Sio ajabu jana Mayele angefunga goli la 18 Saido naye angefunga goli la 18

UTARATIBU WA FIFA UPO KAMA IFUATAVYO.

1.Wanaangali mchezaji aliyefunga MAGOLi mengi zaidi kwenye mashindano.

2.kama wachezaji wamefungana wame( tie) MAGOLi aliyecheza MICHEZO MICHACHE ndio anapewa ufungaji Bora.

3.kama wote WAMECHEZA michezo sawa wanaangalia Mchezaji MWENYE Asisist nyingi.

KAMA TUNGEKUWA TUNAFUATA SHERIA ZA FIFA SAIDO ANGEKUWA MFUNGAJI BORA NBC 2022-2023.
 
Kama jana, Mayele angefunga goli la 18 dakika ya 90 +3...
Je... Saidoo angefunga goli la 18 dakika ya ngapi...?

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Sheria/kanuni zikitungwa zinaendelea kufanya kazi mpaka pale zitakapobadilishwa au kufutwa.
Kama msimu huu hawakutunga kanuni mpya maana yake za msimu uliopita ZINAENDELEA.
 
Sheria/kanuni zikitungwa zinaendelea kufanya kazi mpaka pale zitakapobadilishwa au kufutwa.
Kama msimu huu hawakutunga kanuni mpya maana yake za msimu uliopita ZINAENDELEA.
Kwani kuna sentensi inasema zitaanza kutumika 2021/2022 na kuendelea hadi itakapotungwa nyingine?? Kanuni imefunga Moja kwa Moja "2021/2022" Kwa maelezo yako , ingekuwa hivyo basi jana hiyohiyo mfungaji bora angejulikana.
 
Kwani kuna sentensi inasema zitaanza kutumika 2021/2022 na kuendelea hadi itakapotungwa nyingine?? Kanuni imefunga Moja kwa Moja "2021/2022" Kwa maelezo yako , ingekuwa hivyo basi jana hiyohiyo mfungaji bora angejulikana.
Mimi nimekupa principle za mambo ya kisheria.
Mfano Kiongozi wa kuchaguliwa akimaliza muda wake haondoki mpaka achaguliwe mwengine hata kama Sheria ilikuwa kimya kukusu hilo.
Turudi kwenye mpira. Ule msimu Covid 19 ilipokua imepamba moto, ligi ya Misri kabla haijamalizika ikawa msimu umeisha kunatakiwa majina ya timu zitakazocheza michuano ya CAF.
Kwakujua principles za Sheria, walichofanya ni kuangalia msimu wa nyuma yake tu Basi, hakucheki nani kwa sasa yuko wapi wala nini.
Na kama ni kweli kanuni hazisemi chochote kuhusu hili basi huwezi kulitungia leo. Sheria zinaangalia mbele baada ya kutungwa na sio nyuma kabla haijatungwa.
 
Acha Uongo Misri hawakuangalia msimu wa nyuma yake bali waliangalia msimamo wa ligi kwa wakati huo!!!


Pia si Kwamba Bodi ya ligi hawana kanuni, Kanuni za ligi kwa mwaka 2022/2023 zipo lkn hazifafanui nini kifanyike ikitokea wafungaji wakilingana magoli!!!


Lkn mwishoni Mwa Kanuni hizo imetamukwa, Mambo yote ambayo hayako kwenye Kanuni yatatolewa Maamzi na Kamati kwa uzingativu wa Katiba ya TFF na au Miongozo ya CAF na FIFA!
 
Tufanye basi saido Top score....! kwaio hilo ni moja ya mafanikio yenu wana simba?
 

Muongo ni wewe usie na kumbukumbu.
Pyramid walilalamika kwanini Al Ahli kupewa nafasi CAFCC wakati wao ndio walikua wanaongoza.

Mimi sijakusudia kua Kanuni kwa ujumla wake hazipo, soma kwa makini, nilikuwa nazungumzia kanuni zijazo husiana na kufungana mfungaji bora.
Lakini Mimi nilichogundua kwenye mijada mingi sisi Makolodunduka wengine hatuna hoja zaidi ya Ushabiki maandazi na wengi zaidi tunajitoa ufafamu (tunazifyatua), lakini hata hivyo by accidentary unaweza kukutana na wa tofauti na makundi hayo 2 ingawa probability of occurance ni sawa na probality ya kukuta bucha ya kiti moto kule marikiti za Pemba.
 
Ndg ungekuwa hata na chembe ya kumbukumbu au kama huna jaribu hata kugoogle kwa wakati Misri wanatuma majina Pyramid alikuwa nafasi ya ngapi na Al-ahly ya ngapi?


Pyramid alilalamika baada ya ligi kuisha huku yeye akimpita mpimzani wake!!!


Hilo la kanuni za Bongo tuliache tu maana huelewi chochote na wala hueleweki unasimamia nini!!!
 
Basi tuishie hapa maneno yasiwe mengi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…