HOP HOPPER
Member
- May 12, 2018
- 65
- 109
Habari zenu wote ndugu jamaa ma rafiki
Uzi huu ni maalum Kwa ajili ya kuwapongeza single mamas wote guniani kote. Ukweli kutoka moyoni hongera zenu ziwafikie Popote mlipo kwenye hili gunia lililokuwa zamani dunia.
Sio jambo jepesi kupata kazi mnayotakiwa kufanya watu wawili Kwa muda wa maisha yenu yote maana mtoto hakui kwa mzazi.Kisha kiongizi na mwelekezaji anakuachia anahepa!
Ni kama Fundi ujenzi na saisdia fundi wake. Saidia Fundi kama angejua fundi wake atamkimbia na kumwachia Kazi kubwa ambayo màsikini wa Mungu yeye mwenyewe haijui vzuri asingemwitia hiyo kazi. Lakin afanyeje sasa ikiwa jembe lake limemsaliti. Limechukua advance Juu kwa Juu limetokomea kusikojulikana. Na yeye ndio ameipatana ile kazi.
Ulikosea na kurebiaha makosa yako bila kujua kama unaingia mkenge mwingine hata na Mara nyingine ikawa hivyo,na mara nyingine tena! Pole
Unaweza kuwa na makosa yako lakini yasilingane na adhabu kubwa unayopewa. Mafundi wengi sio waaminifu na Sana waoga wa kazi ngumu.
Usifikirie kwamba ni Bahati mbaya,kila jambo na kusudi lake,inawezekana hao wote Mungu alikuepusha mabalaa ya kutosha.
Tulia wachonge Vizuri Watoto wako.Heshima na adabu ndio msingi wa uwezo wa kuitawala dunia yao.Ukifanya hivyo watakufurahisha na kukufariji.
Naongea kuhusu wale ambao hawakuwahi kuchoropoa Bali walipopata zawadi chungu walitulia nayo wakapiga moyo konde, wakajipanga kukabiliana na matokeo
Hawakuwahi kufikiria kuua wala uuaji haukuwahi kuwa fungu lao.Hawana deni na muumba wao Kwa kosa la mauaji bali wana ujasiri wa kumtaka radhi Kwa mahitaji yao na Watoto wao.
Nakupongeza Kwa kutokukata tamaa ukajaribu na kujaribu tena.Hayo yote ni mafanikio hata kama hakikutokea ulichokitarajia naweza kusema hakuna ullikokosea na ndio maana bado unaendelea kuviatamia Vifaranga vyako.Mungu anakuona asiyedharau nafsi za wanyonge na walioonewa.Wewe kazana tu kuvifinyanga vyungu vyako,utafika wakati vitakufurahisha.
Usiwaze kuua Kwa kuwa kama ndio hivyo basi hata wewe ulistahili kuuawa lakini mama yako alikuacha uishi. Ushukuru na kumwadhimisha kwa fikra zake hizo za ushindi maana alikupenda na kukuonyesha thamani ya maisha.Usiue ukamhuzunisha na kumtweza.Tutakuita muuaji Tena wa kiumbe kisichoweza kijitetea bali kinachohitaji Upendo na kutunzwa na kuufurahia uumbaji wa Mungu.
Nakupongeza zaidi Kwa sababu unajua kupenda.Matatizo waliyonayo wapendwa wako haikuwahi kuathiri Upendo wako Kwa huyo mtoto au Watoto wako,zaidi Upendo wako umekuwa ukiongezeka zaidi hasa unapokunbuka kumbukumbu mbaya za Yale uliyotendewa na huyo uliyejitoa kwake.Unaona ni kama kito cha thamani kilichopatikana Kwa taabu na mikasa mingi.
Ongeza zaidi kupenda maana kupenda na kusamehe ni agizo la Muumba wetu.
Zingatia pia hesabu za kutoa na kujumlisha ili upambanue kwamba ni faida kubwa uliyonayo wewe.Umewekeza uwekezaji wenye faida kubwa kuliko zote lakini kwa upande mwingine ni hasara tu kama ufalme usiokuwa na jeshi. Kuna wakati watahitajika zaidi asiwaone
Nitakupongeza zaidi utakapozingatia kuwatia akili na maadili mema maana gunia halina huruma na wale wasiokuwa na akili.
PAMBANA USIKATE TAMAA.