Ahahahaha! Pole sana ndugu yang lakin haya matusi na kejeli zote hizi umezitaka wewe mwenyewe
Nasema hivii wew ulistahili kutukanwa tena zaidi ya hapa. Shubamiti wew, Kichwa kama sambusa
Unaleta stori hapa aya mbili tu unasema itaendelea, afu unakuja kuleta comments za kubishana na wasomaji wako badala ya kuendeleza stori yako. Kama co Ungese ni nini huo? Wew ulistahili kutukana afu una bahati hujatukanwa sana
Go to hell
Duh mpaka mwili unasisimkaInaendelea...................... 49k viewers si mchezo.
Haya sasa tusonge mbele tarehe, saa, sekunde za malaika mtoa roho zikawadia 6/04/1994. Saa tisa usiku tukaashuhudia kitu kama kimondo kikishuka ardhini ila kikapotelea vichakani kwa mbali nje ya mji. kutokana na kishindo chake pale ubalozini kila mtu aliamka lakini hakuna aliejua hasa ni nini, tukachukulia kawaida tukajua ni yale yale kila siku si tumeshaanza kuzoea watu wakaendelea kuchapa usingizi nawanaume wakaendelea kulinda getini.
Asubuhi mapema tukashudia hali ya ajabu ambayo sijawahi kuiona katika maisha yangu, yani kukatokea kitu kama wingu hivi yanii mtu akisimama mitaa tano au kumi kutoka ulipo huwezi mtambua vizuri hadi awe karibu sanaa. Wenye redio wakafungulia redio zao kusikiliza , ikumbukwe kuwa kipindi chote wapiga mayowe wa propaganda redioni walikuwa hawaongee ulikuwa unapigwa tu muziki wa chama ila alfajiri ikasikika wimbo wa taifa ndo unapigwa watu wakabaki wanashangaa halafu unakuwa unajirudia .dalili ya kitu kibaya ikaanza kuhisiwa kigali yote kimyaa.....
Tukawa sasa tunaingia tarehe yenyewe 7/04/1994 harufu ya damu ikawa inasikika kigali nzima, makelele ya maumivu ya watu yakawa yanasikika kwa mbali kutoka hapo ubalozini ,balozi ndo akawa ametoka kututangazia kuwa sasa hali si nzuri rais habyarimana ameuawa ile kusema tu vile watu wote akili zilituruka wengine wakawa kama wanataka kukimbia hovyo wanaume ikabidi wafanye kazi ya ziada kwani kitendo cha kutoka nje ya ubalozi kingeleta maafa makubwa sanaa. Ila wote pale picha iliyotujia kichwani ni kwamba sasa tunakufa hakuna tena msalie mtume.
Swali likaja nani kamuua rais? Hakuna mwenye jibu. Aise kuna wimbo moja hivi ukiimbwa unakuwa kama vile unaomboleza unafanafana na ile ya Kimasai ukawekwa kwenye radio ukawa unapigwa huku unamtaja rais kuwa ameuliwa na Ng'otanyi(waasi wa kitusi) aisee vita ikawa imeanza rasmi hata balozi sasa akawa hatoki tena tukakaa wote mle ndani hakuna kutoka kufuata chakula wala nini.
Siku ya kwanza mitaa kelele kila upande, sasa interahamwe wakaanza kuvamia hadi balozi za jirani ambao walikuwa wameondoka walinzi wao wakakimbia watu wakazidi kuuawa. chakula pale kwa ni uji tu hakuna sukari wala nini, unajua kama upo vitani mara nyingi unakuwa husikii hamu ya kula na unajiona uko powa tu kumbe unazidi kuisha ( kama kuna mtu alipigana vita humu ya kagera atadhibitisha hilo) halafu unaweza shanga kumekucha ghafla kiza kimeingia ghafla usiku mnalala usingizi wenye wa mang'amung'amu tu.
Balozi zikawa zinaendelea kuvunjwa siku zinaenda magrounet yanarushwa hovyo hovyo risasi zinalia zikitulia labda nusu saa zinaanza tena,unajua rwanda ni milima sasa unaweza kaa usiku unaona roketi inarushwa kutoka upande moja kwenda upande mwingine vimulimuli tu vya moto hadi kuna kucha kelele na risasi zinaanza tena. Sasa ikawa dhahiri kuwa hakuna namna tumuachie mungu tu.
Lakini wakati huo balozi alikuwa kwenye chumba kimoja kati vile vyumba vya sili nilivyosema hapo awali sijui alikuwa anafanya nini , ikafika ya kumi sasa ikawa hakuna kitu tena njaa tupo katikati ya vita mjini umezungukwa na wanajeshi wanapigana live bila chenga jiona ya siku hiyo ndo wakaja wanajeshi wa rwanda ,na toka siku ile ndo niliwaona live wanajeshi wa rwanda majitu yamepanda sura ngumu macho mekundu wakaja na maroli yale 24 na ile defender nyeupe ila waliokuwa kwenye ile defender hawakushuka tukaitwa uwani ubalozini .balozi akatoa tamko akasema SAFARI YA KUWAONDOA KIGALI WATANZANIA NDO IMEFIKA NA KAMA HUNA PAPER ( PASSPORT ) TAFADHARI USIPANDE KWENYE ROLI UKIPANDA LIKALOKUTOKEA MBELE USILAUMU MTU. hii kauli aliitoa kwa uchungu na kwa msisitizo sanaa huwa siisahau maishani mwangu. .
Hapo sasa ndo ngoma ikawa ngumu kila mtu akamkimbilia balozi kuomba amsaidie mkewe na watoto wake, balozi akagoma kabisa wengine akawa anawajibu kama unampenda mkeo baki nae hapa aisee watu wakawa kama vile wamepagawa maroli yapo nje lakini unashindwa kwenda kulipanda paper huna , sasa kuna kisa kimoja kilichojitokeza sintokuja kukisahau.kuna mama wa kinyarwanda mtusi alikuwa na bwanake mtanzania amezaa nae ila yeye kipindi cha vita alikuwa ameleta mzigo tanzania ,hivyo ikabidi mama ajitoe mhanga akamuita balozi awachukue wale mabinti wake mapacha wawili walikuwa kama na miaka 14 hivi weupe pua za kitusi kabisa balozi akakubali mama akabaki ,sasa tutaona mbele walivyotaka kuleta kizaazaa nusu tuchapwe RPG kwa sababu yao.
Sasa tukawa tumejipakia kwenye roli wengine wasio na vibali wakawa wamebaki pale hapo ubalozini, hapo hakuna kusikitikiana mnapeana mkono wa kwaheri basi safari ikawa imeanza na escot ya wanajeshi wa rwanda ,vizuizi kibao tukifika kwenye vizuizi wanashuka wanaenda wanajeshi wenyewe wanavitoa tunapita ,cha ajabu vizuizi vingine vilikuwa havina hata watu sijui walikuwa wakajificha au vipi.
Sasa wakati vita imepamba moto Tanzania wakawa wamefunga mpaka wake na rwanda Ikatulazimu kupitia boda ya burundi sasa kimbembe ndo kikaanza hapo, kuna wilaya kama tatu inabidi upite ndo ufike boda ya Burundi na rwanda kama sijakosea kwa kutokea kigali lazima upitie province ya butare halafu ya Gitarama ya mwisho nimeisahau kitambo sanaa. Sasa province Butare (wenyewe wanaita) ili ufike lazima uvuke mto fulani mkubwa unaitwa Nyabarongo kuna daraja kubwa hivi linalounganisha kigali na hiyo wilaya hapo sasa ndo niliona mchezo wawale jamaa saba wa defender hapo tunaenda lakini magari yanakanyaga maiti barabarani maiti zimezaga kila kona. Ile tunashuka kilima kidogo inakaribia kuulifikia kama kilomita tatu hivi wale wanajeshi wa rwanda wakageuka na gari lao ghafla wakarudi nyuma moyo ukapiga paaahhh nikahisi kuna kitu si chakawaida unageuzaje gari ghafla unarudi kwanini usituache tuvuke ndo urudi aisee.
Mbele tena kidogo ile defenda ikasimama katika ya barabara hakuna gari kuendelea kupita magali yakawa yamesimama tu ile defenda ikawa inaendelea kusogea mbele sisi tumeambiwa tusimame hapo hapo hadi Difenda itakaporudi kutoruhusu tuendelee tukawa tu pale na madereva kila mtu kwenye Kibini wengine kwenye bodi nyuma kimyaaaaaa...
Kama lisaa hivi tukasikia risasi zinalindima vibaya Sanaaa yani ikawa dhahiri kama mbele yetu kama kilomita moja watu wanapigana lisasi live ila hatuoni tatizo la rwanda mapori na vichaka vingii ila risasi zikawa zinalia kama zipo chumbani nikasema sasa huu ndo mwisho wetu.
Mwisho lisasi zikakoma tumekaa kama nusu saa hivi defenda hairudi na risasi hazisikiki tena Mwisho balozi akaamuru tuendelee na safari bila defenda dahhh ile tunafika darajani maiti kibao zimelala hapo ila hakuna defenda tukawa tunaendelea na safari tu.
Sasa tukawa tunakaribia kuimaliza province ya Butare sasa hapo ndo kulitokea kizaazaa cha wale mabinti aise tulikuta bonge la kizuizi...... Na maenterahamwe mchanganyiko na wanajeshi wa rwanda aise........ Nikasema. Sasa tunakufa.................................
Itaendelea...........................................
Sent using Jamii Forums mobile app
Good analysis ila hapo mwishoni umekunya japo ni haki ya kikatiba kunyaKitu nimejifunza hadi sasa:
1. Kutajwa kwa Dar, Nairobi, Kampala, Kinshasa, Ufaransa, Ubeligiji na Marekani, ni dhahiri vita haikuwa ya watusi na wahutu peke yao. Majabari ya vita hiyo yalikuwa nje ya Rwanda.
2. Vita si ya kujaribu kabisa kwani shetani hufanya kazi mwenyewe badala ya kuwatuma wasaidizi wake.
3. Kwamba malori yalipita juu miili ilozagaa barabarani, ni ishara kuwa mapigano Rwanda yalifikia hatua ambayo pengine ulimwengu haukuelezwa ukweli wa kilichoendelea huko na hivyo kukosa usaidizi stahiki wakati muafaka.
4. Ubalozi wa Tanzania kuwa kimbilio, na kutoshambuliwa kama ilivyokuwa kwa balozi nyinginezo kunatia mashaka iwapo hatukuwa washirika muhimu katika vita hiyo.
5. Media, hasa redio ni chombo hatari mno kikishindwa kufuata misingi bora ya kiutendaji.
Mwisho kuliko vita ije hapa kwetu bora CCM watawale milele.
Sent using Jamii Forums mobile app
Mwaka 1989 usiwe mbulula
Kimbari ni 1994
Humu tuna mizimu aisee ..[emoji848]Ahahahaha! Pole sana ndugu yang lakin haya matusi na kejeli zote hizi umezitaka wewe mwenyewe
Nasema hivii wew ulistahili kutukanwa tena zaidi ya hapa. Shubamiti wew, Kichwa kama sambusa
Unaleta stori hapa aya mbili tu unasema itaendelea, afu unakuja kuleta comments za kubishana na wasomaji wako badala ya kuendeleza stori yako. Kama co Ungese ni nini huo? Wew ulistahili kutukana afu una bahati hujatukanwa sana
Go to hell
Namba 5 ndio maana pasco alizimwa na kitimoto yake. Hivi vinchi vyetu ukiruhusu watu watiririke kinanuka huwezi amini. Angalia wachungaji feki wenye karama za kuongea wanavyojichotea watu kwa muda mfupi tu. Africa ukimwaga petrol kidogo tu kinawaka!Kitu nimejifunza hadi sasa:
1. Kutajwa kwa Dar, Nairobi, Kampala, Kinshasa, Ufaransa, Ubeligiji na Marekani, ni dhahiri vita haikuwa ya watusi na wahutu peke yao. Majabari ya vita hiyo yalikuwa nje ya Rwanda.
2. Vita si ya kujaribu kabisa kwani shetani hufanya kazi mwenyewe badala ya kuwatuma wasaidizi wake.
3. Kwamba malori yalipita juu miili ilozagaa barabarani, ni ishara kuwa mapigano Rwanda yalifikia hatua ambayo pengine ulimwengu haukuelezwa ukweli wa kilichoendelea huko na hivyo kukosa usaidizi stahiki wakati muafaka.
4. Ubalozi wa Tanzania kuwa kimbilio, na kutoshambuliwa kama ilivyokuwa kwa balozi nyinginezo kunatia mashaka iwapo hatukuwa washirika muhimu katika vita hiyo.
5. Media, hasa redio ni chombo hatari mno kikishindwa kufuata misingi bora ya kiutendaji.
Mwisho kuliko vita ije hapa kwetu bora CCM watawale milele.
Sent using Jamii Forums mobile app
OK kama kuna case bado zinaendelea ICC hawataweza kuzidisclose. Hongera kwa kuchukua tahadhali zote. Tunajifunza mengi katika hili na kuweka historia sawa kwa wale ambao hatukushuhudia haya zaidi ya kujua kwamba kilinuka huko..Hawawezi kutoa nyaraka hata moja coz kuna watuhumiwa bado wapio ICC na bado kesi zao hazijaisha.na nimefuatilia kwa karibu sanaa lakini Hamna kitu
Sent using Jamii Forums mobile app
Kwanini umechelewa kuleta haya mambo miaka yote hiiAsante ,ila kama nilivyosema mwanzo najitahidi kukumbuka .kichwa kimechoka uzee babaa nisamehe.simu yenyewe natumia ya tigo tujiftishe.
Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]1994 nilikuwa na miaka 10 ndani ya Kigali anavyosema mleta uzi vita isikie tena ya kikabila isikie tu, ndani ya Rwanda wanasema shetani hutuma malaika wake, lakini pale Rwanda shetani aliamua kushuka mwenyewe kupiga kazi,
Tulibahatika kufika ngara lakini ni kudra za Mungu tu, huwa narudi kwenda kuichungulia (musozi tu) maana kuna rafiki yangu amelala pale
Sent using Jamii Forums mobile app
Kitu nimejifunza hadi sasa:
1. Kutajwa kwa Dar, Nairobi, Kampala, Kinshasa, Ufaransa, Ubeligiji na Marekani, ni dhahiri vita haikuwa ya watusi na wahutu peke yao. Majabari ya vita hiyo yalikuwa nje ya Rwanda.
2. Vita si ya kujaribu kabisa kwani shetani hufanya kazi mwenyewe badala ya kuwatuma wasaidizi wake.
3. Kwamba malori yalipita juu miili ilozagaa barabarani, ni ishara kuwa mapigano Rwanda yalifikia hatua ambayo pengine ulimwengu haukuelezwa ukweli wa kilichoendelea huko na hivyo kukosa usaidizi stahiki wakati muafaka.
4. Ubalozi wa Tanzania kuwa kimbilio, na kutoshambuliwa kama ilivyokuwa kwa balozi nyinginezo kunatia mashaka iwapo hatukuwa washirika muhimu katika vita hiyo.
5. Media, hasa redio ni chombo hatari mno kikishindwa kufuata misingi bora ya kiutendaji.
Mwisho kuliko vita ije hapa kwetu bora CCM watawale milele.
Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe hadi leo hujamaliza kisa chako cha kuliwa masikio na dubwana la ajabu na jini lililotengenezwa na Juma Njemba wa ujiji kigoma...
Mkuu tuletee pia na version yako inafikirisha sana, ila mpk watu wanafikia kupigana ujue wamegota mwisho kwa uonevuNdege hio wakati inadunguliwa nilikua Kigali usiku huo. Eneo ndege hio ilipodunguliwa linaitwa Kanombe jirani kabisa na uwanja wa ndege na ikulu ya wakati huo.
1. Mleta uzi ametaja kua ubalozi ulikua eneo la Kicukiro jambo ambalo kama lingekua kweli ukiwa eneo hilo huwezi kuona anga ya eneo la tukio.
2. Ubalozi wa Tanzania ulikua eneo la Kacyiru ni karibu na eneo la tukio na ilisikika milipuko miwili hivi na mwanga sisi hatukuona wingu.
Note: Balozi zote na mashirika makubwa ya UN au ya kimataifa yalikua katika maeneo matatu (Kacyiru, Kimihurura na Kiyovu)
3. Njia waliopita hao ni ndefu sana na unavuka na unavuka wilaya kama tisa hivi kama sijasahau.
4. Diplomats wengi na wafanyakazi wa UN agencies wengi ilikua wakipata shida wanaita wanajeshi wa UNAMIR sijui kwa nini wao hawakuwajua!!!
Nina historia mbaya katika safari nilizofanya kule kati ya 1990-1994.
Mleta mada usichoke kuwahadithia watu humu kuna mengi ya kujifunza.
Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji23][emoji23][emoji23]Alisikika boss wa interahamwe aking'aka
Mnaanza uchawi eeeeeenh kwamba itaendelea kwenye kitabu auPole sana kwa maswahibu yote uliyoyapitia lakini naomba nikushauri kama alivyokushauri mtu mmoja huko juu.., Hii simulizi au ushuhuda wako ni bonge moja la utajiri kama ukiangalia kwa jicho la tatu, achana na kutoa kitabu na kuuza locally hapa Tz,, kuna fursa ya uuzaji vitabu online through Amazon, kule process zote ni bure (ni wewe na mb zako na kompyuta yako) Naamini kabisa kwa kisa hiki ukiiandika vizuri kabisa tena kwa lugha ya kingereza, ukafunguka mambo mengine ambayo humu haujayasema lazima kiuzike, who knows unaweza pata hata connection kitu kikatengenezewa movie.
Ni ngumu lakini sio kama haiwezekani, na sio kwamba lazima ufanye hivi lakini ushauri tu nimekupa, bahati mbaya sana na mimi bado beginner najifunza jifunza bado ili niweze kuitumia hii fursa.. Kama utapendezwa na wazo langu,, ingia you tube mtafute jamaa anaitwa ERNEST MAKULILO ni Mtanzania, anayeishi Marekani. kaeleza process zote jinsi ya kujisajili, kuandika na ku upload kitabu amazon free kabisa kwa ajili ya kukiuza (ila baadae Amazon watakukata pesa ndogo sana baada ya kitabu kuanza kununuliwa, means hautatoa hela yako yoyote mfukoni kuwalipa),, Huyu ERNEST MWAKULILO yeye mwenyewe anafanya hivyo na kauza vitabu kadhaa tayari.
Sent using Jamii Forums mobile app