Singida Black Stars wamepiga hatua kubwa kwenye Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kushinda mechi yao ya pili mfululizo kwa kuilaza Rayon Sports ya Rwanda 2-1 kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam. Baada ya ushindi huo, Rais Samia Suluhu Hassan aliwazawadia shilingi milioni 10 maarufu kama “Goli la Mama” ikiwa ni sehemu ya hamasa na motisha ya kuendeleza ushindani wao barani Afrika.