Sio ajabu jana Mayele angefunga goli la 18 Saido naye angefunga goli la 18

bryan2

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2016
Posts
3,323
Reaction score
4,679
Yes Yanga mabingwa tena la 29 kibindoni sio ubingwa tu pia wanamedali za Caf shirikisho kama mabingwa waliofanana, sio Caf tu pia wana medali za ngao ya jamii waliyoipata baada ya kumnyoa Simba chuma 2.

Huku wale wa upande wa kule wakibaki wanalilia kiatu cha mfungaji bora kama kombe lao la kujivunia msimu huu,nachelea kusema magoli ya Saido ni magoli ya kupikwa maabara ni magoli ya mchongo ni magoli ya kimkakati kwanini nasema hivi jamaa alipewa maelekezo wewe ukitoa free kick lenga goli tu na kweli kila free aliyokua anapiga ikipita ukuta tu ujue hiyo himo.

Yanaweza kuwa na maelekezo kutoka juu au jamaa wamepitisha mlungula lipo wazi Tff haimpendi Mayele ukiangalia hata aliyepewa kiatu mwaka jana kapotea kabisa alitengenezewa mazingira tu ya kupata kiatu huku mayele akizidi kufanya vizuri.

Magoli yote ya Mayele ni magoli ya kutoa jasho hakuna goli hata moja la kupikwa maabara kama ya Saido Mayele hana goli la penalti pia tukumbuke ligi kuu anacheza pia Caf anacheza tena karibia michezo yote.
 
Jana nimemsikia Mayele kwenye short interview baada ya mechi, alihojiwa baadhi ya maswali nikapenda respond yake.

Baada ya nuda kupita journalist mwingine akamfata Mayele akiwa yupo kwenye gari amekumbatia kombe.

Akamuuliza maswali yale yale aliyoulizwa mwanzo, katika hali isiyo ya kutarajia nikastuka kumuoa jamaa anatoa maneno ya majivuno.

Akawa anasema "mimi ndio mfungaji bora kwakua sina goli la penati, hata wakiunganisha magoli yao yote bado hawawezi kunifikia mimi. Nawakera sana"

Hapa nikafikiri vitu viwili.

Kwamba mwana ule wakati anajibu kiungwana bila nyodo alikuwa anajibu vile kwakua hakua na uhakika kuwa anaweza kuwa mfungaji bora kwasababu hajui sheria zinazoamua.

Ila alipopata taarifa kutoka kwa watu waliokuwa wanasema sheria inasema mfungaji bora ni yule ambaye hana penati.

Hiyo ikamjengea confidence kujiona ame qualify hivyo akaona ni muda sasa wa kutuonesha upande wake wa pili wa sarafu kwa kumdhihaki competitor mwenzake.

NB: Bado haijafahamika rasmi mfungaji bora ni nani, zile claims za kusema "ni yule ambaye hana penati" hizo zilikuwa maalumu kwa ajili ya msimu ule na kila msimu unakuwa na sheria zake na ndio maana upo msimu ambao ulitoa wafungaji bora wawili.
 
Tff watamaliza Kila kitu,haraka ya nini!?
 
Niliiona hiyo video. Yanga hawajifunzi tu kuwa majivuno ya kupitiliza yanawakwamisha. Timu ina ushamba mwingi na ulimbukeni wa mafanikio.
 
Teh teh teh teeeeeh!


🟩🟨🟩🟨🟩🟨
 
Hoja yako ni ipi? Kwamba Mpole hakustahili kiatu mwaka jana? Yanga ile kanuni ya sope inaendelea kuwatesa hahaa
 
Assist [emoji91][emoji91][emoji91]
Mechi chache magoli mengi
Penat umepewa ukakosa
Ahame ligi ya zenji ndyo atachukua mfungaji bora
ni mfungaji bora na sio mtoa pasi bora.. umeelewa
 
Kiufupi bdo watu hawajaelewa kutokana na kanuni zetu za mpira wetu bongo[emoji1]
 
Niliiona hiyo video. Yanga hawajifunzi tu kuwa majivuno ya kupitiliza yanawakwamisha. Timu ina ushamba mwingi na ulimbukeni wa mafanikio.
Taarifa kwamba Yanga kuanzia uongozi, wachezaji na mashabiki wana ushamba na utoto, ni ya kweli na facts zinazothibitika. Jana Mayele kathibitisha kwa upande wa wachezaji
 
Changamoto ambayo naona baadhi ya wachezaji wa kigeni ni kuwa na uchache wa lugha ili kujua namna ya kupanga maneno ya kuongea,hiyo imekuwa ikimkabili Mayele ingawa natambua ni vema kuwa na friendly rival kwenye mpira ili kutengeneza drama isiyoisha .
 
Mayele anaongea kiswahili fluently kabisa huwezi kumfananisha na Chama

Hata hivyo kwenye interview yake ya awali aliongea kwa busara sana huku akimpa pongezi mchezaji mwenzake Saido.

Lakini baadaye alikuja kubadilika na kuja na maneno ya kebehi na majivuno.
 

Linamajivuno ndyo maana halifanikiwi
Eti magoli ya penati sina ohh anatafuta huruma wakina kagere tambwe misimu miwili mfululizo top Score lkn hawana majivuno
 
Msimu huu hakuna kanuni hiyo labda watengeneze leo. Naamini wataitengeneza tu ili angalau Kolo apate chochote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…