Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
Mbunge wa Viti Maalum kutoka Singida, Jesca Kishoa, leo Novemba 27, 2024, ametimiza haki yake ya kidemokrasia kwa kupiga kura katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Kijiji cha Maziliga, Nduguti, wilayani Mkalama, Singida, alikozaliwa.
Baada ya kupiga kura, Kishoa amesema, "Leo nimetumia haki yangu ya msingi kama raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kumchagua kiongozi nimtakaye kwa maendeleo ya mtaa wangu. Nikiwa hapa Wilayani Mkalama, naendelea kuhamasisha Watanzania wote kutumia fursa hii muhimu kupiga kura."
Alitoa wito kwa wananchi kuungana katika kuchagua viongozi bora wa Serikali za Mitaa, akisisitiza kuwa uchaguzi huu ni nafasi muhimu ya kujenga maendeleo ya jamii.