Bubu Msemaovyo
JF-Expert Member
- May 9, 2007
- 4,120
- 3,468
Waheshimiwa wana JF Nimeleta taarifa hii ambayo chanzo chake ni WAPO FM inayosema kwamba hapo jana mnamo majira ya saa kumi jioni maeneo ya Kinondoni Mkwajuni Bondeni kulitokea mauaji. Tukio hilo linasema chanzo ni mzozo uliojitokeza kati ya jamaa mmoja mwenye asili ya Asia (Singasinga) ambapo wakati wakiwa katika vyombo vyao vya usafiri Singasinga akiwa kwenye pikipiki na mtu mwingine ambaye sasa hivi ni marehemu akiwa katika gari aina ya Toyota Carina.
Inasemakana singasinga huyu alitaka kulipita gari lililokuwa limeharibika mbele yake na kwa bahati mbaya akaanguka barabarani na katika harakati za kumkwepa huyo jamaa ambaye ni marehemu akabamiza gari lake kwenye kingo za barabara na kupasuka gurudumu. Alimwendea ili kumdai amlipe kwa kusababisha ajali ile hususani gurudumu kupasuka. Singasinga yule aliinuka akiwa na chupa ya kilevi aina ya wine akiwa anakunywa, ubishi ulipokolea alichomoa bastola yake na kumpiga kichwani yule mwenye Carina na kupanda pikipiki yake na kutoweka. Wananchi walioshuhudia tukio hilo kwa bahati mbaya hawakuweza kuchukua namba za pikipiki ile.
Kupitia JF nikiamini ni mtandao mkubwa ningeomba tujitahidi kutafuta taarifa na mwenye usahihi wa namba au kumfahamu huyo Singasinga atoe vyote hapa JF na bila shaka makachero wa polisi ambao ni wanachama wa JF watashughulikia.
Nawasilisha.
Asanteni.