ungonella wa ukweli
JF-Expert Member
- Mar 27, 2012
- 4,210
- 556
Habarini wana jf! Taarifa za uhakika zilizopatikana toka maeneo mengi nchini hasa vijijini wananchi wengi hawajaelimisha au kujulishwa kwa uwazi juu ya nafasi zinazoombwa katika makundi mbalimbali kama ya mtu mzima,kijana.mwanamke na hata mtu mwingine. Wananchi wengi wameomba nafasi hizo kiujumla na kusababisha baadhi ya makundi kutowepo. Mfano baadhi ya maeneo vijana ni wachache kwenye orodha ya waombaji kuliko wazee, maeneo mengine wameomba watu wa aina moja tu kama watu wazima tu. Udhaifu huo umechochewa na watendaji wengi wa vijiji na mitaa kutojua namna ya kuwapata wajumbe hao. Pia baadhi ya maeneo madiwani wakishirikiana na watendaji wa kata wameteua watu wao kwa siri, na kutowatangazia umma juu ya namna ya kuomba nafasi hizo. Baadhi ya wananchi waliohojiwa maeneo mengi nchini hasa vijijini wanasema kulikuwa na ugumu katika kuomba nafasi hizo, hasa watendaji wakiulizwa walikuwa wakijibu hawana taarifa ya mambo hayo. Taarifa zilitolewa siku moja kabla ya tarehe ya mwisho ya kuomba ujumbe wa baraza la katiba yaani tarehe 20 march 2015. MYTAKE: TUME YA KATIBA ilipaswa kutoa semina kwa viongozi wa kata madiwani na watendaji wa vijiji na kata kabla ya kutoa tangazo kwa wananchi la kuomba nafasi hizo. Vinginevyo hatutapata wajumbe sahihi waliochaguliwa na wananchi!