SteveMollel
JF-Expert Member
- Jul 12, 2015
- 8,797
- 25,177
Baada ya kuponea maisha kwa kuzama ndani ya ziwa la barafu, kipindi akiwa msichana mdogo, Cecilia alikata shauri la kumtumikia Mungu kwa kipindi chake chote alichobakiza duniani.
Kwahiyo anapofikia umri, anajiunga na 'convent' ya hapa Italia ili apate kuwa sister kwa kiapo na matendo.
Hivyo anakaribishwa na mama mkuu kisha na sister Isabela ambaye anamsindikiza ghorofani kumwonyesha chumba chake.
Huko juu Isabela, ambaye ni mwenyeji hapa, anamwambia Cecilia mambo mawili; moja kuna eneo ambalo ni 'off-limit' kwa kila sister kukanyaga lakini pili bado ana uwezo wa kugeuza mawazo yake, akakataa kuwa sister na kuondoka eneo hili.
Baadae Cecilia, katika tafrija fupi ya usimikaji, anakutana na Father na Kadinali. Watu hao wanamlisha kiapo, anakuwa sister kamili.
Lakini usiku huu kabla haujaisha, Cecilia anasikia sauti toka kanisani. Sauti ya mwanamke akilia.
Anaenda kutazama, huko anamkuta mwanamke akiwa amelala kifudifudi. Anajaribu kumgeuza akimuuliza kama yuko sawa. Anashangaa mtu ana sura nyekundu.
Anashtuka, na mara anaonana na Mama Mkuu aliyekuwa amesimama nyuma yake. Mama anamwonyesha msumari takatifu ulotumika kumsulubisha Yesu ila kidogo Cecilia anapoteza fahamu na kujikuta kitandani.
Anapoamka anaenda kuungama dhambi zake kwa Kadinali. Anaamini alizidisha mvinyo kwenye tafrija ya jana yake ndo' maana akapoteza fahamu.
Akiwa anaungama, anashangaa Kadinali hasemi kitu, zaidi anageuza uso na kumtazama na mara, kufumba na kufumbua, anadakwa na mikono isiyojulikana imetokea wapi na anastaajabu amelala katikati ya mabwana walovalia majoho meusi.
Bwana mmoja ananyanyua kisu na kumchoma Cecilia tumboni.
Cecilia anaamka tena kitandani akiwa amejawa na woga. Kumbe muda ule hakuwa ameamka, ilikuwa ni ndoto ndani ya ndoto.
Anatupa macho yake gizani, anamwona mtu kasimama kwenye kona. Anawasha taa na kuangaza, hamna kitu tena.
Usiku mwingine, anakurupuka baada ya kusikia sauti ya mtu akihema. Anapotazama anamwona sister mmoja mzee akiwa kando yake.
Anamsaidia sister huyu kumrudisha kwenye chumba chake lakini kabla hajamwacha, anagundua mwanamke huyo mzee ana nyayo zenye makovu ya msalaba.
Kesho yake, akiwa pamoja na wenzake; sister Gwen na Isabela, anajaribu kusema yale aliyoona kwa macho yake lakini hamna anayejali. Ni kama vile anayoongea ni marudio hapa.
Kidogo anapandwa na kichefuchefu kikali, anatapika.
Baadae, Mama Mkuu anamwita mbele ya Father na Kadinali. Haelewi ni nini kinaendelea. Kufika anaambiwa kwa ukali kwamba amekiuka kiapo cha sister kwa kutembea na mwanaume ingali yupo kwenye huduma.
Anastaajabu!
Anaambiwa vipimo vinaonyesha kuwa amebeba ujauzito tumboni. Kwanini amelidanganya kanisa?
Cecilia anakana. Anasema katu hamjui mwanaume tangu kuzaliwa kwake, na haelewi ni nini wanachozungumza watu hawa.
Baada ya kujiridhisha, wakuu wanamtawaza Cecilia kuwa mama mtakatifu wa pili, baada ya mama Maria alomzaa Yesu, kwani wote wamebeba mimba kwa uweza wa roho mtakatifu na hivyo uzao wa Cecilia utamleta pia Messiah duniani.
Habari zinatangazwa rasmi ndani ya eneo hili na watu wanapokea kwa furaha isipokuwa watu wawili; sister Gwen na Isabela. Hawa kuna mambo yamo vifuani mwao.
Baadae, Cecilia akiwa anaoga, hana hili wala lile, Isabela anamvamia na kujaribu kumuua kwa kumzamisha kwenye maji.
Bahati yake, wanakuja wenzake na kumwokoa kabla ya kumkuta maafa. Wanamnyaka Isabela na kumburuzia nje huku akipayuka kwamba ile ilikuwa ni karama yake. Ni yeye ndo' alitakiwa kuwa kama Cecilia!
Baadae Cecilia anamwendea Father na kumuuliza ni nini Isabela alikuwa anamaanisha kwa kusema maneno yale. Father anamtoa hofu kuwa mwananmke yule ana ugonjwa wa akili, ni heri akampotezea.
Lakini ni kweli?
Baadae Isabela anajirusha kutoka ghorofani na kufa papo hapo. Sister Gwen naye anajaribu kumwonya Cecilia juu ya alichokibeba tumboni mwake na pia eneo hili walilopo, sio eneo la kawaida kama anavyoliona kwa macho ya nyama.
Akiwa anafanya hivi, Father anamwona na anajaribu kuingilia maongezi yao yafikie tamati.
Baadae usiku, Cecilia akiwa kitandani, mara anaona picha ya mama Maria mtakatifu iliyo ukutani inaegama upande. Anaiendea kutazama, nyuma ya picha hiyo, anaona maandishi yalonukuliwa kwenye Biblia, Wakorinto 2: 11 - 14.
Mstari huo unazidi kumwongezea mashaka alokuwa nayo, na sasa anaamua kuchukua hatua kujua ni nini kinachoendelea eneo hili.
Kwa tahadhari, anaenda kule alipokatazwa kufika, off-limited area.
Anaingia ofisi ya Kadinali na kuanza kupekua kwenye droo. Ajabu anakutana na taarifa zake za zamani. Habari za yeye kuzama na kuokolewa, na hata zaidi.
Anashangaa ina maana watu hawa walikuwa wanamfahamu hata kabla hajaja hapa? Anaona picha za ultrasound ya mimba yake na kidogo anasikia sauti ya mwanamke akilia.
Anatoka kwenda kufuatilia. Sauti hii inatokea wapi?
Anafika mahali, anachungulia kwenye tundu, anamwona sister Gwen, yule sister alojaribu kumpa tahadhari, yupo kifungoni analalamika kwa maumivu.
Mara kidogo, sister fulani ambaye hamfahamu, wala uso wake haueleweki, anaushika ulimi wa sister Gwen na kuukata kwa kisu!
Cecilia anahamaki.
Kufumba na kufumbua, anazibwa mdomo kwa kiganja cha mkono. Kugeuza uso, anamwona sister yule mzee yuko nyuma yake.
Sister huyo anampatia Cecilia kitu fulani mkononi mwake, na Cecilia anapomwomba amsaidie kutoroka eneo hili, anamwambia haiwezekani abadan!
Labda akiwa maiti.
Sasa ni nini sister Cecilia atafanya? Watu hawa wana mpango gani naye? Kwanini wengine wana chapa ya msalaba kwenye nyao zao? Na hii mimba alobeba tumboni ni ya kitu gani?
Tazama "IMMACULATE" (2024)
Kama unataka kuidownload, ingia Telegram search UZI MKALI utakuta movies zote.