Green Thoughts
Member
- Aug 25, 2022
- 42
- 71
Katika ulimwengu wenye takribani ya watu zaidi ya bilioni 7, watu wenye umri chini ya miaka thelathini (30) wanadhaniwa kuwa ni zaidi ya 50% duniani kote. Na katika hali ya kawaida kundi hili limejumuikwa na vijana pamoja na watoto wadogo.
Takwimu kutoka Benki ya dunia (WB), Shirika la Ajira Ulimwenguni (ILO) zinaonyesha kuwa katika kundi hilo la watu wenye umri chini ya miaka 30, zaidi ya 34% wapo shule za awali na za msingi, 20% wapo shule za sekondari, vyuo vikuu pamoja na shule za ufundi. Huku ikidhaniwa ya kuwa takribani 17% na zaidi wapo katika ajira rasmi na zisizo rasmi.
Takribani 30% za watu wenye umri chini ya miaka 30 zilizobaki zimejumuishwa kwenye makundi kama vile wanajeshi, wafungwa, vijana wa mtaani pamoja na watu wanaofanya kazi katika mazingira hatarishi.
Takwimu hizo zinazoonesha jinsi gani kundi hili tulivyogawanyika kwenye mafungu tofauti tofauti ulimwenguni kote. Ningependa kuizungumzia zaidi nchi yetu pendwa ya Tanzania, ambapo hivi sasa kila mwaka katika ngazi ya vyuo vinavyotambulika kuwa ndio ngazi muhimu ya kumuimarisha kijana yoyote kabla hajaingia kwenye swala zima la utafutaji kupitia taaluma yake vinatoa maelfu ya wahitimu ambao hujipigia hesabu za kuingia kwenye soko la ajira kwa kuajiriwa au kujiajiri.
Takwimu za mwaka 2020 kutoka Ofisi ya Takwimu za Taifa na ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na watu wenye Ulemavu zinaonesha kuwa zaidi ya watu 314,057 wameajiriwa kupitia miradi ya maendeleo ya serikali kama vile ujenzi, mikopo ya halmashauri pamoja na ajira rasmi ya moja kwa moja. Inasadikika idadi hiyo imeongezeka kidogo hadi kufikia mwaka huu 2022 serikali imetengeneza ajira 500,000 kupitia miradi yake pamoja na waajiriwa rasmi. Watu 280,941 kama ilivyoainishwa kwenye mchoro ufuatao umetoka kwenye sekta binafsi.
Chanzo: Ofisi ya Takwimu za Taifa (NBS)
Katika nchi yenye watu zaidi ya milioni 60, huku 50% na zaidi ikiwa ni vijana, inaonesha jinsi gani asilimia kubwa ya kundi hili lipo mtaani katika kufanya harakati tofauti tofauti ili kuweka mkono kinywani.
Ningependa kuchukua nafasi hii kupitia waraka huu, mimi kama kijana wa Kitanzania kuwasihi vijana wenzangu wa Kitanzania ya kuwa, tatizo hili si geni sana nchini na ulimwenguni kote. Kijana mwenye nia ya kutaka kupiga hatua, anaweza akakosa ajira lakini hawezi kukosa kazi ya kufanya. Ningependa kutolea mfano, wa nchi ya wenzetu China, si kwasababu ni nchi iliyoendelea; La Hasha, natoa mfano huu kwasababu ni nchi moja wapo yenye watu wengi zaidi ulimwenguni (Bilioni 1.4+). Wachina zaidi ya milioni 600 wana umri chini ya miaka 30; watu milioni 200 tu ndio walioajiriwa kwenye makampuni binafsi pamoja na serikali kuu. Hebu tujiulize, je hao milioni 400 wapo wapi na wanafanya nini?
Sijasema kuwa hawalalamiki kwasababu ya kukosa ajira, wanaweza wakawa wanalalamika lakini ni watu wenye kujishughulisha kila kukicha. China ni miongoni mwa nchi zinazoaminika kuwa na bidhaa zenye viwango vya juu mno, lakini hawakuishia hapo, kupitia changamoto hizi hizi za ajira, vijana wao wamebuni namna ya kukidhi masoko tofauti tofauti ulimwenguni kulingana na uhitaji pamoja na uwezo wa wateja wa bidhaa hizo. Mfano watu hawa wanaweza kutengeneza simu za Milioni 3 na zaidi kwa ajili ya soko la wenye nazo, pia wanaweza kutengeneza simu ya elfu 15 hadi 20 kwa ajili ya watu wa kada ya chini.
Watu hawa hawakuishia kufundishwa vitu darasani tu kwa ajili ya kuhitimu na kupata vyeti, bali watu hawa walijikita kwenye kupata maarifa na taarifa sahihi ili kujikwamua, kwasababu changamoto yao ya ajira haijaanza leo wala jana.
Sisi tumekuwa wepesi kutumia mitandao hii kuangalia vitu tofauti ambapo si vibaya hasa kwenye upande wa burudani kama vile michezo, muziki, tamthilia n.k. Wapo Watanzania wanaotumia mitandao hii hii vizuri zaidi, katika kujifunza taaluma mbalimbali, na kuchangamkia fursa zenye malipo ndani yake. Watu hawa tunapowaona kwenye mitandao ya kijamii wakifanya mambo makubwa, tunaanza kuishia kuwakejeli, kuwatukana na kusema kuwa wanaunganishiwa na wakubwa, na maneno mengine mengi.
Sitaki kusema kuwa hayo mambo hayapo, lakini nataka kumaanisha ya kwamba, tusipende kuwa watu wa lawama bali tutafute namna ya kupata maarifa na taarifa sahihi. Mitandao imejaa fursa kedekede, ni namna tu ya kujua zinapopatikana na namna ya kuziendea.
Wenzetu wamejitengenezea njia nzuri ya kujitafutia vipato hata kwa ujira mdogo lakini wamekuwa si watu wa kulalamika tena, bali wamekuwa watu wa kugeuza changamoto kuwa fursa siku zote. Leo hii, ukiwauliza hata vijana wa Kitanzania 100 kama wanaifahamu sera ya maendeleo ya vijana ya mwaka 2007 inazungumzia nini, nina uhakika zaidi ya 75% watakuwa hawana majibu sahihi. Hata kufahamu ya kwamba sera hiyo imeshapitwa na wakati na yapaswa kuboreshwa au kubadilishwa, sababu imeshakaa zaidi ya miaka 10, wengi wao hawawezi kufahamu.
Changamoto ya kufanya jambo lolote bila maarifa ya kutosha na taarifa sahihi kumewaingiza vijana wengi matatizoni. Unaweza kutaka kufanya jambo jema kama mwenzako aliyekutangulia na kufanikiwa kupitia jambo hilo, lakini ukaona mambo hayakuendei kama ulivyotarajia, ni kwasababu ya kutowekeza muda wa kutosha kwenye maarifa na taarifa sahihi.
Mtu yeyote mwenye maarifa, hutafuta taarifa sahihi kabla ya kufanya jambo lolote la msingi, hivi ndivyo wawekezaji, wajasiriamali wakubwa au mtu yeyote makini hufanya. Nawasihi vijana wenzangu, tujikite kwenye kutafuta maarifa na taarifa sahihi kwanza, hii itatufanya tupunguze lawama kila kukicha, pia tutakuwa watu wa kuzichangamkia fursa mbalimbali zinazoweza kutukwamua kimaisha.
Nakabidhi,
Andrew Ikingura.

Attachments
Upvote
23