Sina ujasiri wa kuacha kazi

Kama umejiweza vilivyo m ushauri wangu ni bora uache kazi usimamie biashara zako angali saivi una nguvu zako ukifika 60 ubavu huo huna tena kama sasa

Ongeza familia watoto wawili ni kidogo sanaaa fikiria kesho yako usijekosa ata wa kumtuma dukani
Wazo la kupata watoto ili update wa kumtuma dukani ni la watu suni Sana.
 
Wazo la kupata watoto ili update wa kumtuma dukani ni la watu suni Sana.
Hiyo Kauli ya kumtuma dukani ni usemi Tu wa kisoaholojia, uelewe kwamba swala la kuzaa watoto ni muunganiko wa sababu mbali mbali, ikiwemo za KiAnthropolojia, sosholojia, uchumi na kiimani, hakuna jibu la moja kwa moja kwenye swala hili
 
Uhuru wa kifedha kiuhalisia haupo duniani ni misemo Tu ya Inspirational speakers, Dpw bado wanagangaika,😅😅
 
Pole Sana, huwa iko hivyo siku zote ukitaka kuchukua maamuzi yatakayo badili uelekeo wa maisha yako, ni hofu Tu Inakuja hata haijulikani inatoka wapi..

Unajua katika suala lako Hilo jiangalie wewe kama wewe Kwanza, usifikirie mambo ya "itakuaje" au "kitatokea nini au watu watafikiriaje", siku zote kwenye Jambo kama lako hakuna siku itakayotokea utakuwa na huo ujasiri, usipochukua hatua mapema utabaki na wazi Hilo Hilo Hadi unakaribia kustaafu utabaki na zile "ningefanya Tu".

Ujasiri huwa hauji hivi hivi Bali hutengenezwa ndani yako Kwa kujivika utayari, ukishaacha Tu kazi baada ya miezi kadhaa Kila kitu utaona Kipo kawaida na maisha yataendelea...

Ukikaa chini na kutafakari na ukajiona kweli Niko tayari basi usisite, Fanya maamuzi hapo hapo, hakuna mtu yoyote Yule duniani ambaye amefanya maamuzi muhimu ya maisha Yake halafu kwenye huo mchakato wa kufanya maamuzi akajihisi comfortable lazima tu hofu na kukosa nguvu vinakuja but huwa tunakuwa wabishi na Ku move on, lazima uwe mbishi...

Sisi tuliokulia kwenye kujiajiri huwa tunaelewa Sana mambo yalivyo, sometimes kuna maamuzi makubwa ya biashara ambapo mambo yakienda vibaya basi unaanza moja, unafilisika but tunakomaa licha ya kuwa na hofu lakini tunakuwa wabishi tunasonga mbele....maamuzi mengi tumefanya Tukiwa hatuna uhakika but ni guts Tu.

Self belief ni muhimu Sana kuwa nayo, siku zote hakuna muda sahihi wa kufanya maamuzi kama hayo, lazima Tu utajawa na hofu...Na kinachokufanya hofu izidi kuwa kubwa ni kwamba Una Options, kama ungekuwa Huna option basi usingefikiri mara mbili ungejitosa moja Kwa moja kwenye biashara...
 
Ndugu yangu si unaijua JF ilivyo???

tunashindwa kuwa wawazi sababu tunaonekana waongo, tunajivuna na mengine mengi.
 
Asante sana Mkuu kwa ushauri Mzuri.

Nitakuja siku kuleta ushuhuda
 
Dadangu hakuna binadamu anayetosheka ni vile tuu sijui inakuaje

hao watoto unafànya kazi kwa ajili yao, wapambanie tuu

Huyo mume nae hapo ndo balaa siku mmepishana kiasi utawaza mengi

Usiache kazi dearest sis, we love you pambana familia ile,y
Nimependa ujumbe wako ulivyoandika kwa upendo, asante.

Kupishana kwenye ndoa kupo kaka angu ni kawaida.

Kazi inanibana pia upande mwingine, kuna muda natakiwa nisafiri nikafuate mzigo nashindwa, kuna muda natakiwa nisafiri niende mwenyewe viwandani nashindwa.

Taasisi itaruhusu kwa mwaka usafiri hata mara tano ukakae week mbili au tatu!?? Nishadanganya kuomba ruhusa mpaka sababu zimeisha.
 
Ila naona ni vyema mwanaume ndo aache kazi asimamie biashara,ila siyo mwanamke.

Namaanisha kama wote wawili mume na mke ni waajiriwa,nk vyema mume ndo aache.
Kila mtu na biashara zake yeye anasimamia za kwake na mimi za kwangu.

Hatuingiliani, nilifanya hivi ili nijipime kuna mtu kufa, pia kaumwa je naweza kusimama mwenywe? Naweza kutafuta pesa na nikahudumia familia?
 
Kila mtu na biashara zake yeye anasimamia za kwake na mimi za kwangu.

Hatuingiliani, nilifanya hivi ili nijipime kuna mtu kufa, pia kaumwa je naweza kusimama mwenywe? Naweza kutafuta pesa na nikahudumia familia?
Sawa,
 
Unaogopa nini ukiacha kazi?
 
Apply sabatical leave. Nenda kaoamgalie uraiain pakoje. Wenzako tunazeekea humo.kila ukiwaza unachanganyikiwa
 
Kama hvyo mume anakosea apo mwanamke anatamani kuacha kazi ili amuhendo mume wake apate muda nae....

Mume nae anapaswa aoneshe msimamo wake mana wanawake kwenye issue za misimamo sio wazuri..... Wanatumia sanaa hisia
 
FDR ni Fixed Deposit huko Bank

Ambapo unaweka hela then wanakupa riba mfano unaweza pewa asilimia 13-14 ya pesa zako kwa mwaka na hela yako inabaki pale pale.
SIKIA KWA MAKINI,

Kama huna vitu vifuatavyo endelea kuwa mtumishi;

1.Nyumba za kupangisha angalau nne ambapo kila moja inakupa walau million 18 kwa mwaka,kwa zote nne millioni 72.Endelea kufanya kazi tena ongeza bidii.

2.Biashara ya LODGE au gesti angalau LODGE au GEST 3.

3.Uwe na pesa UTT walau millioni 50 hizi ziwepo tu huko, umeziweka kama akiba.

📌Kama huna hivi vitu 3 walau hata 2 kati ya hivi usiache kazi.


Kama unavitu unafanya tofauti na nyumba za kupangisha na lodge.Hizo sio biashara wewe ni machinga tu. Hata kama umekodi vifremu hizo biashara huwezi tegemea kabisa ni very VOLATILE.Fanya kazi kwa bidii walau ufike miaka 55 ustaafu kwa hiyari ambapo utapata na stahiki zako zote.Ila tofauti na hapo USIJARIBU MAANA NI VERY RISKY!!!!


📌UCHUMI WA HII NCHI HAUTABIRIKI!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…