Sio kila kitu ni cha kubinafsisha; kama kinalipa kwanini wasifanye mpaka wapewe vya kufanya?

Sio kila kitu ni cha kubinafsisha; kama kinalipa kwanini wasifanye mpaka wapewe vya kufanya?

Logikos

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2014
Posts
15,460
Reaction score
24,233
Kuna Faida Tofauti na sio lazima iwe ya Kiuchumi..., Huduma ina faida zaidi hata ya hayo so called Gawio....; Unapobinafisha huduma bila mbadala..., mwisho wa siku mwananchi atalipia zaidi kupitia kodi yake (ruzuku) au Huduma Hafifu; Ushauri ni Kuchochea Ushindani (Hao so called Private Sectors washindane na UMMA... cha kubadilisha ni kuhakikisha Uwajibikaji (Mkono ukichafuka unaoshwa na sio Kukatwa)

Huduma nyingi za Umma hazina Mbadala - Public Services are Natural Monopolies
Vitu kama Elimu, Afya, Usafiri na Nishati ni vitu vya lazima na mtu hawezi kuamua kwamba niache.., vitu hivyo vyote vikiwa mikononi mwa watu ambao kipaumbele chao ni faida na hakuna mbadala mwisho wa siku ni mwananchi ndio atakayeumia; lazima kuwe na choice ambayo ni affordable kwa mwananchi na pia kuwe na alternative kwa wale watakaotaka premium. Ukiweka faida kama kipaumbele kwenye vitu ambavyo ni vya lazima (hauna choice) kutafanya huduma kuwa mbaya zaidi

Upotevu / Ufujaji wa Kodi na Mapato

Pesa ambazo unatoa kwenye malipo na kodi zinafaa kwenda katika kuboresha huduma za umma. Lakini ikiwa huduma hio imebinafsishwa, gawio lazima lilipwe kwa wenye hisa. Viwango vya riba ni vya juu kwa makampuni binafsi kuliko ilivyo kwa serikali. (Pamoja na hayo, kuna gharama za ziada za kuunda na kudhibiti soko bandia.), Mbaya zaidi kampuni hizi binafsi hususan zikiwe kwenye sekta isiyo na ushindani wa asili zikipata hasara ni Kodi zako ndio zitatumika kuwalipa ruzuku.

Kutumia Njia za Mikato
Ili kupata faida mara nyingi kampuni binafsi mambo kama afya, mazingira na ustawi wa watumiaji huwekwa kando hususan wanapojua kwamba ni vigumu kuwashika au watatengeneza njia za kuweza kuhonga wakaguzi ili wapunguze gharama iwapo hongo itakuwa ndogo labda kuliko kugharamia kutokuharibu mazingira

Kuchambua huduma za Kufanya
Iwapo kuna huduma zenye faida na nyingine zisizo na faida kampuni binafsi zitajikita kwa zenye faida na kule ambapo hakuna faida patajikuta panakosa huduma au kupata huduma za kinadharia (kusuasua) au kudai ruzuku kwa serikali ili kutoa huduma sehemu hizo

Vishawishi Vya Profit at all Costs hupelekea Uhalifu
Mfano kama kampuni binafsi itapewa kuendesha Magereza na ili wapate fedha zaidi wanahitaji kuhudumia wafungwa zaidi..., hili linaweza kupelekea wao kuhakikisha watu wengi zaidi wanafungwa.

Ugumu wa Usimamizi
Kama ni watu hao hao wameshindwa kusimamia mashirika ya Umma na kuyaendesha hata ukiwapa kazi ya kusimamia na kuchunguza mashirika binafsi kama yanafanya kazi watakachofanya ni kula Rushwa na kujitajirisha na kubadilika na kuwa watetezi wa mashirika husika na sio UMMA

Kupoteza Uwezo
Kama tukiuza Commanding Heights zetu zote na kuwapatia watu ambao ndio watakuwa wanafanya hata ule uwezo wa kuyachukua baadae tutakuwa hatuna sababu tutakuwa hatuna ujuzi wa kuyaendesha tofauti na kama tungejikita kwenye kujifunza uendeshaji na uboreshaji na kushindana na sekta binafsi na kuwa kama kichocheo cha mfano wa kuigwa hivyo kupelekea hata sekta binafsi kushindana na sisi (UMMA)

Walipa Kodi ndio Dhamana
Tambua kwamba Makampuni ya Huduma za Jamii ni ya lazima na hayawezi kuachwa yakaanguka, iwapo yakianguka ni Kodi zako ndio zitatumika kuyanyanyua.., na yasipopata faida ni Kodi zako ndio zitagharamikia
 
 
Back
Top Bottom