Pre GE2025 Singida: CV za Wabunge mwaka 2020 - 2025. Mbunge wako ametimiza ahadi zake?

Pre GE2025 Singida: CV za Wabunge mwaka 2020 - 2025. Mbunge wako ametimiza ahadi zake?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Wakuu,

1. Isack Francis Mtinga - MBUNGE WA IRAMBA MASHARIKI

Tarehe ya Uchaguzi (2020): Alipata kura 35,457

Elimu

Shahada ya Sayansi ya Chakula na Teknolojia, Chuo Kikuu cha Sokoine (1999-2003)

Mchango katika Siasa

Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Singida
Mjumbe wa Baraza Kuu la UVCCM
Kamishna wa Wilaya kwa maeneo mbalimbali

Chama: Chama Cha Mapinduzi (CCM)


2. Yahaya Omary Massare - MBUNGE WA MANYONI MAGHARIBI

Tarehe ya Uchaguzi (2020):
Alipata kura 16,961

Elimu

Shule ya Msingi ya Mondo (CPEE, 1973)
Shule ya Sekondari ya Kati (1977)
Chuo cha Mpwapwa - MATI ngazi ya Cheti (1978)

Kazi alizozifanya

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM Manyoni (2012)
Afisa Mifugo Msaidizi (1978-1984)

Chama: Chama Cha Mapinduzi (CCM)


3. Chaya Pius Stephen - MBUNGE WA MANYONI MASHARIKI

Tarehe ya Uchaguzi (2020): Alipata kura 43,847

Elimu

Shule ya Msingi ya Iseke (1986-1992)
Shule ya Sekondari ya Mwanzi (1993-1996)
Shahada ya Environmental Science, Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (2001-2004)
MSc. in Public Policy and Management, Carnegie Mellon University (2007)
Masters of Public Health, Muhimbili University of Health and Allied Sciences (2017)
Ph.D. in Public Policy, Chuo Kikuu cha Dodoma (2009-2013)

Kazi alizozifanya

Afisa wa Udhamini wa Watoto, World Vision Tanzania (1999-2001)
Mratibu wa Mradi, World Vision
Mhadhiri Msaidizi, Chuo Kikuu cha Dodoma
Mkurugenzi wa Shirika la Amref Health Africa Tanzania (2014-2017)
Mtaalamu wa Sera za Jamii, UNICEF Tanzania (2017-2020)

Maswali Bungeni

Maswali 17 ya msingi
46 ya ziada
michango 32

Chama: Chama Cha Mapinduzi (CCM)


4. Abeid Ighondo Ramadhani - MBUNGE WA SINGIDA KASKAZINI

Tarehe ya Uchaguzi (2020): Alipata kura 36,284

Elimu

Shule ya Msingi ya Mrama (1988-1994)
Shule ya Sekondari ya Mwenge (1994-2000)
Al-farauq Islamic Seminary (2000-2002)
Shahada ya Kwanza, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (2003-2006)
Shahada ya Uzamili, Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (2016-2023)

Kazi alizozifanya

Afisa katika Ofisi ya Rais, Usimamizi wa Umma na Utawala Bora (2008-2020)
Mkurugenzi Mtendaji, Shirika la Waendee (2016-2020)

Chama: Chama Cha Mapinduzi (CCM)


5. Elibariki Emmanuel Kingu - MBUNGE WA SINGIDA MAGHARIBI

Tarehe ya Uchaguzi (2020): Alipata kura 32,720

Elimu

Shule ya Msingi Musimi (1988-1994)
Shule ya Sekondari Mkwese (1995-1998)
Shahada ya Kwanza, Chuo Kikuu cha Mzumbe (2002-2005)

Kazi alizozifanya

Afisa Rasilimali Watu, COSTECH (2006-2008)
Mkuu wa Wilaya, Kisarawe (2012-2015)
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida

Chama: Chama Cha Mapinduzi (CCM)


6. Miraji Jumanne Mtaturu - MBUNGE WA SINGIDA MASHARIKI

Tarehe ya Uchaguzi (2020): Alipata kura 32,720

Elimu

Shule ya Msingi Moshono (1981-1987)
Chuo cha Ufundi Arusha (1988-1990)
VETA Dodoma, Cheti cha Umeme (2000-2001)
Cheti cha Kompyuta, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dodoma (2009)


Kazi alizozifanya

Mwenyekiti wa Kikoa cha Wazazi Dodoma Urban (2008-2012)
Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Makete na Mufindi (2012-2015)
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi (2016-2019)

Chama: Chama Cha Mapinduzi (CCM)


7. Mussa Ramadhani Sima - MBUNGE WA SINGIDA MJINI

Tarehe ya Uchaguzi (2020):
Alipata kura 23,220

Elimu

Shule ya Msingi Mughanga (1985-1991)
Diploma ya Ualimu, Butimba Teachers College (2007-2009)
Shahada ya Uzamili, Open University of Tanzania (2017-2020)

Kazi alizozifanya

Katibu wa Habari, CCM Mkoa wa Singida (2012-2017)
Mwalimu (2002-2015)
Mjasiriamali (1996-2001)

Chama: Chama Cha Mapinduzi (CCM)
 
Ushindi wa namba 5 na 6 idadi kura za ushindi zinatia shaka sana.
 
Kuna CV ya mbuge flani, iko sawa kabisa na mchango hafifu kwenye jamii yetu.
 
Back
Top Bottom