Sio siri, bila wapinzani Bungeni ghadhabu za Spika 'hazinogi' kabisa. Filamu zetu zinakosa mvuto

Sio siri, bila wapinzani Bungeni ghadhabu za Spika 'hazinogi' kabisa. Filamu zetu zinakosa mvuto

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,137
Reaction score
17,908
Wengi mnajua jinsi Spika Job Ndugai alivyokuwa 'akiwashughulikia' Wabunge wa Upinzani wakati ule wa Mwendazake. Alikuwa akitimiza agizo la 'kuwashughulikia' wapinzani ndani ya Bunge huku kazi ya kuwashughulikia nje ya Bunge ikifanywa kwa ustadi mkubwa na Mwendazake mwenyewe. Walengwa wakuu wamekuwa ni CHADEMA na Wabunge wao.

Kulingana na kikichotokea wakati na baada ya uchaguzi wa mwaka jana, CHADEMA 'haina Wabunge' katika Bunge la sasa. Ndiyo kusema, Spika hana 'targets' zake za kuzishughulikia. Ghadhabu zake zinakosa pa kujitokeza na kuzifaidi. Sasa ameamua kuanzisha maigizo yasiyo na maazigo.

Bunge la CCM yetu limefikia 'kuwashughulikia' wanaCCM wenyewe. Hakuna wapinzani wa kushughulikiwa. Inabidi tu kuwe na filamu ya Askofu Gwajima na Jerry Silaa. Wote hawa wana majimbo Dar es Salaam. Wote hawa wameonesha vituko kuelekea na mbele ya Kamati katika kuicheza filamu isiyotia hamu.

Askofu Gwajima alikataa kiti na kinasasauti. Akapata kiki yake. Jerry yeye alikataa kusindikizwa na askari kulekea mbele ya Kamati ya Maadili ya Bunge kwa kile alichokisema kuwa anajua anapokwenda na anazijua Kanuni za Bunge. Pia, akawasili na nyaraka na vitabu mujarabu vyenye majawabu yasiyo na tabu. Naye akatrend. Filamu ikaendelea.

Laiti kungekuwa na wapinzani Bungeni, Spika Ndugai angefurahi sana kucheza 'picha' zake na kutamka maneno yake mbele ya Wabunge. Angeonesha mabavu yake kwa kila mtanzania. Wapinzani wamekosekana. Sasa ni CCM dhidi ya CCM. Ni kama fisi kula fisi mwingine. Spika atakuwa anajuta kukosekana kwa CHADEMA Bungeni.

Askofu Gwajima hakamatiki?

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Mwanza Mjini)
 
Hakuna bunge pale zaidi ya 'sarakasi za ccm' ndio maana hakuna mvuto wowote mle.
 
Tunahitaji sana vyama pinzani, tunatamani wenye mapenzi mema kwa taifa letu wajenge upinzani wenye tija!!

Upinzani uwe na manufaa kwa wananchi na sio kwa viongozi peke yao....

Sio wale wa kutuyumbisha kwa kumkamata fisadi na kumstaafisha, na kisha fisadi huyohuyo akaweza kuwanunua kwa zilezile pesa za ufisadi wakamnunua na wakamsafisha

Kwa lile tukio hakuna mwenye imani na wale watu kamwe!


VUTA-NKUVUTE
 
Kweli majuto ni mjukuu, tumejaza watu wajinga waganga njaa kule ndani hawana msaada zaidi ya kupigania matumbo yao.
Watanzania tujitafakari sana ili 2025 tufanye maamuzi ya busara kwa mustakabali wa taifa hili.
 
Back
Top Bottom