Pre GE2025 Singida: Mitungi zaidi ya 29,000 yatolewa kwa bei nafuu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Katika kilele cha siku ya Wanawake Duniani Mkoa wa Singida, imeunga mkono jitihada za Mheshimiwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan za kupambana na matumizi ya nishati chafu na kuhamia kwenye nishati safi, kwa kutowa mitungi zaidi ya 29,000 kwa wanawake wa Mkoa wa Singida kwa bei nafuu ambayo ita zinufaisha kaya 350,000 za mkoa huo.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Bi. Halima Dendego, amesema hayo kwenye kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wanawake kimkoa, ikiwa ni sehemu ya kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani na kudai kuwa mitungi hiyo itawasaidia wanawake hasa wa vijiji kuboresha afya zao ambazo zilikuwa zikiathirika na moshi wa kuni.

Nashauri hao wanufaika waambiwe ukweli!
Mitungi ni mabomu!
 
Mitungi 29,000 itanufaishaje kaya 350,000!!???
Kaya ni nini kwani!!??
 
Katika kilele cha siku ya Wanawake Duniani Mkoa wa Singida, imeunga mkono jitihada za Mheshimiwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan za kupambana na matumizi ya nishati chafu na kuhamia kwenye nishati safi, kwa kutowa mitungi zaidi ya 29,000 kwa wanawake wa Mkoa wa Singida kwa bei nafuu ambayo ita zinufaisha kaya 350,000 za mkoa huo.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Bi. Halima Dendego, amesema hayo kwenye kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wanawake kimkoa, ikiwa ni sehemu ya kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani na kudai kuwa mitungi hiyo itawasaidia wanawake hasa wa vijiji kuboresha afya zao ambazo zilikuwa zikiathirika na moshi wa kuni.

Bei ya kujaza gesi ishuke maana ilikogawiwa, ikiisha Yale machuma (mitungi ) hugeuka kuwa vigoda vya kukalia tu. Serikali isikie kilio hiki !
 
Ni kwamba sera za sasa ifikapo uchaguzi ccm inatumia rushwa kuomba wachaguliwe kwa mtindo huu.

Juzi tumesikia mbunge msukuma ana kwambia kanunua gari la wagonjwa kwa pesa yake.Hata kama ni kweli au uwongo.

Wengine nao wanatoa pesa kwenye vikundi,misaada ambayo ilitakiwa tokea kupata ubunge wao walitakiwa kuendeleza wanacho kifanya ila wanafanya ikifika uchaguzi.
 
Back
Top Bottom