Sina ujasiri wa kuacha kazi

Usiache kazi
 
Asante kwa ushauri kuna kitu kipya umenipa hapo, likizo isiyo na malipo nitalifikiria hili.
 
Asante sana mama yangu, nalifanyia kazi
 
Nikuambie kitu, katika haya maisha jaribu usiwe mtu wa negativity.

Anyway mimi sio tajiri, ila naweza kukidhi mahitaji yangu so nimeridhika na hali yangu
 
Hakuna kazi ngumu kama kuacha kazi, achilia mbali wewe uliyepo kwenye well-paying job, hata anayepata 150k kwa mwezi bado anaona shida kuacha kazi, so it's very understandable.

Kazi inakupa security, ona hata familia inakushangaa unaachaje kazi wakati wao wanaona kazi yako inawasaidia hata wao.

Lakini hili ni lako na mumeo, wengine ni observers na washauri tu. Kama wawili mnaamua mnaweza kuishi bila ajira rasmi, mnaweza kujilipia health insurance kupitia biashara zenu, mnaweza kuendesha maisha yenu na vipato visiathiri maisha yenu, elimu za watoto na maendeleo mengine, unaacha tu.

Changamoto ya biashara, nyingi hazina long lifespan, yaani sisi waafrika hatuwezi kuweka mazingira mazuri ya kuendesha biashara kwa miaka 50 ijayo.
 
Watu huwa wanawaza mara mbili kuacha kazi kwakuwa hawana uwakika na kipato chao kama kitakuwa endelevu au laa! Kwa maana hawana uwakika na biashara kama itafanikiwa au kuanguka.

Lakini kwa upande wako naona uko vizur kwanza una vyanzo vya mapato zaidi ya kimoja na vyote kwa mujibu wa maelezo yako vinafanya vizur,ninachokiona kwako ni hofu na mazoea tu,kwahiyo ni muda wa kufanya maamuzi ya kuacha kazi.


Naomba next month by July uje na uzi tayar umeacha kazi.​

All the best.
 
Je una mental illness?
Yaani una Pata hela nje ya kazi na inazidi?
What the *** are you waiting for..

Anyways nakujua pm tuyajenge, mimi Natafuta lishangazi gen z wamenishindaa
 
Mume wangu aliniachia maamuzi nifanye mwenyewe.

Hata leo nikimuambia nimeacha hana neno ila naogopa tu.

Yeye ni muajiriwa na Mfanyabiashara pia, yeye hana mpango wa kuacha.
 
Nitakuja hapa kutoa mrejesho December Mkuu.
 
Sasa si uache kazi kama haina faida yoyote kwako, usitupigie kelele humu
 
Ajira ni ulevi kuacha ni tatizo
Ningekuwa wewe ningemtrain kijana wangu afanye kazi hizo za kujiajiri badala yangu ili mimi nibaki na kazi za serikali.
Namaanisha ni bora kukamatia ajira moja mliyonayo kuliko kijana wako anaendelea kufight kusoma kutafuta ajira za serikali wakati ajira nyumbani zipo.
Kiuhalisia mali mnazotafuta ni za watoto sasa kama ni hivyo kwa nini na watoto nao wasishiriki kuzitafuta angali mko hai
 
Mume wangu aliniachia maamuzi nifanye mwenyewe.

Hata leo nikimuambia nimeacha hana neno ila naogopa tu.

Yeye ni muajiriwa na Mfanyabiashara pia, yeye hana mpango wa kuacha.
Wewe uliazimia kuacha by 40, mimi ningekushauri uende hadi 50. Utapata mda wa kuunganisha maisha ya ajira na biashara 50-65 hapo.

Swala hapo ni malezi ya watoto ambao naamini unawalea remotely, kama wanalelewa vizuri sioni haja ya kuacha kazi mapema hivi. Mume utamlea tu hata kama unafanya kazi, kwani haridhiki na muda unaompa.
 
Biashara yako wateja hawaji kwa sababu ya cheo chako ofisini au ofisi yako?

We inaonekana siyo shap kwenye mambo yako.Maana ukiwa shap unapata muda wa kukaa na watoto maana ila ukiwa slow unachelewa kufika home.

Ofis yenu ipo mkoani km unaweza uhamie huko ili uondokane na heka heka za usafiri uwahi kufika na kurudi

Miye nikisema naacha kazi Mama yangu tunampoteza.
 

Kwa ulipofikia na kwa kuwa Mume wako pia anafanya kazi, unaweza kuacha na pengine kusimamia vizuri zaidi hizo biashara zako. Naomba pia kirefu cha FDR (sisi watu wa zamani kidogo tunapitwa na baadhi ya codes)

Kama ni shirika Binafsi; Andika tu barua ukiwapa pengine miezi tatu (Kulingana na nafasi yako) kuwa unaomba kuacha kazi. Ni vizuri kuacha kazi vizuri na usiondoke kibabe, kwani kuna kesho.....
Sababu; Mume wako yupo mbali kikazi hivyo unatamani kuungana naye ili mshirikiane kwenye malezi ya watoto.

They way you handle responsibilities is truly impressive; You are thoughtful, reliable, and clearly grounded in your values. Hongera sana!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…