Singida BS wamsagia kunguni Uchebe, wadai hakuwa na sifa za kuwa kocha mkuu wala msaidizi

Singida BS wamsagia kunguni Uchebe, wadai hakuwa na sifa za kuwa kocha mkuu wala msaidizi

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Kufuatia taarifa zilizosambaa kwenye vyombo vya habari kuwa Singida Black Stars ilimfuta kazi Kocha Patrick Aussems kwa sababu ya mechi dhidi ya Yanga ya tarehe 30/10/2024 visiwani Zanzibar, klabu hiyo imeeleza sababu za kuondoshwa ni kwasababu hakuwa na sifa ya kuwa kocha mkuu wala kocha msaidizi kwa ligi kuu ya NBC kwa mujibu wa kanuni za TFF.

Taarifa ya leo Februari 19, 2025 iliyotolewa na uongozi wa Singida Black Stars imetolea ufafanuzi kauli tata zilizotelewa na kocha huyo aliyeondoka klabuni hapo mwishoni mwa mwaka 2024 aliyedai kuwa uongozi wa Singida umekua na tabia ya kuingilia majukumu kitendo kilichomchukiza na kuamua kuondoka klabuni hapo ambapo imeeleza kuwa jambo hilo sio la kweli na kubainisha kuwa vyombo vya habari vinatoa taarifa ya upande mmoja pasipo kusikiliza upande wa pili.

Sababu nyingine ya Mbelgiji huyo kuondoka ni matokeo mabaya ya michezo mitatu huku akijitetea kuwa wachezaji wamechoka kwa kuwa hana wachezaji wa kuwabadilisha sababu iliyowachukiza viongozi huku kocha huyo akidaiwa kukataa kuwatumia Kelvin Nashon, Najim Mussa na Benjamin Tanimu bila sababu za msingi.

Vilevile klabu hiyo imeeleza kuwa kocha huyo wa zamani wa Simba Sc alisema timu inafanya vibaya kwa kuwa Mji wa Singida ni mbaya na hauna entertainment akitaja hakuna kumbi za starehe za usiku, Bahari, vinywaji, shopping malls na viburudisho vingine akishawishi uongozi uihamishie timu kwenye majiji makubwa kama unataka kufanikiwa.

Uongozi ulitafakari na kuona hauwezi kuihamisha timu wala hauwezi kuihamishia Bahari Singida, basi umwondoe yeye akatafute bahari na viburudisho anavyovitaka.

Aidha kocha huyo amedaiwa kukataa makazi aliyopewa na klabu na kutaka kuishi kwenye Hoteli ya kifahari tu. Tangu awasili Singida Aussems alikuwa anaishi Regency Hotel pekee kwa muda wote mpaka anaondoka. Regency Hotel ni miongoni mwa hoteli zenye hadhi ya juu Singida jambo ambalo sio endelevu.
1739979823279.png

1739979868670.png

1739979983801.png
 
Vipi na yule kocha wa Afrika Kusini aliyeondoka baada ya kudai waziri alikuwa anamuingilia majukumu yake.
 
Back
Top Bottom