Sio kweli kwamba Wazanzibari hawana makabila

safuher

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2019
Posts
11,837
Reaction score
17,412
Suala la kwamba wazanzibari hawana makabila sio sahihi kabisa,wanayo makabila.

Huu uzi siandikii ati kwa kuwa makabila yataleta manufaa yoyote kwa wazenji ama madhara yoyote,bali naandika kusahihisha ufahamu tu.

Kwanza Kabila ni jamii ya watu yenye umoja fulani upande wa lugha na tamaduni, si lazima upande wa eneo na utawala wa siasa.

Kwa hivyo watu fulani wakiwa wanazungumza lugha mbayo wataelewano wao wenyewe lalini pia wakawa na tamaduni fulani ambao utawatofautisha na watu wengine hilo ni kabila tayari.

Zanzibar kuna kimakunduchi wanazungumza maneno na wana tamaduni ambazo ni tofauti na watu wengine.

Mmakunduchi akiwa anaongea kama wewe sio mmakunduchi huwezi kumuelewa,ila wao kwa wao wanaelewana.

Hili ni kabila tayari kwa sababu wana lugha yao maalumu na tamaduni zao kule makunduchi.

Tujikumbushe kidogo lugha ni nini?

Lugha ni mfumo wa sauti za nasibu zilizokua katika mpango maalum na zilizokubaliwa na jamii ya watu fulani ili zitumike katika mawasiliano.

Kwa mujibu wa maana hii kimakunduchi ni lugha kwa sababu kipo katika mpango maalumu.

Wamakunduchi wenyewe jamii yao wameikubali mfumo wa sauti hizo na zinaleta maana na wanawasiliana pia.
Lakini kwa asiyekuwa mmakunduchi hawezi kuelewa.

Je, kimakunduchi ni lahaja?

Kimakunduchi sio lahaja.

Turudi katika tafsiri ya lahaja,lhaaja mpaka sasa watu mbali mbali wameelezea neno la lahaja kinamna yake.

Mfano kuna maelezo yanasema hivi Lahaja ni vilugha vidogovidogo vya lugha moja ambavyo hubainishwa na jamii au jiografia.

kwa tafsiri hii manake kama kimakunduchi ni lahaja manake ni lugha tayari ila ni kilugha kidogo.

sasa swali la kujiuliza lugha ndogo inasifa ggan ama inapimwaje ?

kwa idadi ya wazungumzaji au kuwa na maneno mmengi?

Kama idadi ni wangapi?
Kama watu wawe wangapi ?

Utaona kuwa majawabu yake moja kwa moja sio rahisi kupata takwimu.

Kwa maana hii kimakunduchi ni kabila ndani ya zanzibar kwa mujibu wa maelezo hayo hapo juu.

Lakini pili tunaambiwa wazanzibar wengi hasa kule pemba wana asili ya tanga.

Kama kuna wazenji wana asili ya tanga basi tanga kuna makabila.

Kuna wazenji wana asili ya omani basi omani kuna makabila.

Kama kuna wazenji wana asili ya saudia basi saudia kuna makabila.

Kama kuna wazenji wana asili ta tanzania bara basi tz bara kuna makabila.

Ushirazi sio kabila kwa sababu hakuna lugha ya kishirazi.

Washirazi wanazungumza kiswahili hivyo pengine washirazi lugha yao ikawa ni kiswahili,hivyo kishirazi ni kabila hewa ambalo halina hata lugha ya kuzungumzwa.

Shiraz asili yao ni waajemi kuna mji uko huko iran unaitwa shiraaz sijui kama ni lugha ama laa kwa huko.

Tufanye ni lugha.

Kama kishirazi ni lugha kwa nini mzanzibar ambae baba yake na mama yake wote ni waswahili wanaonekana alafu yeye anajiita mshirazi ?

Kuna kabila ambalo hurithiwa kiholela namna hii?

Yani kwa kuwa wewe umeenda arabuni(maybe saudia) ukakaa zako miaka kumi huwezi kuwa mkureishi hata kidogo.

Sote tunakubaliana kwamba watua weusi asili yetu ni africa na africa kuna makabila.

Ni jambo haliwezekani watu weusi wote pale zanzibar wawe washirazi.

Kuna rafk nagu mmoja yeye ni mshirazi ananiambia lakini kainipa stori yake anasema babu wa baba yake ni mtu wa kigoma,lakini yeye ni mshirazi.

Zanzibar makabila yapo sema tu walishatawaliwa na waarabu kuanzia ukabila wakafanywa kabila liwe ushirazi tu wale ambao walitoka tabora nao wakajiita washirazi bila kujua ni katika kutawaliwa wakatae makabila yao.

Nashangaa utakuta muunguja anakataa kabisa kwamba yeye hana kabila,sijui kaaambiwa ukabila una ubaya gani,alafu hapo hapo hajui kama waarabu wanaofuata tamaduni zao wana makabila yao kibao tu.

Naomba niishie hapa kwa kuanzia mengine tutajadili kwenye comment.
 
Mkuu safuher
Kwa mfano Mimi Ni mswahili lugha yangu kiswahili lakini Baba yangu Mzanzibari lakini asiye na kabila kati ya mmakunduchi,mkojani,mtumbatu Wala mnani je huyo utamwita ana kabila?
 
Mkuu wengine HAWAJUI MAKABILA YAO
 
Kwa hio wakaazi wa Unguja mjini wao watakuwa kabila gani?
 
Kila mmoja ana kabila lake.

Mjini unguja ni kama dar tu.

Dar kuna mkusanyiko wa wadigo,wahindi,wazaramu n.k

Pale mjini unguja kuna wamakunduchi,kuna waoman ambao kimsingi wana makabila huko,kuna wahindi ambao nao wana makabila huko,kuna wajambiani n.k

Kwa hiyo pale pana mkusanyiko wa makabila.
 
Mkuu safuher
Kwa mfano Mimi Ni mswahili lugha yangu kiswahili lakini Baba yangu Mzanzibari lakini asiye na kabila kati ya mmakunduchi,mkojani,mtumbatu Wala mnani je huyo utamwita ana kabila?
Usiseme hana kabila sema halijui kabila.

Kama humjui baba yako usiseme huna baba,baba yako yupo ila humjui.

Sio kweli kwamba baba yako ni mzanzibar asiye na kabila,kikubwa atakuwa halijui kabila lake.

Ukitaka ukweli mwambie akutajie babbu yake aliyemzaa asili yake wapi,na huyo babu baba yake asili yake wapi hapo utajua kabila lake na lako.

Ukisema tu kwamba hana kabila maana yake unaikata historia yako kuishia kwa baba yako kwa kuwa hajui kabila lake basi na wewe utasema hujui kabila.

Mimi binafsi kabila langu ni mmwera wa kusini,lakini sijui hata hiko kimwera,lakini siwezi kusema sina kabila ati kwa sababu naongea kiswahili.

Waunguja wengi hawataki kuchimba historia ya mababu zao kwa sababu wanajikuta wanaangukia katika makabila
 
Hakuna asiye na kabila whether ni wa nchi hii au kutoka nchi nyingine!
 
Back
Top Bottom