Sindano ya Tetenas haipatikani hospitalini

Lyatuu the Great

JF-Expert Member
Joined
Nov 5, 2013
Posts
212
Reaction score
85
Sikuwahi kufikiria kuna siku hospitali zetu zitakosa sindano muhimu kama hii ya tetenas teba haoa Dar. na wizara ya afya ikakaa kinya bila hata kutoa tamko au kutujulisha wananchi juu ya uhaba huu wa sindano ya tetenas na ni muhimu katika hospitali zetu.

Ni jana tarehe 22/3/2016 mke wangu aliumia mguu kwa kukatwa na bati ikabidi nimwambie aende hospitali sinza palestina akapata matibabu ila akakosa huduma ya sindano ya tetenasi akaagiziwa aende hospitali nyingine ndipo alipojaribu zahanati za jirani kama AAR Sinza madukani ila pia akakosa huduma hiyo.akajaribu zahanati nyingine ikiyoko njia ya sinza kijiweni kwenda tandale pia akakosa huduma hiyo Akarudi nyumbani.

Kwa bahati nzuri nilikuwa ndio narudi nyumbani kuchukua baadhi ya nyaraka niendelee na kazi zangu za siku aliponiambia nikamuambia tuongozane wote kwenye hospitali zaidi kutafuta hufuma hii ya sindano ya tetenasi tukaanzia mwanamyamala tukakosa dipensary zote pia wanasema wameshapeleka mahitaji ya sindano ya tetenas ila hawajaletewa.

Dawa bado nilihangaika hospitali na zahanati mbalimbali bika mafanikio mwisho tulipewa wazo la kununua dawa hiyo kwenye phamarcy ya nakiete iliyopo mwenge ndio nikapata.Naiomba wizara ya afya kupitia kwa waziri wake Ummy Mwalimu na Naibu wazuri Dkt Hamis Kigwangala wajitahidi dawa muhimu kama hii iwe inapatikana kwani ni hatari kwa kukosekana kwa dawa hii katika hospitali na zahanati pia.
 
ni kweli haipatikani yani maisha haya mbona tutasoma na namba za engine.
 
Yaani jana nimesumbuka sana tangu saa 7 mchana hadi jioni ndio napata dawa hiyo tena kwa kununua. Wizara ya afya ijitahidi kulitatua hili kwa haraka
 
Nenda kwenye clinic yoyote ya mama na mtoto huwa zipo ila kuna siku maalum ya kutolewa
 
Nilizunguka hata clinic hakuna na tena clinic ndio wanasema hata chanjo tu za watoto kuna baadhi ya chanjo hawana na hawajaletewa licha ya kupeleka listi ya mahitaji tayari
 
Rais kasema tufyatue watoto tu!!! Wao mambo ya afya hawajui...ela zimepelekwa kuimarisha policcm ili kuzuia UKUTA
 
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16] eti hela zimepelekwa wapi?
 
Huku kwetu bunju tangu mwezi wa tano mwaka huu hiyo sindano haipatikani, si hospitali za serikali wala za binafsi. Nilipata ajali ya kuchomwa na msumari nilihangaika mpaka basi, nikaikosa.
 
Wapo busy na kuhamia Dom....

Kuna mahali niliona wajawazito wakilalamika hiyo chanjo haipatikani hospitalini pia
 
Hata muhimbili hamna hiyo sindano kuna mtu namjua ameikosa jana,kesho ndio anataka akajaribishe regency!
 
Kwa wenzetu hii pekee ilikuwa sababu tosha ya hao viongozi wa wizara ya afya kujiuzulu...kwetu ni business as usual!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…