Singida Big Stars tunaanza Ligi na Tanzania Prisons, patamu hapo

Singida Big Stars tunaanza Ligi na Tanzania Prisons, patamu hapo

Hussein Massanza

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2012
Posts
1,016
Reaction score
2,195
Watu wa Soka,

Salamu kutoka Singida Big Stars.

Ratiba ya Ligi Kuu imeshatoka na mechi yetu ya kwanza tumepangiwa kucheza uwanja wa nyumbani na Wajelajela Tanzania Prisons siku ya Jumanne Agosti 16, 2022.

Nafahamu kwamba Mashabiki wetu, watanzania na watu kutoka mataifa mbalimbali siku hizi wanapenda kufuatilia timu yetu kila inapocheza, hivyo ratiba hii iwaongoze kujiandaa kutazama mechi ya Jumanne ambayo itakuwa ni ya kwanza kwetu baada ya kufuzu kuingia Ligi Kuu..

Prisons tunawaheshimu, lakini mipango yetu ni mikubwa zaidi kwahiyo tutacheza mpira mzuri wenye kusaka point 3 za mapema mapema ili tusonge mbele.

Tutarudi hapa kupeana matokeo!

KIKOSIII.jpg
 
UPDATE: Azam TV tayari wameshawasili hapa Singida kuhakikisha wanarusha MUBASHARA matukio yote kama ilivyo ada!
 
UPDATE 2: Dario Frederico atajumuika na kikosi katika mazoezi kesho asubuhi baada ya kupona majeraha madogo aliyoyapata katika mechi na Mtibwa Sugar.
 
Back
Top Bottom