Sinaga Swaga inairudisha Hip Hop ya Bongo kwenye mstari wake – Young Killer

Sinaga Swaga inairudisha Hip Hop ya Bongo kwenye mstari wake – Young Killer

STUNTER

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2015
Posts
13,076
Reaction score
17,247
Rapper Young Killer anadai kuwa wimbo wake
mpya, Sinaga Swaga umekuja kuirudisha ‘real hip
hop’ kwenye mstari. Amedai kuwa kipindi cha hivi karibuni rappers
wengi wa Bongo wamekuwa wakilegeza ngoma
zao ili kuvutia biashara, lakini yeye ameamua
kukaza.

“Dhumuni la kufanya hii ngoma, nimetaka
kuwaonesha kwamba hip hop yetu bado ipo na
ina nguvu kubwa na ina uwezo wa kufika mbali
zaidi ya hapo ambapo ipo endapo tutaendelea
kuisupport na kuipa nafasi,” rapper huyo
amemuambia mtangazaji wa Pride FM, Eddy Msafi.

Rapper huyo amesisitiza kuwa masikio ya
mashabiki wa muziki Tanzania yanahitaji ngoma za
aina ya Sinaga Swaga na si kupewa nyimbo za
kuimba na kuchezeka tu.
 
Mimi nimekuta hiloneno la "Sinaga swagga" kwa bae nikashangaa hii Status kaitoa wapi....

kumbe young killer kasababisha
 
wimbo wa kawaida sana, sina swaga ya kuusikia mara nyingi nyingi aisee na kichupa hakiko vizuri sana ila kajitahidi
 
Kitu hata kiwe sio cha kawaida ukikiwekea ukawaida kitakua cha kawaida tu hta km sio cha kawaida
naona umesifiwa kukimbia umepitiliza hadi kwenu........kila mtu anamtazamo wake na huo ndo wangu ww pia unao wako
 
Ni wimbo mzuri ila bado haujafikia ubora wa Young Killer yule wa Dear Game,Jana na Leo au August 13.

Kikubwa nilichokiona humu Ni kaamua kuja name style ya Ney wa Mitego kaamua kuwaponda watu Kwa kuwataja majina labda anatafuta Attention ya watu.

Wimbo wa kawaida afate ushauri wa wanaomkubali arudi Kwa Mona Gangster kuanza upya si utumwa.
 
Ww mpenda taarabu umekuja hadi huku.......
 
Obviosly Huu wimbo tangu juzi ulipotoka nauskiza, na kwa siku naeza nikaurudia hata zaidi ya mara 20....
Me kama dozi mkuu... asubuhi mchana na jioni bila kusahau usiku

Nimeukubali sana
 
Ni wimbo mzuri ila bado haujafikia ubora wa Young Killer yule wa Dear Game,Jana na Leo au August 13.

Kikubwa nilichokiona humu Ni kaamua kuja name style ya Ney wa Mitego kaamua kuwaponda watu Kwa kuwataja majina labda anatafuta Attention ya watu.

Wimbo wa kawaida afate ushauri wa wanaomkubali arudi Kwa Mona Gangster kuanza upya si utumwa.

Sidhani kama ataweza kurudi kwa Monami. Labda.
 
Back
Top Bottom