Sintah alikwama sana kwa Juma Nature

Aiseee...!!!
 
Ila ITV imehusika sana kuwapa promo hawa warembo wakati ule..nakumbuka kaole Sanaa group imehusika sana kuwa brand wengi wao..watunzi na waongaji kama Chrissant Mhenga walihusika sana.
 

Huyo dogo aliekua anatangaza ITV anakwenda kwa jina la BICCO,

Dogo alikuja akatongoza kiukweli ila akatolewa za mbavuni, akanywa sumu.

Bicco ilibaki kidogo afe kisa penzi la NORA, ila leo nadhani hata akipewa bure hawezi kukubali.


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Kwenye inaniuma sana anadai ilimuuma sana alivyoona Sinta akipigwa denda kwenye dirisha la gari mpaka gari ikagoma kwendaaaaaaaa.

Hii ya kupigwa denda mpaka gari kugoma kwenda kuna msanii mmoja anahusika sasa ni marehemu.
Alikufa kwa ajali ya gari mitaa ya kati ya Morocco na Mwenge( hapo kati).

Huyo Sinta aliwahi kuwa video vixen kwenye wimbo wa huyo msanii, jina la wimbo lilikua linaitwa MPENZI,

Hii video ndio ilileta mapinduzi katika video zilizohusisha na video vixen kucheza nusu utupu bongo, narudia tena hii ndio video ya kwanza bongo ambayo ingebidi ifungiwe na basata kama ingekua ni leo, maana kwa kipindi kile ilikua ni video iliyokua na matendo ya wazi sana.

Wasanii na madirector wa bongo ndio wakaanza kufanya zao baada ya hiyo.

Huyo msanii(marehemu) alikua mwenyeji wa mikoa ya kanda ya ziwa ambae alikua anaishi nje ya nchi( SWEDEN [emoji1236] Kama sijakosea).

Ndio moja ya wasanii wa kwanza kwanza kutoboa akiwa sambamba na kina SUGU.


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Ha ha haaaa enzi za Sinta na Nature aisee kitambo sana hiyo ni miaka ya 2001 . TV zilikuwa ni zile za visogo afu Ukiwa na ungo (satellite dish) kubwa la kutengenezwa mtaani na lina wavu flani nakuambia mnaoneka nyie ni matajiri Sana. Alafu computer zilikuwa desktop za visogo Pentium 2[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…