Singida Big Stars tumemsajili Kipa wa Taifa, Metacha Mnata

Hussein Massanza

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2012
Posts
1,016
Reaction score
2,195
Watu wa Soka,

Leo ninafurahi kuwajuza kuwa Mlinzi Imara kutoka Timu ya Taifa #TaifaStars asiye na presha na mechi ndogo wala kubwa, Metacha Mnata, ametuhakikishia kuwa lango letu litakuwa salama kupitia uzoefu wake.

Tayari tumeinasa saini yake na atakuwa nasi kwa mkataba wa miaka miwili katika nafasi ya GoliKipa.

Karibu Singida Big Stars, Kipa wa Taifa, Metacha Boniphace Mnata.

metacha2.jpg
 
Hongereni SINGIDA Big Star. Naamini kwa usajili mnaofanya mtaleta ushindani kwenye ligi.

Ila tu mkumbuke Kuna Mnyama,#Nguvumoja hatuachi kiumbe au masalia, tunararua.
 
Shaibu Ninja, Kaseke na Yassin chukueni pia watawasaidia!

Feisal Salum kaletewa wachezaji kibao nafasi yake, mkiona anawekwa benchi kule Yanga mchukueni kwa mkopo aimarishe safu ya ushambuliaji!
 
Asante kwa ushauri mkuu
 
mkitaka mfike mbali kwenye timu yenu ondoeni ushabiki na timu kubwa izi mbili simba na yanga ili yasije yakawatokea kama ya mbeya city viongozi wote wahandamizi walikuwa kijani tupu kilichotokea mpaka leo wote tumekiona
 
Hii timu ina malengo mazuri na najua mkikomaa mtabaki ligi kuu na mtafika mbali. Jifunzeni kwa geita gold, polisi tz, ruvu labda mtatoboa. Mkileta uyanga kama singida united na mbeya mimi mwanasimba natangaza laana kuu kwenu. Mwigulu atasababisha hiyo timu ichukiwe na watu kwa uyanga wa kitopolo. NAWACHEKI TU ILA MKIJICHANGANYA NAWALAANI.
 
Hongereni. Ni usajili mzuri. Metacha Mnata ni mlinda mlango mzuri.

Binafsi sikufurahia kabisa kuondoka kwake Yanga kipindi kile. Maana angevumilia kidogo tu zile changamoto, mpaka wakati huu huenda angekuwa ndiyo Tanzania One wetu.
 
Hongereni SINGIDA Big Star. Naamini kwa usajili mnaofanya mtaleta ushindani kwenye ligi.

Ila tu mkumbuke Kuna Mnyama,#Nguvumoja hatuachi kiumbe au masalia, tunararua.
Kama mlivywararua Mbeya City na Kagera Sugar msimu uliopita.
 
Hii timu ina malengo mazuri na najua mkikomaa mtabaki ligi kuu na mtafika mbali. Jifunzeni kwa geita gold, polisi tz, ruvu labda mtatoboa. Mkileta uyanga kama singida united na mbeya mimi mwanasimba natangaza laana kuu kwenu. Mwigulu atasababisha hiyo timu ichukiwe na watu kwa uyanga wa kitopolo. NAWACHEKI TU ILA MKIJICHANGANYA NAWALAANI.
Ulishindwa nini kuipa laana Yanga isichukue makombe matatu mikononi mwenu au kuzilaani Mbeya City na Kagera kwa kuwafunga?
 
Hongereni. Ni usajili mzuri. Metacha Mnata ni mlinda mlango mzuri.

Binafsi sikufurahia kabisa kuondoka kwake Yanga kipindi kile. Maana angevumilia kidogo tu zile changamoto, mpaka wakati huu huenda angekuwa ndiyo Tanzania One wetu.
Kama Tanzania one wenu sawa, ila sio wa taifa zima kiujumla.
 
Mkimcheleweshea mshahara tu mjiandae na "dole la kati", waulizeni utopolo hawana hamu nae
 
jiangalieni sana nyie wasingida, huyo dogo ni kipa mzuri sana ila sasa mkae mkijua huyo dogo ni duka, badaye msije mka lia
 
Hongereni. Ni usajili mzuri. Metacha Mnata ni mlinda mlango mzuri.

Binafsi sikufurahia kabisa kuondoka kwake Yanga kipindi kile. Maana angevumilia kidogo tu zile changamoto, mpaka wakati huu huenda angekuwa ndiyo Tanzania One wetu.

Asante sana mkuu. Yes Metacha ni kipa na nusu.
 
Watu wa Soka,

Leo ninafurahi kuwajuza kuwa Mlinzi Imara kutoka Timu ya Taifa #TaifaStars asiye na presha na mechi ndogo wala kubwa, Metacha Mnata, ametuhakikishia kuwa lango letu litakuwa salama kupitia uzoefu wake.

Tayari tumeinasa saini yake na atakuwa nasi kwa mkataba wa miaka miwili katika nafasi ya GoliKipa.

Karibu Singida Big Stars, Kipa wa Taifa, Metacha Boniphace Mnata.

Kaka kumbe mlimsajili akiwa hajamaliza mkataba na POLISI?
 
Back
Top Bottom