Sanaa kuna vitu nikiviweka humu hata Washington. DC watanisaka kwa udi na uvumbi ndo maana mengine nafukiafukia tu.liende
Sent using Jamii Forums mobile app
Wale watu hawakua wanapigana wala kuuwana bali walikua wanaua tu. Na ilkkua ni mauwaji yaliopangwa. Bora wangeendelea kupigana baina ya majeshi ya serikali na majeshi ya Kagame hadi mshindi apatikane au wange implement makubaliano ya Arusha waliokua wote wamesaini bila kuua raia.Mkuu tuletee pia na version yako inafikirisha sana, ila mpk watu wanafikia kupigana ujue wamegota mwisho kwa uonevu
Sent using Jamii Forums mobile app
Uchawi upi? Ule ni ushauri tu nimempa maana yake sio kwamba aikatishe hapa ili aitolee kitabu, hapana, nadhani utakua hujanielewa point yangu.. Unajua hizi issue za history history ni asset kubwa sana hasa kwa wenzetu wazungu wanaopenda mambo ya kufanya tafiti na documentary..
babu nakushauri kwa hapa ulipofikia waambie inaendelea kwenye group la wassap anayetaka kujiunga analipia sh 2000 nakuapia litajaa na utapiga mpunga balaa teh teh teh teh
Bahati mbaya mlolongo wa masimulizi haujapewa namba ili nikurejeshe katika kipande husika, Bossless alidai ubalozi wa Malawi na nyinginezo zilivamiwa siku chache kabla ya hawajapandishwa malori kuondoka Kigali, wakati huo mambo yalipamba moto. Vamizi za balozi hazikulenga wanadiplomasia bali wale wanyarwanda walokimbilia hapo kusaka hifadhi kama ambavyo walikuja ubalozi wa Tanzania. Na hadi watanzania wanaanza safari yao, hakukuwa na shambulio wala uvamizi mkubwa kwenye ubalozi wetu.Hapo namba 4 ni balozi zipi zilishambuliwa na watu kuuawa ndani ya balozi hizo? Kuheshimiwa kwa ubalozi wa Tanzania siyo kwa sababu ya jitihada zake ilizokuwa ikifanya na pia kuwa mwenyeji wa mazungumzo ya kutafuta muafaka kati ya serikali ya Habyarimana na vyama vya upinzani ambavyo baadhi yake vilikuwa vikiendesha vita ya msituni?
Umeonaeee wameanza kumhamisha mawazo mleta mada wakati jamaa ameamua kutema nyongo tu kwa yanayomsumbua siku nyingi.
Mkuu! wakati raia wanauawa hovyo hawa askari wa UNAMIR walikuwa kimya tu bila kufanya kitu?Wale watu hawakua wanapigana wala kuuwana bali walikua wanaua tu. Na ilkkua ni mauwaji yaliopangwa. Bora wangeendelea kupigana baina ya majeshi ya serikali na majeshi ya Kagame hadi mshindi apatikane au wange implement makubaliano ya Arusha waliokua wote wamesaini bila kuua raia.
Sent using Jamii Forums mobile app
Well spoken kiongozi. Na nikwambie kitu mara baada ya ndege ile kushambuliwa na kuuawa kwa marais hao mtutsi yeyote aliyekuwa ughaibuni alifanya sherehe kubwa au ndogo, kwa uwazi au kwa usiri kufurahia tukio hilo.Bahati mbaya mlolongo wa masimulizi haujapewa namba ili nikurejeshe katika kipande husika, Bossless alidai ubalozi wa Malawi na nyinginezo zilivamiwa siku chache kabla ya hawajapandishwa malori kuondoka Kigali, wakati huo mambo yalipamba moto. Vamizi za balozi hazikulenga wanadiplomasia bali wale wanyarwanda walokimbilia hapo kusaka hifadhi kama ambavyo walikuja ubalozi wa Tanzania. Na hadi watanzania wanaanza safari yao, hakukuwa na shambulio wala uvamizi mkubwa kwenye ubalozi wetu.
Yaani kitu ambacho akili yangu huwa haikiamini katika mikutano ya usuruishi ni nia ya dhati ya wenyeji wa mikutano hiyo. Mara nyingi wasuruhishaji wanao upande wanaoutegemea ushinde. Ndo maana tunayo matukio kadhaa ya viongozi kulipuliwa angani wakitokea katika hiyo mikutano ua suruhu! Rejea kwa Museveni dhidi ya South Sudan; Abyarimana na mwenzake wakitokea Tz... Hata Nkurunziza amekataa kuhudhuria baadhi ya mikutano kwa hofu ya kukutwa na yalowakuta watangulizi wake.
Jamii huelezwa kile ambacho wakuu wanataka kifahamike, ukweli huwa hauwekwi hadharani.
Sent using Jamii Forums mobile app
Kunya ni haki ya kiafya si ya kikatiba, kama wewe haunyi ujue bawasili ndo inakwamisha...nakutania mkuu!Good analysis ila hapo mwishoni umekunya japo ni haki ya kikatiba kunya
HahahahahaBossless, Babu babu uko wapi wajukuu tushaoga tupo kibarazani tunakusubiri
Sent using Jamii Forums mobile app
Tunaweza kusema mauaji ya huko Rwanda yalichochewa zaidi na chuki ya kikabila ndani ya Rwanda kwenyewe na kama kuna uhusika wa nchi jirani huenda ni kwa uchache sana tofauti na chanzo kikuu ambacho ni chuki za kikabila ndani ya nchi husika.Well spoken kiongozi. Na nikwambie kitu mara baada ya ndege ile kushambuliwa na kuuawa kwa marais hao mtutsi yeyote aliyekuwa ughaibuni alifanya sherehe kubwa au ndogo, kwa uwazi au kwa usiri kufurahia tukio hilo.
Wiki chache sana kabla ya tukio la ndege kutunguliwa kulikuwa na mkutano mkubwa sana pale jijini Mwanza uliowakutanisha watutsi wote kutoka kanda yote ya ziwa. Mkutano huo mkubwa na wa aina yake ulifanyika pale Vijana Social Hall jirani na uwanja wa mpira wa CCM Kirumba. Lango kuu kulikuwa na udhibiti mkubwa sana na walioruhusiwa kuingia ndani ni watutsi pekee yake.
Hata hivyo mimi nikiwa nje nilibahatika kuwaona watu fulani watutsi waliokuwa wakiishi Mwanza kipindi hicho kwa kivuli cha wafanyabiashara na wengine watumishi wa serikali waliokuwa na nyadhifa kubwa kubwa kwenye taasisi mbalimbali za serikali wakihudhuria mkutano huo ulioashiria kwamba kuna jambo kubwa walikuwa wanapanga kulitekeleza, wanataarifiwa au kuwekana sawa. Kiufupi hakuna mtutsi yeyote aliyekuwa na umri wa zaidi ya miaka 18 ambaye hakuhudhuria mkutano huo pasipokuwa na sababu maalumu maana kulikuwa na uhamasishaji sana ili wahudhurie bila kukosa.
Baada ya vifo vya marais hao wawili, mauaji ya kimbari yaliyofuatia na baadae watutsi wengi kurudi kwao Rwanda, wengi wa watu hao niliowafahamu waliokuwa katika mkutano huo walipata nyadhifa kubwa kubwa katika serikali ya Rwanda.
Hata baadhi ya watu nchini (watutsi) waliokamatwa kwa kudaiwa kufanya sherehe za waziwazi kutokana na furaha waliyokuwa nayo baada ya kuuawa kwa marais hao, baadae waliachiwa huru kwa amri kutoka mamlaka za juu. Ndiyo maana kuna speculations za hapa na pale kwamba hata TZ kuna upande ilikuwa ikipendelea kwenye yale majadiliano yaliyokuwa yakiendelea ili kuleta muafaka wa amani/kiuongozi.