The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
TAKUKURU YABAINI UPIGAJI WA FEDHA SINGIDA
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU mkoa wa Singida imefanikiwa kuokoa zaidi ya shilingi milioni 75.3, baada ya kufuatiliaji utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika sekta za elimu.
Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari juu ya utendaji kazi wa TAKUKURU, Mkuu wa taasisi hiyo Mkoa wa Singida Sipha Mwanjala amesema kuwa wameokoa fedha hizo baada ya kufuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika kipindi cha kuanzia Oktoba hadi Disemba mwaka jana na kubaini kuwa baadhi ya wazabuni wamelipwa kabla ya kufanyakazi na ukwepaji wa kodi.
Hata hivyo pamoja na pongezi kwa kuokoa fedha hizo, maoni ya baadhi ya wakazi wa mji wa Singida ni TAKUKURU kuchukua hatua zaidi dhidi ya wahusika ili kukomesha vitendo kama hivyo.
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU ndicho chombo chenye jukumu la kusimamia vita dhidi ya rushwa, kwa kuchunguza na kuchukua hatua kulingana na sheria namba 11 ya mwaka 2007.