Sindano za makalioni; wale tusiopenda /waoga wa hii kitu tukutane hapa.

Mwanzo nilikuwa sipendi japo pia nilikuwa siogopi sindano. Baada ya kupata ajali nilizizoea kabisa sindano. Tena kuna moja nilikuwa nikidungwa kwenye paja nasikia maumivu yote yameisha na ku-relax kabisa. Doctor wangu aliniambia haitakiwi kuizoea kwani inaleta u-teja na inatumika pale tu mgonjwa anapokuwa na maumivu makali sana. Mpaka sasa sindano kwangu we choma upendavyo siogopi kabisa.
 
Yupo mmoja pale KAIRUKI... alinchoma sindano ya TACKLE.... yaani mpk anamaliza kupress dawa mm sina habari...
Hahahaaaaaa.

Huyo ni sawasawa na mmoja nilipatiwa huduma naye pale Sanitas
 
Mimi mpaka leo nikienda hospital nikimuona doctor anaanza kuhangaika na masindano namwambia achana nayo
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mie sipendi sindano yoyote ile, wala dawa yoyote ile Mungu nisaidie nisiugue.

Nikiwa kidato cha kwanza mwaka 1980 niliandikiwa sindano za masaa, nakumbuka nilichoma moja tu. Zingine sikurudi tena na nyumbani walikuwa wanajua nilikuwa nakwenda kuchoma kumbe naishia njiani.
 
Aisee sindano siipendi yani niko lazi ninywe paramangret kuliko kuchomwa sindano

Kuna siku nilikua naenda kununua dawa kwenye zahanati moja hapa kitaa, docta akananishauri nipime ili nipate uhakika wa ninachoumwa kuliko kuchukua dawa bila kujua.

Nikamkubalia nikamwambia ila kwa sharti moja tu usinichome sindano. doctor akatahamaki akasema haiwezekani ukapimwa bila kuchukuliwa damu, nikamwambia kama shida yako damu basi usijari kuna kakidonda mguuni niliumia jana kama vipi tuchukue damu hapo hapo kuliko kutoboa sehemu nyingine kuniongezea kidonda cha makusudi.
 
Sasa yani uko form three afu bado bikira jamani? Unataka hiyo biology izibe?

Au kwani hapa inazungumziwa sindano ipi???
Babu unazeeka vibaya ujue, akili zimerudi utotoni kabisa[emoji3] [emoji3] , mleta uzi kasema zile sindano zinazowekwa dawa kulingana na umri Wa mgonjwa arrgh
 
Babu unazeeka vibaya ujue, akili zimerudi utotoni kabisa[emoji3] [emoji3] , mleta uzi kasema zile sindano zinazowekwa dawa kulingana na umri Wa mgonjwa arrgh
Hahahaha nisamehe mjukuu. Unajua sisi wazee wa zamani tushazoea kuongea kimafumbo. Kumbe hapa inazungumziwa sindano ya mahospitalini?

Basi hebu upelekeni huu uzi jukwaa la utabibu...
 
Asante sana nesi kwa kutujulisha hili
 
Hahahaha nisamehe mjukuu. Unajua sisi wazee wa zamani tushazoea kuongea kimafumbo. Kumbe hapa inazungumziwa sindano ya mahospitalini?

Basi hebu upelekeni huu uzi jukwaa la utabibu...
Hahaaaa, babu wewee enzi zenu kulikua na sindano gani zingine tofauti? [emoji3] [emoji3] ,babu nimekushindwaaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…