Singida Big Stars tumejiandaa kuwakabili Prisons kesho, watajua hawajui

Singida Big Stars tumejiandaa kuwakabili Prisons kesho, watajua hawajui

Hussein Massanza

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2012
Posts
1,016
Reaction score
2,195
Watu wa Soka,

Tumejiandaa vya kutosha kuanza mchezo wetu wa kwanza wa Ligi Kuu kesho dhidi ya Tanzania Prisons.

Mashabiki wetu tunawakumbusha kukata tiketi mapema kupitia N-CARD kisha mjitokeze kwa wingi uwanja wa LITI (zamani Namfua) kesho mapema sana kuisapoti timu yetu. Hakutakuwa na tiketi za mkononi.

Mechi itaanza SAA NANE KAMILI MCHANA.

IMG-20220815-WA0010.jpg
 
UPDATE

Mazoezi ya mwisho mwisho leo kabla ya mechi yetu na @prisonssc kesho saa 8 kamili mchana. Tiketi za mechi zinapatikana kupitia mfumo wa kisasa wa N-CARD pekee! Kata mapema. Fika mapema.

FaMi8NgWQAMzo-5.jpg
FaMi9-cXwAEGGDu.jpg
FaMjA4fXkAIVeYm.jpg
FaMi_74WIAI6RBA.jpg
 
Kwani nani Ni mmiliki wa hii timu na kwann isingebaki Kua timu ya benki tu
 
Hawa Singida Big Stars, very soon. Tutaisahau Yanga na Simba

Singida Big Stars ni hatari fire
Cheza na Wote ila siyo Simba na Yanga. Kama Timu Kubwa za Mecco FC, Pamba FC, Sigara FC, Kajumulo FC baadae Tanzania Stars na Moro United tena iliyokuwa chini ya Tajiri Mkubwa wa Mafuta Merrey Balbouh zote zilisambaratishwa na Nguvu ya Simba na Yanga ndiyo itakuwa hii Singida Big Stars FC yenu?

Hii ni Timu ya Kisiasa na itakuwepo hadi 2025 ila baada ya Kiongozi wa Serikalini Waziri wa Wizara Muhimu ambayea naimiliki japo anajitahidi mno Kuficha akishashinda tu Ubunge hii Timu nayo itasambaratika kwani hata huko nyuma kabla ya kubadilishwa Jina huu Mchezo ulifanyika.
 
Big up, mmeonesha uwezo....
Nitaipima Singida Big Stars baada ya Mechi 7 za mwanzo na nashangaa kuona Watu ndani ya Mechi moja tu mnawapa Jeuri hivi wakati Soka la Tanzania linajulikana jinsi lilivyo na Mazingaombwe na Upanjuani Upanjuani mwingi tu.
 
Hii timu haina kiungo mkabaji wa kueleweka, pia ukimuondoa Peter Cruz na Dario Singida inabaki majina tu.

Ni timu ya kawaida mno, sitarajii maajabu yoyote.
 
Watu wa Soka,

Tumejiandaa vya kutosha kuanza mchezo wetu wa kwanza wa Ligi Kuu kesho dhidi ya Tanzania Prisons.

Mashabiki wetu tunawakumbusha kukata tiketi mapema kupitia N-CARD kisha mjitokeze kwa wingi uwanja wa LITI (zamani Namfua) kesho mapema sana kuisapoti timu yetu. Hakutakuwa na tiketi za mkononi.

Mechi itaanza SAA NANE KAMILI MCHANA.

View attachment 2324288
Jezi tu za hii timu kwa hapa nchini hutaabiki kufahamu ni ya mlengo upi.
 
Tafteni beki kabla dirisha halijafungwa mtakuja kutia aibu...!!wawa hajawahi kuwa beki haya SHAURI YENU
 
Back
Top Bottom