Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Jumapili MKOA wa Singida unatarajia kuyatumia maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yanayofanyika kila mwaka Machi 8, kwa kugawa mitungi ya gesi 29,000 yenye bei ya ruzuku kwa wanawake ikiwa ni hatua kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia mkoani hapa.
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego, akizungumza na waandishi wa habari leo amesema maandalizi ya Siku ya Wanawake Dunia katika mkoa huu yamekamilika ambapo miongoni mwa mambo yatakayofanyika ni kuhakikisha inafanyika promosheni ya kutosha ya kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia.
Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
"Rais Dk.Samia Suluhu Hassan yeye ndiye kinara wa nishati safi duniani kwa hiyo katika taifa lake ameweka mipango mbalimbali ya kuhakikisha kwamba tunawafikia watu wengi kwa nishati safi ya kupikia na serikali inakuwa ndio namba moja na wadau wengine wanafuata," amesema Dendego.