Singida: Miili ya watu watano waliozama bwawani yapatikana

Singida: Miili ya watu watano waliozama bwawani yapatikana

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
1625589809532.png
Miili ya watu watano waliokufa maji katika bwawa la Ntambulo mkoani Singida imepatikana huku vifaa duni vikitajwa kuchelewesha kazi ya kutafuta miili hiyo.

Kati ya miili iliyopatikana ni wa mwanafunzi wa shule ya msingi na juhudi zaidi zinafanyika kumtafuta Mohamed Ayub.

Ajali hiyo ilitokea jana Jumatatu Julai 5, 2021 baada ya mtumbwi waliokuwa wamepanda watu saba kupinduka katika bwawa hilo na watu wawili kuokolewa wakiwa hai akiwemo dereva wa mtumbwi huo.

Leo Jumanne Julai 6, 2021 Vikosi vya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji vilipata miili hiyo kwa kutumia mitumbwi na nyavu za kuvua samaki.

Awali, Kamanda wa kikosi hicho mkoani Singida, Ivo Ombella aliwahakikishia wananchi kuwa miili yote itapatikana kwani vijana wake wamejipanga vizuri kwa kazi hiyo.

"Vijana hawa wana weledi mkubwa na kazi hii na wanaendelea vizuri, na hatutaondoka eneo la tukio mpaka miili yote ipatikane," amesema Ombella.

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk Binilith Mahenge amekitaka kikosi hicho kutumia utaalamu wao wote kuhakikisha wanarudisha faraja kwa waliopoteza ndugu zao.

"Umati huu una hamu kubwa ya kuwaona wapendwa wao waliopotea kwenye maji wakiwa kwenye mtumbwi unaozaniwa kupigwa na wimbi, mwanzo walikuwa saba lakini wawili walifanikiwa kuokolewa wakiwa hai, mmoja ametolewa leo akiwa amepoteza maisha hivyo bado wengine wanne," alisema Mahenge.

Mwananchi
 
Mungu awalaze salama [emoji120]
 
Back
Top Bottom