Sintosahau nilipomnyooshea mwalimu kidole cha kati

ACTIVIST13

Member
Joined
May 26, 2018
Posts
13
Reaction score
16
Kwanza kabisa nianze kwa kusema "Fuata taratibu zote za kujilinda na korona "

Niende moja kwa moja kwenye mada yangu, aise ilikua mnamo mwaka 2005 shule la msingi X mkoani Kilimanjaro. Nakumbuka ilikua ni Juma 5,siku ambayo kulikuwa na ukaguzi wa usafi, kulikuwa na utaratibu ya kuwatoa watu wachafu na kuwaadhibu viboko vya kutosha tu mbele ya shule na wanafunzi wote.

Basi bwana, siku hiyo nakumbuka mwalimu alinikurupua kasehemu fulan ambako nilikuwa najificha mara nyingi kwani nilikuwa sipendi kwenda parade hivyo ikanibidi siku hiyo nikae parade maana chimbo lilikuwa limeshavamiwa. Sasa nilikuwa nimejisahau kukata kucha na pia soksi zilikuwa za rangi nyeusi badala ya nyeupe, Mwalimu Sarah bila kuhoji aliponiona tu akasema wewe apo toka mbele. Ah! nikajifanya sijasikia na nikawa simuangalii, akarudia tena wewe hapo mweusi kuliko wote toka mbele, nikajifanya sio mimi tena. Aisee Mwalimu Sarah si akanisogelea, ohoo akaona na kosa jingine la kucha hapo hapo akanitoa mbele na viboko vya mgongo vikinifuata nyuma.

Baada ya kufika mbele nakumbuka mwalimu mmoja alikuwa anaitwa Mwalimu Mponji akakaidhiwa kiboko atuadhibu dadeki yule ticha alikuwa anajua kuchapa aise alinipiga 5 nzito nilihisi nimeshushiwa gunia la nyuki matakoni, bas bwana baadae wakatuachia tukaingia darasani.

Muda wa chai mara nyingi walimu walikuwa na tabia ya kuita mwanafunzi yeyote wanamuagiza vitafunio center fulani hivi, basi bwana mida ya chai imefika hivi nakumbuka nilikuwa wa kwanza kutoka darasani, nikaona mwalimu Mponji ananiita kwa mbali "Wewe dogo, njoo nikuagize maandazi hapo madukani"

Aise sababu niliamini hanijui vizuri na alikuwa distance kidogo na mimi aise nilimnyooshea middle finger halafu nikatafuta uelekeo wangu mwendo. Aah! me nikajua nimesave, ile ile mida hata dakika 8 zilikuwa hazijapita nipo zangu njiani nawahi chai na kiporo cha mama mzazi nikaona vijana wa 4 kwa nyuma yangu wanakuja wanakimbia mdogo mdogo kama hawana muda na mimi, nakumbuka walikuwa ni darasa la 7 wale walikuwa wakubwa kwangu maana me nilikuwa darasa la 5 muda huo. Aise, ile wamefika tu kwangu nkashangaa wamenivaa wakanichukua ki so so (kinguvu nguvu), wale machalii walinibeba bwana mpaka shule. Aise ile siku nilipigwa na kaofisi kote ka nidhamu.

Mwalimu Mponji akawa hasemi nimemtukanaje ila walimu walikuwa wakifika wakiuliza dogo kafanya nini akawa anawaambia dogo kanitukana, wakimuuliza kakutukanaje anawajibu kanitukana dogo hana adabu.

Kesi iliisha hata home haikufika il yule ticha Mponji ndio alikuja kuwa rafiki yangu mkubwa sana, ila baada ya muda alihamishiwa huko Tarakea ndio tukapotezana mpaka leo hii. Tafadhali kama mwalimu Mponji yupo humu naomba niPM nimekukumbuka sana teacher wangu.
 
Mm nilipokuwa darasa la tano tusi pekee nililokuwa nalijua ni 'shenzi'
 
Ajabu hii. Umeficha jina la shule umetaja majina ya waalimu.
 
Write your reply...WENGINE DARASA LA TANO TUNAVIZIA WALIMU WANOKO USIKU TUNAWACHAPA BAKORA
 
Sasa hivi unatkansna na maisha sasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…