Sintah alikwama sana kwa Juma Nature

Interest

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2015
Posts
3,434
Reaction score
7,072
Miaka ya 2000 huko ilizuka ghafla couple ya nguvu iliyobustiwa na magazeti ya udaku. Nature na Sintah..

Okei. Mapenzi huota kokote lakini hii combo mpaka leo siisomi ilikaaje kaaje.

Sintah alikuwa mtoto wa mjini. Mdangaji kwa lugha ya kisasa ambaye alibahatika kupata exposure mapema ya ujanja ujanja wa hapa na pale. Ilifikia hatua akawa anaitwa Jennifer Lopez 'JLo' wa Bongo. Very classic!

Nature yeye alikuwa supastaa kutoka uswahilini huko Temeke. Jina kubwa kuliko uwezo. Uwezo wa kutengeneza maisha na kuishi kinyota. Kibongobongo alipeta lakini hakuwa mjanja. Well, alikuwa mjanja wa kishamba.

Ni kudanga? Labda. Zile story za kwenye Inaniuma sana na Sitaki demu zinaweza kuchora picha halisi ya jamaa alivyokuwa anatumika bila kujua maana drama za mahusiano yao zilikuwa dili kwa magazeti. Enzi hizo Sintah ndio queen wa maskendo hakauiki magazetini kabla hajaja kurithiwa na Wema Sepetu.

Swali la mshangao: Kama Sintah alikuwa akicheza league za vigogo wakiwemo akina Cool J, Dkt. Machache na the co., Meddy MP na ma-don wengine wa enzi hizo, kwa Kiroboto alikwama wapi?

Ustaa? Alikuwa nao.
Pesa? Ipi.
Mapenzi? Asingemfanyia masinema.

Pisi ilikwama sana. Muda umeongea.
 
Huyu mdada yupo bado kwani?
Pepo za vuli na kusi zilijichanganya wakati ule
Alikuwa hodari wa kuchambua maisha ya watu
Wakati wa kuchambua ujue kuna siku nawe utachambuliwa
Alifikiri yeye ni rafiki wa Zari, Zari alipokuwa Madale alimtafuta mtu wa class yake Madame Rita, Sintah tulibaki kucheza nae mduara tu kwenye 40 za watoto.
 
Juma Kassim Kiroboto ( Juma Nature) Mtoto wa Kurasini Kijiji Cha Wavuvi alikuwa Na Usela Mwingi Sana Na ndio maana waliotajirika kwa Jina Lake Ni wengi Sana

Yule Binti alikuwa anapenda kudanga Na Watu Maarufu Na ndio sababu miongoni mwa Fimbo alizokula zilikuwa Za Kijana huyo Mla ndumu

Enzi hizo Bongo record ya PFunky ilikuwa Kama Sebule ya TMK
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…