.
Then muulize alikuwa na maana gani kufanya hivyo? Then whatever the reaction atakayokuwa nayo, you keep coool and take time.
Ili mradi umelitoa moyoni na amejua kua ukweli umeujua.
Asikwambie mtu, hata km atakuwa mbogo kiasi gani, bado ule ukweli ulomwambia utamuuma sana, na utamtesa mno, labda awe GAIDI
 
Dada yangu pole sana. Najua machungu hayo na hasa kama ulikuwa unamuamini mumeo 100%. Nilishapatwa na janga kama lako lakini mimi mke wangu alikuwa na mahusiano na rafiki yangu wa karibu bila mimi kujua. Kuna siku alijisahau haku-logout email zake, nikachukua laptop kwa lengo lakutumia kama ilivyo kawaida huku mke akiwa jikoni. Kupitisha macho haraka haraka nikaona email yake moja ikiwa na kichwa cha habari "SWETIE" kuifungua ilikuwa inatoka kwa rafiki yangu kuja kwa mke wangu huku ikiwa na maneno mengi sana ya mahaba. Basi nikashikwa na shauku ya kuchimba zaidi. Kufungua sent na deleted messages nikakuta vitu vya ajabu sana ambavyo sikuweza kuamini. Nili-forward zote kwenye email yangu kama ushahidi. Nilishindwa kukaa nyumbani ilibidi nitoke kwenda kupata moja moto moja baridi huku nikitafakari kwa makini lile suala. Usiku nilirudi nimelewa ingawa si sana na nikapendekeza kwa mke wangu tuialike ile familia kwa ajili ya dinner wiki endi ifuatayo. Nilivumilia kwa muda wa siku sita, siku ya siku ikafika ile familia ikaja. Nilizi-print zile email ofisini mapema kabisa. Kabla chakula hakijawekwa mezani nikaanzisha lile suala, nikamuhoji mke wangu na yule jamaa mbele ya mke wake huku nimefunga milango yote. Kwa kweli walikataa na kuapa kwa nguvu zao zote, ndipo nilipotoa ushahidi wa zile emails. Mke wangu alianguka chini na kuanza kulia huku akikubali kosa na kuomba msamaha, rafiki yangu akawa hana la kusema zaidi ya kuomba msamaha huku akitetemeka ile mbaya. Mke wa jamaa naye akawa mbogo kwa mume wake na kwa mke wangu. Mwisho wa siku niliona ni hekima kubwaga manyanga mapema. Sikuona faida ya kuwa na mke ambaye si mwaminifu, nilikuwa mwaminifu 100%, alikuwa anajua kila kitu nifanyacho, ama ninapanga kufanya nini lini na kwanini. Alikuwa anajua rasilimali zote ziko wapi, tuna bank akaunti ngapi na zina kiasi gani. Ukweli nilijitahidi kumweka karibu na kumpa kila atakacho. Lakini pamoja na hayo yote namshukuru Mungu kwani bado niko hai na naendelea vizuri sana na shughuli zangu za utafutaji, mwanangu yuko na mama yangu mzazi kwa sasa. Sijui kama nitaoa tena na kama nitaoa sijui kama nitakuwa kama nilivyokuwa mwanzo.
 
Kama haujatunga hii story basi wewe nimwanamke uliyefundwa na uliingia kwenye ndoa ukijua umefuata nini!hukukurupuka hongera sana!nakushahuri mambo mawili!an option,siyo lazima yote!1=Kama unahiitaji ndoa yako mwite rafiki yako na maarafiki wengine amba mko karibu hata marafiki wa karibu na mmeo waalike dinner wakati mmemaliza kula mnapata drinks hakikisha hayo yote yanafanyika nyumbani kwako!Wambie unajambo unataka kuwambi usimame umwambie rafiki yako,"AshaDii nakupenda sana ila nakuonya na nakuambia achana na mume wangu na kuanzia leo wewe soyo rafiki yangu tena!!mgeukie mumeo mwambie mumeo kama unanipenda achana na rafiki yangu!!nimefahamu mda mrefu sasa nimevumilia sasa basi then nyanyua glass yako make cheers"Lazima wataishiwa nguvu naka atakuwa mstaarabu anaweza kukuomba sorry!
 
@Kipipi,Wala hujakosea sometime haya mambo huwa tunayakaribisha wenyewe mtu unakua close na mtu kuzidi hata ndugu yako,unamwamin mpaka kwa mumeo,wengine unakuta anahadithia mpaka ya chumban anavyofanyiwa na mumewe unakuta shost anaijua ndoa yen kuliko hata mwenyewe,nadhan huyu dada pamoja na kuongea na mumewe naye ajirekebishe aachane na mambo ya mashost kwan wengi co wazuri wana roho ya wivu tena saa ingine hauna maana zaidi ya kuharibia wenzao!
 
KWELI BIBIE INABIDI UBADILI TABIA,UTATUITAJE WANAUME HATUNA HAYA WALA AIBU???.........KUMBUKA WANAUME WA HAPA JF WALAAAAAAAAAA, HATUNA TABIA HIZO Auuuuu ulikuwa unazungumzia wanaume nje ya JF??
 
Fafanua hapa!Sijui kama wengine wamekuelewa mimi sijakuelewa!

Namaanisha uwezekano wa mumeo kum approach rafiki yako ni mdogo sana lazima ilikuwa rafiki yako ndio alikuja kwa mumeo so sioni sababu ya wewe kuvunja mahusiano na mumeo.
 
pole sana dada kwa yaliyokukuta ila usinge kaa kimya ungeendelea kuongea na mumeo ili ajue kuwa ni ww na umeshagundua kuwa anakusaliti na pia rafiki yako ungemuuliza palepale coz ulikuwa na evidance.Kwa sasa kaa chini na mumeo umueleze kila kitu ili ajue kuwa unaelewa nn kinaendelea kat yake na huyo rafiki yako mnafiki.pole sana
 
Asante mwaya. Simu yake ina password, hua hapendi niguse hata kama nataka kumpigia mtu na yangu haina salio.
Wote wanao cheat lazima simu iwe na pass-word na hurusiwi kupokea hata kama yeye mwenyewe hawezi kuwahi. iyo moja mbili you are lucky if you see it hanging around without his presence.
 
if was me Mis ningewaita wandugu wa karibu(hasa hasa wale wambea ili waeneze habari na kwa wengine) na pia wazazi wa huyo shosti niweke issue hadharani then nitoe my decision. 29 yrs safari bado ndefu
 
Pole saana dada sijui nikushauri nini
 
Thea is no nid of biting around the bush, mi ningewakutanisha wote I min huyo anayejiita mume wangu na huyo "rafiki" kisha nawachana bila chenga, coni 7bu
ya kufanya vinginevyo.
 
KWELI BIBIE INABIDI UBADILI TABIA,UTATUITAJE WANAUME HATUNA HAYA WALA AIBU???.........KUMBUKA WANAUME WA HAPA JF WALAAAAAAAAAA, HATUNA TABIA HIZO Auuuuu ulikuwa unazungumzia wanaume nje ya JF??

hahahaha umeamua kuwa mtetezi wa haki za wanaume?
 
pole sana, huwa yanatokea..mara nyingi wezi wa waumea au wake za watu ni wale marafiki wa karibu
 
dada ongea vizuri na mumeo myamalize umsamehe maisha yaendelee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…