Kumekuwa na taarifa za mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu kwenye baadhi ya mikoa nchini. Mkoani Singida jambo hili sijalisikia lakini ni vyema mamlaka wakachukua hatua ya kuhamasisha usafi wa mazingira na haswa kwny migahahawa ya chakula na wauzaji wa vyakula mtaani.
Ukipita maeneo ya sokoni iwe soko kuu, Msufini, au hata stendi ya zamani Ginery ni kawaida kukuta wauza samaki wakiwa wanauza samaki bila kufunikwa. Lkn pia wao wauzaji wanashikashika hao samaki bila kuvaa japo mifuko laini kuepusha kuwagusa na mikono moja kwa moja.
Nafikiri Singida akipatikana mgonjwa mmoja tutashika rekodi ya kuwa na wagonjwa wengi wa kipindupindu kuliko sehemu nyingine nchini.
Mkuu wa wilaya Gondwe fanyia kazi jambo hili.