Sio sahihi Ward ya EBOLA kufunguliwa Temeke

Sio sahihi Ward ya EBOLA kufunguliwa Temeke

Nyamgluu

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2006
Posts
3,160
Reaction score
1,726
Raisi Kaenda leo kufungua wodi ya kupokea wagonjwa wa ebola TEMEKE !

Ugonjwa kwa sasa uko wapi, ukisoma distribution pattern yake, where is the most likely place kwa huu ugonjwa ku attack kwanza? Airport au mipaka yetu ya North West.

Halafa anasema hakikisheni maji yana flow vizuri sababu nimeona haya flow vizuri !

Mijitu imeshakula billions hapo!

Ah! At times hasira zinafanya ushindwe hata kujieleza!
 
Mkuu una hoja.Ila punguza kwanza hasira ili uweze kueleweka vizuri.
Nchi yetu sote hii,tukosoane katika namna ya kujenga na si venginevyo.
 
Hili li nchi hili *@&%~~(3;. kabisa!!
Kikwete ana shauriwa na nani? Siwezi kumlaumu yeye sababu uelewa wake naufaham. Sasa hio mijitu inayomshauri ni nani!!

Kaenda leo kufungua wodi ya kupokea wagonjwa wa ebola TEMEKE!!!!
Ugonjwa kwa sasa uko wapi, ukisoma distribution pattern yake, where is the most likely place kwa huu ugonjwa ku attack kwanza? Airport au mipaka yetu ya North West.
Halafa anasema hakikisheni maji yana flow vizuri sababu nimeona haya flow vizuri!!
Mijitu imeshakula billions hapo!

Ah! At times hasira zinafanya ushindwe hata kujieleza!

mkuu hata mimi Kikwete kanishangaza yani baada ya yeye ndio aelekezwe mambo ya kitaalamu kuhusu wagonjwa wa ebola watakavyo kuwa cared na miundo mbinu yote.
Badala yake nilichoona hapo temeke yeye ndio anawaelekeza wataalamu(madaktari) jinsi ya kuwahudumia wagonjwa wa Ebola.

Yani huyu jamaa analeta uswahili hadi kwenye mambo ya kitaalamu!!!!!
 
Wewe hujawaelewa....kwa viongozi wa nchii hii wilaya ya temeke ndio dampo la kila kitu kibaya....hawataki ebola ifike huko kwingine wanaipeleka temeke ili ugonjwa ukaue walalahoi huko.....wasikutane nao.....wakiweka ward airport na wao wanatumia airport itakuaje?
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
LabdaTemeke ndo yenye wageni wengi wanaoingia na kutoka!
 
Duh, kwa hiyo Mtu akipata Ebola huko Mpakani mwa nchi yetu na Kongo basi asafirishwe mpaka Temeke! Kwa nini wasijenge hiyo Hospitali huko kwenye uwezekano wa Ebola kuingia yaani Mpakani na nchi zenye huyo Mlipuko?


 
Kaka mkubwa anaingizwa chaka sana ila na yeye pia ana mapungufu yake ndio maana wadau wanampoteza ili wachukue chao mapema.
 
Mkuu una hoja.Ila punguza kwanza hasira ili uweze kueleweka vizuri.
Nchi yetu sote hii,tukosoane katika namna ya kujenga na si venginevyo.

Ok mkuu unajua nilikasirika zaidi sababu mimi ni mtaalamu katika tropical infectious disease control. Kilicho fanyika pale ni siasa tupu na hatari sana kwa Taifa na uji.nga sana.

Ngoja nikueleze tu kidogo kwa nini ni hatari. EBOLA ni a very highly infective virus. Yani kwenye kugrade level ya tahadhari ya kuchukua katika ku handle mdudu huyu scientist wanachukua tahadhari ya juu kuliko kitu chochote. Iko category 5 ya infection ambayo ndio highest.
Africa nzima kuna maabara 1 tu iliyopo South Africa ambayo ina kiwango cha usalama cha kuweza kuruhusiwa ku run research ya ya virusi kama EBOLA, hii ni kutokana na umahiri wake wa kuambukiza.
Nafikiri nawe umeona katika television yale masuti wanayovaa watu wa afya wanapoenda maeneo yenye EBOLA.
Pia umeona kifaa maalumu walichobebewa wazungu wale waliopata EBOLA kwenda kutibiwa huko kwao. Na kule kwao waliwekwa kwenye high quarintine rooms. Hivi vyumba ndugu vimejengwa mahususi kiasi ambacho hewa ilioyoko mle ndani haitolewi nje bila kuchujwa, maji yanayotoka mle hayapelekwi kwenye system ya kawaida ya maji na vitu vingine vingi kuepusha risk ya maambukizi.

Sasa kile kibanda alichoenda kufungua huyu rahisi wenu na kuwaambia ni wodi mahususi ya wagonjwa wa EBOLA hakiwezi hata kuzuia maambukizi ya TB. Na ni uji nga kuweka ile wodi sehemu yenye kadamnasi kama TEMEKE.
Hivyo kama ikitokea kweli akatokea mgonjwa wa EBOLA na mkampeleka pale Temeke, (Mungu epusha) itakua ndio mnapalilia maambukizi ya huu ugonjwa na kuukaribisha kabisa Tanzania kwetu.
Yani inaweza kutokea mlipuko huo ambao hamtaamini.
Kama basi ilibidi ijengwe wodi ya wagonjwa wa EBOLA cha kwanza ilitakiwa iwe karibu na mipaka yetu ya Kaskazini Magharibi, na mbali mno kutoka katika eneo lolote lenye watu, sababu hatuna ujuzi wala uwezo wa kujenga a quarentine ward katikati ya jiji kwenye mahopsitali yetu. Hili tu jamaa kaenda fungua halafu mabomba hayatoi maji!! Ingetafutwa secure isolated area ndio hio ward ijengwe.

Kujengwa kwa ile ward Temeke ni rahisi kutaka kuonekana ana jali na uongozi wake uko makini lakini ni uji.nga na hatari sana kwa Taifa letu. Tuache kuchanganya Siasa kwenye mambo ya kitaalm.
 
Back
Top Bottom