Deejay eXii
Member
- Feb 22, 2025
- 33
- 37
Sinners ni filamu mpya ya kutisha inayoongozwa na Ryan Coogler, ikimshirikisha Michael B. Jordan katika nafasi kuu. Filamu hii inatarajiwa kutolewa tarehe 18 Aprili 2025.
SHORT STORY
Katika kipindi cha marufuku ya unywaji wa pombe holela nchini Marekani (Prohibition era), ndugu mapacha Smoke na Stack (wote wakiigizwa na Michael B. Jordan) wanarejea katika mjini kwao baada ya muda mrefu.
Wanapofika, wanakutana na mfululizo wa matukio ya kutisha yanayohusisha viumbe vya ajabu vinavyowahangaisha wakazi wa mji huo.
Wakiwa na dhamira ya kulinda jamii yao, ndugu hawa wanaamua kukabiliana na hofu zao na kuamua kuuvaa ujasiribwakipambana na nguvu za giza zinazotishia kuangamiza kila kitu wanachokipenda.
MAIN CHARACTERS
Michael B. Jordan kama Smoke na Stack – Ndugu mapacha wanaorejea nyumbani na kukutana na matukio ya kutisha.
Hailee Steinfeld kama Mary – Mwanamke mwenye siri nyingi, anayehusishwa na matukio ya ajabu katika mji huo.
Delroy Lindo – Mzee wa mji anayejua historia ya viumbe vinavyosumbua jamii.
Wunmi Mosaku – Mtafiti wa mambo ya kisayansi.
Jack O'Connell – Rafiki wa zamani wa ndugu hao.
Filamu hii inaashiria ushirikiano mara tano kati ya Michael B. Jordan na Ryan Coogler, baada ya kazi zao zilizopita kama Fruitvale Station, Creed, na Black Panther.
Kwa wale wanaopenda filamu za kutisha zilizojaa hadithi za kusisimua na uigizaji bora, Sinners ni filamu inayosubiriwa kwa hamu kubwa.
Wazee wa kazi mpooo......dubwana hilo March 7 tu 👊
#enjoy
#bestmovie
#LikeAndShare
#TuFollow