Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Video hii imerekodiwa katika eneo la Sinza Afrikasana Jijini Dar es salaam ikionesha usumbufu wanaoupata wapita njia pamoja na magari na kuathiri shughuli za kila siku baada ya maji kujaa katika eneo hilo kutokana na mvua iliyonyesha leo.
Wakazi wa eneo hilo wanasema hali hii imekuwa ikijirudia kila msimu wa mvua na kusababisha ucheleweshaji wa shughuli za kiuchumi na kijamii hivyo wameziomba mamlaka husika kuchukua hatua za haraka na za kudumu ikiwemo kuboresha mifereji ya maji ya mvua ili kuondoa tatizo hilo