Sio kila ndio ina ukweli kiundani kuna baadhi ya ndio zaambatana na utani

Sio kila ndio ina ukweli kiundani kuna baadhi ya ndio zaambatana na utani

bahati93

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2015
Posts
1,334
Reaction score
2,463
Jamii Hip #0p wozaa

Nadhani sina haja ya kusema mengi kwani kuna baadhi ya mambo yanafanana na utani. Mambo yenyewe ni msanii kulalamika kuibiwa mistari. Msanii ni mtu muhimu sana katika jamii yeye anafanya kazi sawa na watu wa dini na mizimu kwa namna yake. Mtu msanii hutumiwa na jamii kama kiungo fulani cha kuwaunganisha watu na nguvu hali fulani hivi inayoishi na jamii, hii hali kuleta hali fulani ya hisia mioyoni mwa watu.

Sasa changamoto ni pale msanii anapofikiri sanaaa yake ni mali yake na kusahau kuwa kapewa bure. Na hiyo nguvu huwa haina kikomo ukishaamua kujifungua ndani ya mtu. Endapo tu msanii ataleta ubinafsi wa kungangania kitu fulani alicho create hapo ndo linakuwa anguko lake kwa sababu hayo ni mawazo ya kimaskini. Na hiyo nguvu ya kuumba inamtoka, msanii ana kazi moja katika jamii nayo ji kuumba hivyo vitu vinavyofunguliwa kichwani mwake.

Yapaswa kustawi sio kufikiria ufinyu wa mali na mistari.
 
Back
Top Bottom