KERO Singida: Zahanati ya Kijiji cha Mjughuda inatoza pesa huduma huduma zinazopaswa kutolewa bure

KERO Singida: Zahanati ya Kijiji cha Mjughuda inatoza pesa huduma huduma zinazopaswa kutolewa bure

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Yusuphnyonyi

New Member
Joined
Feb 17, 2025
Posts
1
Reaction score
0
Hii hali ipo kwenye Eneo la Zahanati ya Kijiji Cha Mjughuda, kata ya Ikhanoda wilaya Singida vijijini mkoani Singida. Ambapo wahudumu wa Zahanati hiyo wanatoza hela na kuwalipisha wananchi hela ili wapate huduma ambazo kimsingi zinatolewaga bure.

Huduma hizo ni kama vile
1-Kadi za kliniki kwa watoto wadogo na wajawazito.
2- Huduma za uzazi wa mpango.
3- Matibabu Kwa watoto chini ya miaka 5.
4- Huduma haipatikani kuanzia saa 11 jioni hadi saa 2 asubuhi nje ya huo muda hupati huduma kabisa

Hii ni kero sana wazazi wanajifungua nje ya kituo bila huduma ya wahudumu au daktari.
 
Back
Top Bottom